Amejenga hii bila mkopo wa benki, ilimchukua miaka nane kumaliza

Unaacha legacy kwa wanao na ndugu wa karibu.
Ila kweli uko sahihi..alaf sky unapenda mambo ya ujenzi bila shaka unafanya kazi kwenye hi sekta.mimi kiukweli bado sijapata wazo la kujenga.. wastan wa kipato changu kazin kwa mwaka NI million 12-15 basic salary + field rate included.. good news Sina wategemezi ila TU sijui kwanini sifikirii kujenga
 
Kuna wanaojenga kwasababu wanalipa kodi ya pango kubwa sana, binamu yangu alijenga nyumba mara baada ya kuanza kazi baada ya kuishi kwa ndugu kwa manyanyaso. Ukiwa kwenye comfort zone si rahisi kuwaza kujenga.
 
Kwa mshahara huu, unachukua mkopo kununua kiwanja, unajenga banda ili kulinda kiwanja. Nyumba kubwa unajenga ukilipwa mafao ya kustaafu.
Usipostaafu? Madame hatuna mkataba na Mungu

Nashauri kufanya yaliyo ndani ya uwezo wetu ili tufanye kwa muda na tufaidi tulichofanya

Nyumba yangu nimejenga ya kawaida kwa mwaka mmoja na mwaka huu nitafanya finishing kwa mkopo ili niishi

Sasa kujenga miaka 12 boonge la jumba huku ndani ya miaka hiyo unalipa kodi ambayo ungeifanyia jambo jingine kwa miaka 10 uliyookoa kwa kujenga miaka miwili. Na unaanza kuishi ukiwa huna fahari yoyote maana ujana ndio umejaa fahari uzee unawaza makazi mapya mbinguni ama akhera

Pengine ukafa kabla haijaisha
 
Mtu anaejenga apartments mara nyingi ni kwa biashara na ana makazi yake ya kuishi. Huyu bwana amejenga apartments 12, akipangisha kwa laki tano kila moja ana milion 6 kwa mwezi. Akizitunza nyumba vizuri hii ni cash flow mpaka mauti yanamkuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…