Ally Kamwe msemaji wa Yanga afungwe break, Haya sasa Mzee wa watu kakujibu kiutu uzima

Kakosea
Ameomba radhi
Yameisha
Ni utani wa jadi tu mtu hachaguliwi Cha kutaniwa Wala sio tusi
Yanga na Simba Ni watani wa jadi
Utani hauchagui mtu, jinsia, Wala Rika
Au nyie Makolo mseme hadharani Kama hamtaki utani
Young Africans
Bingwa cafcc
Mkuu ww ni show Gah na unatafunwa nyuma...... HAHAHAHAA USIHOFU MKUU SISI NI WATANI WA JADI
 
Halafu utasikia vijana hatuna ajira, wakipewa wanaharibu kama hivi.

Enzi za JPM aliwaamini vijana akawapa nafasi lakini mambo ndio kama haya. Hao wazee waendelee tu kukaa madarakani.

Sio wote ila wengi hatujui mipaka yetu. Binafsi angemtania Ahmed Ally ningemuelewa matani ya ujana na wale wanajuana.

Huu usemaji wa vilabu ni kacheo flani hakana maana yoyote, kwa mpira ulipofikia sasa hivi.
Huu usemaji unakuwa timamu ukiwa nje ukishaingia ni kama unapewa vidonge vya kufyetua akili.
 
Ally Kamwe aombe radhi kwa huo ujinga
 
Vitu vingine ni vya kawaida na watu kutaka kukuza Jambo tu....!, Kipindi manara yupo Simba alivyosema yanga wenye akili ni 2 Kuna aliyemwona kakosea?.
Ahmad Ally majuzi Kati alitamka watu wa Yanga ni sawa na MAITI Kuna aliyemnyooshea kidole?, Utamaduni huu wa kipuuzi umeasisiwa na watu wa Simba. BTW kwani mbona aliyesema Andazi ni bora kuliko CCM hajaonekana kuwa na dharau kwa CCM na Rais wa Nchi?.
 
huo ndio utani wa jadi wenyewe, haina tofauti na aliyebeba jeneza kuingiza uwanjani.
 
Mgunda kaongoe maneno mazito sana. Kwani Ali Kamwe alianza vipi hadi kufikia kwa Mgunda? Mbona mechi ni Yanga vs USM Alger na bora hata angekuwa kamtupia madongo Ahmed Ally tungesema labda karudisha madongo. Sasa huyu baba wa watu kamuanzia nini?
Ukisha kuwa mke wa boss unasahau majukumu yako, unaona ushavuka level za kazi yako.
 
Muulize Manara atakuambia alivyopelekewa moto na Karia baada ya kuchutama.

Kuna muda namna nzuri ya kumfundisha mtu ni kupitia adhabu. Sio kila kichwa kina uwezo wa kujifunza kupitia msamaha. Ukifuatilia mfululizo wa matamshi ya huyo jamaa utagundua sio msamaha unaomfaa.
 
Katika watu ambao kabla ya kuongea napima maneno yangu ni watu wazima.

Hawa watu wazima wamepita vingi na wameona vingi bado tuna mengi ya kujifunza kwao..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…