Si kweli,changamoto nikua kuna kundi limeaminishwa kua bila wazungu atuwezi kutatua matatizo yetu mfano ya utawala,uchumi nk. Nawaogopa sana watu wanaoshadadia kua Bunge la Ulaya,Marekani sijui mambo gani eti wanapitisha azimio... yaani kana tuenda shule kusoma ujinga. NAWASHANGAA WATU WASIOJUA MADHARA YA NEO-COLONIALISM.. Tunao uwezo wa kutatua changamoto zetu kiuhalisia achana na hizi zinazo kuzwa kwenye mitandao
Na tatizo lako umekaririshwa historia ya darasa la tatu na nne kuwa NEO COLONIALISM ni sharti ifanywe na wazungu (watu weupe) tu...
Hata hujui kuwa wapo weusi wenzetu wachache ni washenzi na wana tabia zilezile kama walivyokuwa makaburu na wakoloni wengine nyakati zile hapa Afrika...
Hivi fikiri hili...
Kwani mauaji ya 29/10/2025 ya maelfu ya watoto, kinamama na kinababa ili weusi wenzetu wachache, wenye tamaa ya madaraka wapate madaraka ya utawala kwa gharama za damu za weusi yalifanywa na wakoloni wa kizungu kwani au weusi wenzako kabisa hawahawa unaowaona binadamu lakini kumbe ni wanyama
Bishweko?
Na kwa taarifa yako ni kuwa, hata katika karibu miaka 80+ ya utawala wa wakoloni Wajerumani na Waingereza (wazungu), hawa jamaa weupe (wazungu) hawakuwahi kuua watu wengi namna hiyo kwa wakati mmoja na ndani ya siku 2 tu ili kulazimisha utawala wao wa kikoloni...!!
Lakini Samia Suluhu Hassan (mweusi mwenzio) aliweza kufanya hivyo kwa siku 2 tu akaua watu hovyo mitaani kwa maelfu eti ili yeye na CCM yake watawale..!
Hizo ndizo akili za watu unaodai wanaweza kutatua mambo yao wenyewe bila msaada wa watu wenye akili zaidi kuliko wao...
Nasema hili kwa sbb akili ya kuua wanadamu wenzako ili eti upate madaraka na mamlaka ya kuwatawala wananchi uliowaua, hizo sio akili bali ni matope 100%...
Jingine ni hili..
Kwamba inawezekana vipi Samia Suluhu Hassan na weusi wenzake huko CCM anashindwa kuwa mkweli tu katika jambo dogo kabisa linaloitwa "maridhiano", badala yake wanajaribu kutumia ujanja ujanja, ulaghai ulaghai kwa kurubuni wengine kwa rushwa na hongo ili washiriki kwenye ulaghai wao lengo likiwa ni kufunika udhaifu na maovu yao badala ya kukiri makosa na kuyatubia...?
Unadhani watu hawa wana akili sawasawa za kufanya mambo mazuri pasipo msaada wa watu wengine wenye akili zaidi kuwazidi wao...?