Ina maana wasomi wote waungane kwenye chama kimoja?
elimu haitoshi kabisa, mfano, msomi wa Kenya na msomi wa Tanzania ni tofauti kabisa kwa kila kitu kuanzia uelewa, ujuzi, tabia na hata kipato. Wasomi wetu wanapenda kwenda nchi za Magharibi na Asia kwasababu mbalimbali zikiwemo zile za elimu, mikutano na ajira. Ule uzuri wa nchi zile vikiwemo mazingira, uchumi, siasa na sheria ni matunda ya wasomi wao. Hawa wa kwetu ni shameless, visionless, cowards, mistrustful, non persistence, cheap with shallow argumentative.
Siku zote na mara zote wanavisia faida ya leoleo inayowahusu wao na watu wao za karibu, wasipoiona wanachanganyikiwa. Hawajui kama historia inaandika neno kwa neno, tukio kwa tukio na tabia kwa tabia ya kila mfumo zuri au baya hata liwe dogo kama chembe ya haladari. Ndiyo maana historia haiwasahau akina Chifu Mangungo, Tiptip, Lumumba, Samora, Chipaka, Kambona, Bibi Titi, TAA, ZPPP, ZNP, TANU, Hitler, Hiroshima, Gadaff, nk