Amini, Usiamini. Nimepona Magonjwa 100+ Kwa Jina la Yesu!

Amini, Usiamini. Nimepona Magonjwa 100+ Kwa Jina la Yesu!

Mbona hili bandiko lako linaonekana kama vile umejiongezea gonjwa lingine na yamekua magonjwa 101 sasa.
 
Hizo ni hekaya kama za Abunuwasi tu.

Biblia nimeisoma kuliko hata wewe.

Kwa hivyo huwezi kunidanganya kitu.

Sana sana utashindwa kujibu maswali yangu uanze kufanya ad hominem fallacy kusema kwamba I'm lacking holy spirit to understand the scriptures. While the scriptures are illogical.
Badala ya kujivuna kuwa umesoma/unaijua Biblia kuliko mimi, itapendeza zaidi uki-share faida ulizopata kwa kusoma Biblia. Anyway, I appreciate that you’ve taken the time to study the Bible deeply; it’s clear you have a strong commitment to seeking understanding. My intention is not to argue or belittle anyone’s knowledge or faith, but rather to share what I’ve learned through my own journey.

Regarding your point about logic, I believe the Bible often challenges human logic because it reveals divine truths that are sometimes beyond our comprehension. As Isaiah 55:8-9 says, 'For My thoughts are not your thoughts, neither are your ways My ways,' declares the Lord. 'As the heavens are higher than the earth, so are My ways higher than your ways and My thoughts than your thoughts.'

Instead of debating, perhaps we could exchange insights and learn from each other, respecting that our understanding may come from different perspectives and experiences.
 
Huu ni ushuhuda wa kweli kabisa. Katika maisha yangu nimekuwa nikiugua magonjwa mengi ya aina mbalimbali. Kifuani, tumboni, miguuni, katika vidole, machoni, masikioni, puani, kichwani, nk, nk. Muda hautoshi kuyaeleza kwa kina. Kwa haraka haraka naweza kusema tangu ujana wangu nimeugua zaidi ya magonjwa 100. Namshukuru Mungu kwakuwa amekuwa akiniponya magonjwa kila yanaponiijia. Ninachokifanya, kila nikiumwa, namuomba Mungu aniponye kwa Jina la Yesu, kisha naweka mkono wangu juu ya sehemu inayoumwa na kuuamuru ugonjwa utoke kwa Jina la Yesu; kisha naamini kwamba imekuwa hivyo. Wakati mwingine inachukua muda kuona matokeo lakini wakati mwingine ugonjwa unatoweka saa hiyo hiyo. Maneno aliyosema Yesu ni kweli kabisa. Katika Mk 16:17-18 anasema: “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu(Yesu) watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.”

Huu ni uthibitisho kuwa Mungu yupo na anatenda miujiza hata leo kwa watu wanaomuamini. Kwa ushuhuda huu sikuambii usiende hospitali. La, hasha! Ukiwa na pesa, nenda. Nenda hata hospitali za nje ya nchi. Hata mimi kuna wakati huwa naenda hospitali kwa kuwa najua kwamba Mungu anaweza pia kuponya kwa kuwatumia madaktari. Hata hivyo ninapoenda hospitali bado naweka matumaini yangu kwa Mungu kwakuwa najua madaktari nao kuna magonjwa yako juu ya uwezo wao au elimu yao; na wakati mwingine nadhani huwa wanajisahau, badala ya kutia moyo wanakatisha tamaa. Kuna siku nilipungukiwa damu, nikaenda kumuona Daktari. Aliponipima na kuhakikisha damu imepungua, akaniuliza: “Damu umepeleka wapi wewe?” Usipokuwa na matumaini kwa Mungu ukiulizwa swali hilo la kuvunja moyo unaweza ukaugua mara mbili zaidi. Na kwa magonjwa niliyougua, kama kila ugonjwa ningekuwa nakimbilia hospitali, ningehitajika kuwa milionea maana ningepaswa kulipa pesa nyingi za matibabu. Namshukuru Yesu anaponya bila kulipa hata senti. Nawasikitikia wanaosema eti Mungu hayupo. Wanakosa baraka hizi za uzima.

Hata hivyo kuna vigezo na masharti ya kuzingatia ili mtu aone kikamilifu uponyaji wa Mungu kwa Jina la Yesu. Baadhi ya vigezo vimeelezwa katika Andiko hili: Kutoka 15:26. “Mungu akasema, ‘Kama mtaisikiliza kwa bidii sauti yangu mimi BWANA Mungu wenu na kuyafanya yaliyo sawa mbele yangu, kama mtayatii maagizo yangu na kuzishika amri zangu zote, sitaleta juu yenu ugonjwa wowote niliowaletea Wamisri, kwa kuwa Mimi ndimi BWANA, niwaponyaye.’” Uponyaji wa Mungu ni wa bure kwa wote wanaozingatia maneno hayo. Ukisikia Mtumishi anakuambia ulipe pesa kwanza ndio akuombee, jihadhari naye. Yesu alipowapa mamlaka wanafunzi wake ya kukemea pepo na kuweka mikono juu ya wagonjwa ili wapone, aliwaambia amewapa bure, hivyo wanapaswa kutoa huduma hiyo bure(Mathayo 10:8).

Yamkini unaumwa, umetibiwa kila mahali hujapona. Usikate tamaa. Ushuhuda huu ukutie moyo kuwa unaweza kupona kwa uwezo wa Jina la Yesu Kristo. Yote yawezekana kwake aaminiye(Mk 9:23). Amen.
Imani huponya 🙏
 
Kunywa taratibu hiyo chai na Super Loaf, halafu tumbo likianza kuuma nenda hospitali utapewa dawa. Maumivu yakizidi waite Watumishi wa Mungu watakuombea utapona kwa Jina la Yesu.
😄😃😃😃😃😃
 
Ukisoma comments utajua ni jinsi gani kizazi hiki kimefika hapa

Hakimtaki Mungu ,hakiamini Matendo yake makuu,

Mmezoea mazingaombwe na utapeli wa kina mwamposa,suguye, Mazinge,zumaridi na wala nguruwe wengine basi mnaona kama Yesu hawezi kutenda

Binafsi nimeshuhudia miujiza ya Yesu ya kutosha ,


Kama Unajua taratibu za maombi, Unajua law of nature ,basi utashuhudia miujiza mingi sana kwa Jina la Yesu


Nikiona kebehi kwa Yesu ,Huwa naishia kucheka tu

Ila Dunia imeenda mbali sana

Itakuwa kama siku za Nuhu ,watu watakuwa wakila na kunywa ,wakioa na kuolewa
 
Back
Top Bottom