Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
Thanks. Acha wafu wazikane wao kwa wao.Kwani wanaompinga Magufuli ni wapinzani!? Bulembo mpinzani?, Makamba mpinzani!? Samia anayeponda falsafa za Magufuli ni mpinzani!? Nape mpinzani!? Wapinzani wa Magufuli wa kweli ni wenzake wa ccm waliokuwa wanangoja afariki, chama kirudi kwa wenye nacho kama Nape alivyosema.
Huu utamaduni wa kishenzi una mizizi ndani ya CCM. Ni mapambano ya ndani kwa ndani: uncivil civil war. Wapinzani nao wamejeruhiwa na kusemewa mbovu. Leo Lissu anaitwa mlemavu kwa kejeli! Ni vigumu sana kutarajia ustaarabu katika mazingira haya - selectively.
Wastaarabu watabakia kuwa wastaarabu. Lakini endapo siasa za kishenzi zitaendelea kuzawadiwa na walioshikilia dola, wasema ovyo watazidi kuongezeka. Malalamiko yatakuwa suala la zamu.