Amejenga hii bila mkopo wa benki, ilimchukua miaka nane kumaliza

Amejenga hii bila mkopo wa benki, ilimchukua miaka nane kumaliza

Kuna wanaojenga kwasababu wanalipa kodi ya pango kubwa sana, binamu yangu alijenga nyumba mara baada ya kuanza kazi baada ya kuishi kwa ndugu kwa manyanyaso. Ukiwa kwenye comfort zone si rahisi kuwaza kujenga.
Hii sio sahihi. Mtu anakufadhili. Ukifanikiwa ukaondoka yanakuwa mafanikio. Anakukisha, unalala, si ajabu anakupa na nauli. Mwisho wa siku manyanyaso.
 
Mmoja aliniambia biashara yake ni mboga mboga, amejenga green house na analima hizi mboga zinazoliwa kila siku, mfano nyanya, carrots, hoho. Kila siku anapeleka mzigo wa laki nne sokoni.
Mwambie akuambie na ambayo hajakuambia
 
Mwambie akuambie na ambayo hajakuambia
Eka tano za mboga mboga zinaweza kukuingizia laki tano kwa siku.

Uwe na miundo mbinu ya umwagiliaji; kusima, pump, utandaze mabomba.

Ajira viabarua watatu kwa 10,000 kila mmoj kwa siku. Wale shift, wawili waanze 12 asubuhi kuchuma mboga na kuziweka kwenye ndoo.

Unahitaji pick up ya kupelekea mazao sokoni. Unapack ndoo 12-15 za mboga mbali mbali.

Ukishachukua mauzo kumbuka kuacha laki mbili bank kila siku.

Ukifika mafanikio hata ya, ajiri afisa kilimo akupe ushauri wa magonjwa na tiba za mazao. Unaweza kumlipa kati ya laki 3-5.
 
Kwa mshahara huu, unachukua mkopo kununua kiwanja, unajenga banda ili kulinda kiwanja. Nyumba kubwa unajenga ukilipwa mafao ya kustaafu.
Unastaafu, unachukua mafao, unajengea nyumba, unahamia, hela imeisha, unakosa ya kununua chakula, unaomba majirani chakula, wanakuchoka maana unaomba sana, wanakuwekea sumu, unakufa.....
 
Unastaafu, unachukua mafao, unajengea nyumba, unahamia, hela imeisha, unakosa ya kununua chakula, unaomba majirani chakula, wanakuchoka maana unaomba sana, wanakuwekea sumu, unakufa.....
Kama hali yako ni mbaya kiuchumi unabaki kwenye nyumba ya nyuma hii ya mbele unaweka mpangaji. Kwasababu kiwanja ulinunua muda mrefu eneo hilo litakuwa limesha changamka.
 
Back
Top Bottom