Kwa jinsi ulivyo elezea unaonekana na wewe ni mwenzao sema wamemurusha ndo maana umekuja kuwachomesha.Hakuna ufala kama masikini kumwibia masikini mwenzie..siku zote ukiona utapeli unafanyika na usiposema juu ya utapeli huo jua na wewe ni tapeli.
Yaani hadi inatia hasira, kwanini vijana wa siku hizi hatuna ufuatiliaji wa mambo, unaambiwa kuhusiana na Kampuni usiyoifahamu vyema kama msomi na mkononi una simu janja kazi kufuatilia stori za mwijaku na baba levo, unashindwa kuingia Google uandike Alliance Global utapeli uone kama utapata walahu dondoo kuhusu experience za users i.e kwenye Google kuna makala ya gazeti la Mwananchi kuhusiana na utapeli wa Alliance Global huko Kilimanjaro n.k, Umeshindwa huko basi pitia Jamii Forums, Haya tuseme facebook ingia search andika Alliance Global moja kwa moja itakuijia video ya makala ya Ripoti Maalum kutoka ITV..June 15, 2022 kuhusiana na matukio ya hawa matapeli n.k
Hawajibu maswali wale
Walichoniambia ni kuwa hilo swali atakujibu aliyekuleta.
Nikawaambia atanijibuje huyu wakati yeye bado sio mnufaika wa hii biashara kama nyinyi.
Hamuoni kama naye huyu yupo hapa kujifunza na moja ya sababu za kumfanya atoe hela ni pale anapokuwa hana mashaka na hii biashara.
Na mashaka yetu yanahitaji majibu mazuri kutoka kwenu ili yaweze kuondoka.
Hawakujibu kitu wakanisisitiza nije semina ya pili nitapatiwa majibu nikaamua kuwapotezea.
Wezi wale bora jamaa alisanuka mapemajamaa yangu aliitwa na wale jamaa wanajiita Qnet 2018[emoji28][emoji28]akapigwa seminar ya kutosha kwa maelezo yake anasema aliwaelewa kabisa,kimbembe kikawa kiingilio.
anasema aliporuhusiwa kuuliza swali akiwa tayari na goosebumps akauliza,sasa bro si unikope hiyo 5mln niingie then baada ya mwezi nikianza kuingiza $$$$ unakata percent yako mpaka hela yako irudi[emoji28][emoji28],jamaa akamjibu kwa swali,kwani hakuna hata sehemu unaweza kukopa au hata kuuza mali uliyo nayo ukapata hiyo hela???
mwamba kwa swali hilo akili ikafunguka,kumbe lengo hapa ni hii 5mln yangu sio mimi nifanikiwe,akaaga na kusepa[emoji23][emoji23]
Vanilla Vanilla Vanilla 😬Bongo kweli nyoso..bongo balaa![emoji124][emoji124][emoji24]
Vanilla kilo 1 = 1,000,000Wezi wale bora jamaa alisanuka mapema
Wizi, utapeli na/au dhulma ni vibaya sana bila kujali kuwa umtendeaye ni masikini au tajiri.Hakuna ufala kama masikini kumwibia masikini mwenzie..siku zote ukiona utapeli unafanyika na usiposema juu ya utapeli huo jua na wewe ni tapeli.
Afu hawa bado nawasikia kwenye kipindi cha michezo cha Wapo Radio wanaendelea kufanya promosheniVanilla kilo 1 = 1,000,000
Aisee tutafika mbinguni tumechoka sana na hawa matapeli uchwara[emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Hapo kahsaletwa mrembo mkaliii anakokota begi
Eti katua kutokea Ohayo Missouri kwenye maonyesho na kilele Cha mafaniko ya bidhaa na testimonies za watu mashuhuli..... Eti huyo ndio yule tulikuwa tunaongea nae akiwa kwa Flight ameunga kuwawahi ..me mbavu sina.[emoji23][emoji23]
Nitaanzisha Uzi wa kutaja makampuni yote ya Kitapeli.hata universisty abroad ya mtu anaitwa Tonny ya kupeleka wanafunzi nje ya nchi ni matapeli kuliko matapeli wote duniani mshenzi sana huyo TONNY na genge lake ofisini
Kuna motivation spika mmoja enzi hizo nilikuwa natoka na sista'ake, hivyo kila day akosi kuja kumpiga dada mtu mizinga ya mafuta kwa ajili ya gari lake na kila day mchana na jioni lazima aje kula, sasa siku moja nipo na washkaji tumeongozana sikujua mara moja wanaelekea wapi nikawafata tu, saa ngapi wasizamie kwenye ukumbi fulani wakaniambia kuna mchongo mmoja wa fursa za pesa upo mahali hapo tusikilizie,Ahahaha na wabongo tunavyoamini mtu anae miliki Gari ndio mwenye pesa na tajili lazima watu walizwe [emoji848] watu wanacheza na akili tu
Sent from my A37fw using JamiiForums mobile app
Ni kweli mkuu, katika dunia hii ya sasa siyo kila fursa ni fursa kuna fursa zingine wewe ndiye fursa yenyewe.[emoji23]Unavyoitwa kwenye fursa wewe ndio fursa watu hawaitani kwenye hela aise
Hakuna siri ndugu yangu hapa duniani hata ungefanyia uvunguni bado watu watajua tu, kama ungekuwa makini stori yangu inamwelezea dada mmoja aliyetaka kuingizwa mjini kupitia mchezo huu wa kitapeli na nilichokielezea chote nimesimuliwa na huyo dada na nilimsindikiza mpaka eneo la tukio bila kusanukiwa na matapeli, na nikamwelekeza chakufanya aende tu kuwa-enjoy kama vile haelewi chochote kisha aniletee data za kinachojiri huko ukumbini.Kwa jinsi ulivyo elezea unaonekana na wewe ni mwenzao sema wamemurusha ndo maana umekuja kuwachomesha.
Malipo ni hapa hapa ndugu yangu
Ni kweli kabisa, vijana wa kisasa nowdays tunatumia interneti vibaya sana, yaani muda wote MB's zinateketea kuangalia video za ovyo (maselebu, pono, michezo,vichekesho)TikTok, facebook, X na instagram, kutwa nzima huna hata site moja uliyoitembelea kujihabarisha au kujinoa ufahamu matokeo yake unakuwa msomi mwenye stupidity ya hali ya juu na matokeo yake ni kukumbana na hakina Alliance Global.wanasema mwafrica ukitaka kumnyima maarifa yaweke katka mfumo wa maandishi.
fikiria ndugu yetu huyu katoa elimu kupitia JF,kuna kirundu amekaa sehemu na ana degree hajui hata JF ni kitu gani[emoji28][emoji28][emoji28].
yaani huyu ni mhanga ajaye wa Alliance Glabal mpya yenye jina jingine lakini lengo likiwa lile lile kupiga mazezeta.watu hawako aware kabisa na hivi vitu wanaishi kama maiti.