Ameniomba Msamaha lakini ameniwekea Masharti

1. Nisubiri nikomae 2. Sijui kipi kitangulie 3. Nina ubinafsi 4. mchumba wangu ni hamnazo 5. sijajiandaa kuwa na familia 6. jambo dogo kama hilo linanishinda
Toa ushauri ili nisiendelee kuwa katika haya unayoyafikiria kuwa yapo

1. Nimekupa ushauri kuwa usubiri Kwanza ukomae,

2. Ujue nini maana ya Familia.
Mkeo ndio wewe, Watoto wenu ndio matunda yenu. Ni lazima uwe na upendo na uweze kulinda familia yako Kwa gharama yoyote.

3. Usichopenda kufanyiwa usimfanyie mwenzako. Tafsiri yake Acha Ubinafsi.
Fikiria wewe ndio umetoa taarifa kwenu kuwa kuna Mchumba atakuja umtambulishe, Ndugu wote wanajua na pengine wamejiandaa, alafu mwisho wa siku huyo Binti anakuambia amepata ushuru, unaulizia udhuru gani ukitegemea taarifa ya maana, ATI demu wako anakuambia sijui rafiki yake kapata matatizo, utamuelewa?

4. Kuomba Msamaha ni dalili ya MTU anayejitambua, mwenye upendo, anayejali na MTU mnyenyekevu kuwa amekosea.
Kama huwezi kuomba Msamaha ATI mpaka uambiwe sijui ubembelezwe hiyo ni dalili ya kutojitambua, uchanga na kutokukomaa.

5. Kuwa mwanaume ni kuwa na Akili.
Kuiona Jana na Leo kisha kuikadiria kesho(maono)
Sio kila Jambo uombe ushauri, ni dalili kuwa Bado Akili yako haijaweza kujisimamia na huna uwezo wa kuwa Baba.

Kumbuka ukiwa Baba, Mkeo ataitegemea Akili yako kutatua matatizo yake na familia.
Sasa kama Akili haijakomaa Mkeo atapata wapi wa kumtegemea kimawazo?

Mwisho, usidhani nimekukandia, Ila najaribu kuongea Kwa Lugha Kali ili upate uchungu uweze kunielewa kirahisi
 

Mada yako Ipo kwenye mrengo Hasi, na chanzo cha uhasi huo ni mhusika wewe ndani ya hicho kisa.

Wewe ndiye umemkatili huyo Binti.

Sasa ukiambiwa ukweli unaona kama tunamitazamo hasi.
Wewe kama huna Mtazamo Hasi, nini kinakushinda kwenda kuomba Msamaha mpaka uite Jambo hilo ni masharti ya huyo Mchumba wako?
Jambo ambalo Kwa MTU mwenye Akili wala asingesubiri kuambiwa akaombe Msamaha kwani angeenda mwenyewe.

Acha Ubinafsi
 
Hujanikandia, unaeleza mtazamo wako, ambao, kwa namna yoyote si sheria kwangu wala jinsi nilivyo. Utabaki kuwa mtazamo wako. Uhalisia uko hivi, akili yangu nii komavu sana. Leo yangu na kesho yangu imeshabarikiwa sana kiasi nisichoweza kueleza. Siombi msamaha kwa jambo mtu analolisababisha mwenyewe. Ninawajibiika kuomba msamaha kwa kile nilichokisababisha mimi. Ukinielewa vibaya ukafanya maamzi mabaya na ukategemea mimi nikuombe msamaha, haitaweza kutokea. I have to close this case. Sitaomba msamaha na yeye asubuhi hii namjulisha kwamba sitaweza kuendelea na hayo mahusiano. Tuendelee kushauriana kwa manufaa ya wengine pia.
 
"Mtu mwenye akili",,,labda useme mtu mwenye huruma. Wenye akili hawapo hivyo!
 
Hatujamponda kwa kuwa amemsaidia rafikiye,tumemsema kwa sababu ya kutotoa taarifa ya kuahirisha jambo aliloahidi hata pale baada ya mchumba wake kususa angetakiwa atume wazee watoe taarifa kule ukweni,but unfortunately hakufanya hivyo
 
Hii duuu kwenye
Ni kweli ulikosea. Ushatoa ahadi unaenda kutoa mahari, alaf unapotelea mitini, lazima uwatake ladhi, lakini ujielezee.
Jibu zuri kama hilo

Inaonesha upo kwenye makundi ya watu wasiopenda kujishushaπŸ˜…
Kama unamtaka ni vyema na busara kugusia kwa nini ulikwama na una malengo na binti yao, endapo walifikiri vingine ikawaudhi, unawaomba radhi
 
Kuna jambo nature ilitaka kukuokoa lakini huelewi somo
 

"Miezi michache iliyopita, nilitengana na mwenzi wangu wa muda mrefu baada ya kusitisha kuota mahari nyumbani kwao na kuamua kumsaidia rafiki yangu ambae alikuwa kwenye changamoto fulani za kimaisha"

Embu soma hayo maelezo yako, afu uone Nani kakosea baina yako na huyo Mchumba wako.

Hujui kuvunja ahadi ni moja ya Usaliti?
Ushamuahidi mtoto wa Watu alafu unakuja na visababu uchwara visivyo na kichwa na miguu.

Ungekuwa na Akili ungefanya moja ya mambo haya;
1. Ungetakiwa kuomba Radhi
2. Ungetuma Wawakilishi kule ukweni.

Afu ushasema ni Mchumba wako WA muda mrefu, kumaanisha kama MTU mwenye Akili unayejua thamani ya muda na mahusiano, usingeweza fanya kitu kama hicho.

Ni Sawa na MTU mjinga ambaye amekaa kwenye mahusiano Kwa miaka 10 alafu ndoa au mahusiano yake yavunjike ati Kwa kushindwa kusema neno "Samahani" lenye silabi nne.
Ni MTU mjinga tuu asiyejua anataka nini kwenye Maisha..
 
namjulisha kwamba sitaweza kuendelea na hayo mahusiano.
Wewe ndo ulimuambia unamkaribisha akijiona anakuhitaji. Anyways, mpige chiniβ€”ni Sawa kwa sababu hakusikiliza na kuchukua 50 zake,
Ila pia unaweza kuwa romantic na kumwambia β€œmpenzi, you should have listened, anyways, wazazi wamekasirika, nakupenda sana, nitajua la kufanya”

Unaenda siku ya kutoa mahari, unaelezea situation na kutoa samahani kama angalizo tu la endapo walichukia
 
"Mtu mwenye akili",,,labda useme mtu mwenye huruma. Wenye akili hawapo hivyo!

Wakuonewa huruma hapo ni wewe πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Sisi wazoefu WA mapenzi tunajua nini kinafuata kwako kwenye ishu za mahusiano.

Kesho kutwa hapa utakuja kuwatukana Wanawake ni Mbwa,
Nipo nimekaa hapa
 
Omba msamaha kwa kutoka nje ya muda,peleka hela za watu. Usichelewe ukikutana na jamaa wanaopinga hili jambo unaweza ukashawishiwa ukaghairi kabisa
 



Nimemuambia naona anakaza Fuvu.
Ni mbinafsi Sana.

Mimi ningemshauri huyo Bibie amuombe Msamaha mshikaji kisha ampige tukio litakalomfurahisha.
Huwaga wengine hatumalizagi mambo yetu ubao ukionyesha tumepigwa
 

Kama umekosea Kwa nini usiombe Msamaha?πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Au haujiamini?πŸ˜€πŸ˜€
Kuomba Msamaha sio kujidhalilisha Mkuu. Acha mawazo potofu ya Watu wajinga na wenye ushetani
 
Ila huyo mwanamke hana akili pamoja na kumuaibisha bado kajileta mfyuu zake
Mapenzi mkuu. Husababisha upofu. Majuto ni mjukuu. Ila upo sahihi kabisa. Kuna mwingine namjua aliamua kujilipia mahari mwenyewe. Yaani bwana alikuwa anasuasua (ila walikuwa wanaishi na demu) basi demu akatoa fedha akandaa ndugu wa kule kwa bwana wakapeleka mahari. Mwanaume alikuwa ni mtu wa kujirusha hivi, handsome fulani hivi, demu akakolea mno. ndoa ilifungwa lakini ugomvi ukawa hauishi. Na kila walipokuwa wanagombana jamaa anawaambia marafiki zake, ''kwanza alijioa mwenyewe huyu''.
 
Yaani unapanga kupeleka mahari halafu unahairisha na unapoambiwa uombe msamaha unasema unakorogwa kichwa? Dada wa watu kapewa ishara muhimu sana kuwa wewe hufai lakini maskini ameshindwa kuitambua. Wewe huna tofauti na Magufuli kitabia na ndoa yako itakuwa kama ilivyokuwa yake.
 
Kama ulitoa taarifa, hakuna haja ya kuomba msamaha...
 
Ukiona mapicha picha mwanzoni inafaa ujiweke kando na huyo mtu.
Kuna ndg yetu alilazimisha kitu kama hiki hadi leo anajutia
 
Huenda habari hii ni changamsha genge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…