Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ambwene Yesaya (A.Y), ameeleza mtazamo wake kuhusu mjadala wa “mdundo wa taifa” katika mahojiano na kituo cha redio cha East Africa Radio, Aprili 10, 2026 akisisitiza kuwa muziki hauwezi kulazimishwa kuwa na mwelekeo mmoja bali hujijenga na kukua kiasili.
AY amesema kuwa mdundo wa taifa hauwezi kutengenezwa kwa kukaa na kupanga, bali hujitokeza wenyewe kadri muziki unavyoendelea kukua na kubadilika. Ameeleza kuwa hata katika nchi nyingine, mitindo ya muziki hujitofautisha bila kulazimishwa, akitolea mfano jinsi muziki wa Bongo Fleva unavyotambulika kirahisi unapopigwa nje ya Tanzania.
"Sisi wote tukae hapa tutengeneze mdundo wa taifa? No, vitu vina-elevate vyenyewe, vinajipika mpaka vinafika."
"Ukienda Kenya, ikipigwa unajua hii ni Bongo Fleva, huu ni muziki wa Kenya... kwahiyo ina-blend hivyo."
"Kilichoniuma ni kwamba tunaacha hivi vitu vyetu vya Bongo Fleva, tunaanza kukimbilia kwenye haya manini... huwezi, labda nitoe mfano mmoja wa kucheza drafu; mimi nikikaa nje naona zaidi kuliko wewe unayecheza."
"Sisi kwa sababu Bongo tuko hivi hivi, ‘ah nyie si mnaiga wapi sijui nini’, ukienda nje ndio unajua tofauti ya Bongo Fleva na muziki mwingine."
"Hata ukiangalia albamu ya kwanza ya kina P-Square, walikuwa wanaiga iga, halafu kukaja wakati wakawa wanaiba nyimbo za Congo kidogo hivi, wakaja kwa Nigeria... lakini sasa hivi si wamekaa tayari kinigeria kabisa? Kwahiyo mdundo wa taifa mimi honestly naonaga haiwezekani."