Ambao wameoa mwanamke daktari naomba kujua raha na karaha

Ambao wameoa mwanamke daktari naomba kujua raha na karaha

Bado hajaolewa

Sikutaka kupasha naye kiporo maana aliniambia anataka kunibebea mimba, kwa Uzee huu nisije kumaliza pension yote kusomesha mtoto wa Uzeeni 🙌
Sasa pensheni unataka kufanyia nini mkuu? Maana hata hela ya pensheni hawashauri kujengea wala kununulia gari, wanasema ndio wakati mzuri kutembea kwa miguu kwa wastaafu.
 
Sasa pensheni unataka kufanyia nini mkuu? Maana hata hela ya pensheni hawashauri kujengea wala kununulia gari, wanasema ndio wakati mzuri kutembea kwa miguu kwa wastaafu.
Unataka hela ya Pension nitumie kilipia Ada watoto wa Uzeeni badala ya kuitumia kula maisha

Tuoneeni huruma Wazee 🤗
 
Wengi wana swing mood jiandae na makwazo yasiyoisha kutokana na stress za kazi. Simu unapiga hazipokelewi kwa wakati, sms ndio kabisa ukilalamika utaambiwa una gubu jiandae kutukanana kila wakati.
sasa na wewe mwenyewe lazima ujiongeze unapigaje simu muda wa kazi na unaijua kazi yenyewe, ameletwa mgonjwa na ambulence atapokea simu hapo?
 
Unataka hela ya Pension nitumie kilipia Ada watoto wa Uzeeni badala ya kuitumia kula maisha

Tuoneeni huruma Wazee 🤗
Hao ndio wa kuwahudumia sasa maana hao wanatakuwa bega kwa bega wakati ambao hautakuwa na nguvu maana wakubwa wote watakuwa kwenye familia zao na majukumu yao. Watoto wa uzeeni huondoa upweke wa nyumba kipindi ambacho nyumba nzima mpo wawili au mmoja.
 
Nitacheza na Wajukuu zangu tu, suala la kuambiwa ada za watoto ni milioni 7 Kwa Mwaka wakati huo unakuta mtoto yupo darasa la 4 na muda huo pension yangu ya Mkupuo ni milioni 178 sio poa kabisa 😜🙌
 
Habari za muda huu, kama kichwa cha habari kinavyoeleza, naomba kujua changamoto za kuoa mwanamke ambaye ni daktari kabla sijachukua maamuzi, daktari nikimaanisha Medical Doctor (MD).

Karibuni
IQ yako imzidi.
 
Wengi wanajiona matawi sana, so elimu yako na yake visipishane sana..otherwise utapata shida kidogo.
Kipato chako kiwa cha kueleweka, ikibidi kiwe kikubwa zaidi, itakupa kujiamini zaidi mbele yake.
Hakikisha una plan B ya kulombana, kuwekwa pending yaweza kuwa desturi.

Kuna careers zinajiona beyond heaven, MD ni mojawapo.
 
Wengi wana swing mood jiandae na makwazo yasiyoisha kutokana na stress za kazi. Simu unapiga hazipokelewi kwa wakati, sms ndio kabisa ukilalamika utaambiwa una gubu jiandae kutukanana kila wakati.
Hili la simu kutopokelewa ni 100% , ukienda na mapenzi ta njiwa yale ya kila muda kuchati na kuongea ni lazima ujione yatima.

Otherwise, ni binadamu kama wanawake wengine na ugumu au urahisi wa mahusiano siku zote hutegemea kiwango cha upendo kati yenu na sio kazi au occupations.
 
1. Kwanini uoe mwanamke aliyekuzidi cheo/ pesa?
2. Kama una wivu, kwanini uoe mwanamke ambae anafanya kazi zenye shift za usiku?
3. Kwanini uoe mwanamke ambaye una mashaka naye hata kabla hujamuoa?
 
Wakati wewe kila ukimuangalia unafurahia taswira ya sura na umbile lake maridhawa; Yeye akikuangalia anaona hadi taswira ya skeleton yako! (cartoon joke).
 
Back
Top Bottom