Aliyewashtaki viongozi wa kanisa katoliki (Lucy Antony) ashushiwa kipigo na watu wasiojulikana

Lucy Antony Michael (35), Mkazi wa Yombo Dovya, Mtaa wa Makangarawe, Wilayani Temeke, Dar es Salaam amevamiwa na watu wasiojulikana akiwa anatoka nyumbani kwake, ambapo watu hao walimpiga na kumshambulia maeneo mbalimbali ya mwili wake

Lucy ambaye ni miongoni mwa watu waliojitambulisha kuwa ni Waumini wa Kanisa Katoliki walioenda kwenye Ubalozi wa Vatican, uliopo hapa nchini kwaajili ya kupeleka barua ya malalamiko juu ya mwenendo wa baadhi ya viongozi wa Kanisa hilo hivi karibuni, amesema kabla ya kuvamiwa na kushambuliwa kwake kwa siku kadhaa amekuwa kwenye misukosuko ya kupokea simu na kutumiwa sms za kejeli, matusi na wengine kumtishia maisha

Akizungumza na Waandishi wa Habari akiwa nyumbani kwake leo, Jumapili Januari 11.2026, Lucy amehusianisha kushambuliwa kwake na maoni aliyotoa mbele ya Wanahabari kuhusiana na mwenendo wa baadhi ya viongozi wa Kanisa Katoliki, jambo ambalo ameeleza kuwa amelifanya kwa nia njema ya kujenga iliyolenga kuwarejesha viongozi hao kwenye mstari, maoni ambayo yamepokelewa kwa hisia hasi kwa baadhi watu kwenye jamii

Aidha, bada ya kushambuliwa Lucy amefikisha malalamiko yake kwenye Kituo cha Polisi Makangarawe na kupewa RB No. MAR/RB/49/2026

Shuhuda wa tukio hilo Sabina Michael, Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Ashura Salum na Daud Leonard ambaye ni mmoja wa waumini wanaosali pamoja na Lucy, kwa nyakati tofauti wameeleza kusikitishwa na tukio hilo sambamba na kuziomba mamlaka husika kuchukua hatua stahiki kwa wote waliohusika, huku pia wakiomba kuimarishiwa zaidi usalama mtaani kwao kwani matukio ya aina hiyo yanaweza kusababisha wasiwasi kwa jamii.

Pia Soma: Kundi la 'Wakatoliki' latinga Ubalozi wa Vatican Tanzania kumshtaki Askofu Ruwai'chi na Fr. Kitima
Miaka 35?

Mbona kanaonekana kapo 49 kuipenda ccm ni ugonjwa,mtoto mdogo anaonekana mzee hivi?
 
Ety Daudi Leonard ni muumini mwenzake wanaosali pamoja 😂 Ila mpaka sasa hatujui wanasali parokia ipi, hv hao waandishi hapo hakuna hata mmoja wa kuuliza swali simple kama hilo?
 
Ruwaichi angekataa kwamba hao siyo wakatoliki,tena wangoni akina komba kule ni ukatoliki tupu
 
Lucy Antony Michael (35), Mkazi wa Yombo Dovya, Mtaa wa Makangarawe, Wilayani Temeke, Dar es Salaam amevamiwa na watu wasiojulikana akiwa anatoka nyumbani kwake, ambapo watu hao walimpiga na kumshambulia maeneo mbalimbali ya mwili wake

Lucy ambaye ni miongoni mwa watu waliojitambulisha kuwa ni Waumini wa Kanisa Katoliki walioenda kwenye Ubalozi wa Vatican, uliopo hapa nchini kwaajili ya kupeleka barua ya malalamiko juu ya mwenendo wa baadhi ya viongozi wa Kanisa hilo hivi karibuni, amesema kabla ya kuvamiwa na kushambuliwa kwake kwa siku kadhaa amekuwa kwenye misukosuko ya kupokea simu na kutumiwa sms za kejeli, matusi na wengine kumtishia maisha

Akizungumza na Waandishi wa Habari akiwa nyumbani kwake leo, Jumapili Januari 11.2026, Lucy amehusianisha kushambuliwa kwake na maoni aliyotoa mbele ya Wanahabari kuhusiana na mwenendo wa baadhi ya viongozi wa Kanisa Katoliki, jambo ambalo ameeleza kuwa amelifanya kwa nia njema ya kujenga iliyolenga kuwarejesha viongozi hao kwenye mstari, maoni ambayo yamepokelewa kwa hisia hasi kwa baadhi watu kwenye jamii

Aidha, bada ya kushambuliwa Lucy amefikisha malalamiko yake kwenye Kituo cha Polisi Makangarawe na kupewa RB No. MAR/RB/49/2026

Shuhuda wa tukio hilo Sabina Michael, Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Ashura Salum na Daud Leonard ambaye ni mmoja wa waumini wanaosali pamoja na Lucy, kwa nyakati tofauti wameeleza kusikitishwa na tukio hilo sambamba na kuziomba mamlaka husika kuchukua hatua stahiki kwa wote waliohusika, huku pia wakiomba kuimarishiwa zaidi usalama mtaani kwao kwani matukio ya aina hiyo yanaweza kusababisha wasiwasi kwa jamii.

Pia Soma: Kundi la 'Wakatoliki' latinga Ubalozi wa Vatican Tanzania kumshtaki Askofu Ruwai'chi na Fr. Kitima
Lazima tuheshimiane. Anayesaliti nchi anastahili kusalimiwa!
 
Amesalimiwa kidogo.

Watu waache ukuda.
Tumsifu [Yesu Kristu..], Milele Amina.. ukurukuda ukizidi sana unatembelewa kichapo kitakatifu na zawadi unapewa.. maana hata Yesu aliwatembezea kichapo wale jamaa waliokua wakifanya biashara Hekaluni akawaambia "Nyumba yangu sio pango la wezi na walanguzi.." huku anawatembezea mkongoto mmoja mmoja piga sana..
 
Niliandika hapa huyo mdada apatiwe ulinzi wa kutosha maana alichokifanya ni hatari kwa maisha yake. Haiwezekani akatumika kutifua taasisi ile nyeti halafu waumini wake wakamuacha azagaezagae kiholela vile huku sio hata muumini wao. Ile ishu ya kutumiwa ni hatari lazima upewe ulinzi muda wote
 
Lucy Antony Michael (35), Mkazi wa Yombo Dovya, Mtaa wa Makangarawe, Wilayani Temeke, Dar es Salaam amevamiwa na watu wasiojulikana akiwa anatoka nyumbani kwake, ambapo watu hao walimpiga na kumshambulia maeneo mbalimbali ya mwili wake

Lucy ambaye ni miongoni mwa watu waliojitambulisha kuwa ni Waumini wa Kanisa Katoliki walioenda kwenye Ubalozi wa Vatican, uliopo hapa nchini kwaajili ya kupeleka barua ya malalamiko juu ya mwenendo wa baadhi ya viongozi wa Kanisa hilo hivi karibuni, amesema kabla ya kuvamiwa na kushambuliwa kwake kwa siku kadhaa amekuwa kwenye misukosuko ya kupokea simu na kutumiwa sms za kejeli, matusi na wengine kumtishia maisha

Akizungumza na Waandishi wa Habari akiwa nyumbani kwake leo, Jumapili Januari 11.2026, Lucy amehusianisha kushambuliwa kwake na maoni aliyotoa mbele ya Wanahabari kuhusiana na mwenendo wa baadhi ya viongozi wa Kanisa Katoliki, jambo ambalo ameeleza kuwa amelifanya kwa nia njema ya kujenga iliyolenga kuwarejesha viongozi hao kwenye mstari, maoni ambayo yamepokelewa kwa hisia hasi kwa baadhi watu kwenye jamii

Aidha, bada ya kushambuliwa Lucy amefikisha malalamiko yake kwenye Kituo cha Polisi Makangarawe na kupewa RB No. MAR/RB/49/2026

Shuhuda wa tukio hilo Sabina Michael, Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Ashura Salum na Daud Leonard ambaye ni mmoja wa waumini wanaosali pamoja na Lucy, kwa nyakati tofauti wameeleza kusikitishwa na tukio hilo sambamba na kuziomba mamlaka husika kuchukua hatua stahiki kwa wote waliohusika, huku pia wakiomba kuimarishiwa zaidi usalama mtaani kwao kwani matukio ya aina hiyo yanaweza kusababisha wasiwasi kwa jamii.

Pia Soma:
Hii sura sio ya kikristo kabisa! Hafananii kabisa kuunyenyekea msalaba.
 
Back
Top Bottom