Pre GE2025 Amos Makalla Mwenezi mpya CCM Taifa, Ally Hapi Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ally Hapi ni mfano mzuri kwa kufanya kilimo baada ya kutenguliwa ukuu wa mkoa. Ameonesha kwa vitendo kwamba siyo lazima apate cheo cha kisiasa ili aishi.
Kwa uzoefu aliopata kwenye kilimo, atakuwa kiongozi anayejua shida za wakulima.
 
Kilasiku hahahaha wanabadirishana nafasi tu, that means Chama hakuna workforce ya kutosha. Wanachama wajitathmini
 
Mvinyo ileile kwenye chupa tofauti tofauti..., miaka nenda miaka rudi. Nadhani hii ni aidha hadi YESU akirudi AU CCM ikiondoka madarakani.
Miaka nenda rudi ni walewale tu alafu Chama kinajidai kuwa na wanachama zaidi ya mil 12. Je katika idadi yote hiyo wanaostahili kuteuliwa ni walewale tu?
 
Happi amerudi kwenye cake ya taifa?? Km namuona kidampaa akifurahi kututambia wenzie, basha wake kapata teuzi.

Tutakomaaaa mwaka huu, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Happi amerudi kwenye cake ya taifa?? Km namuona kidampaa akifurahi kututambia wenzie, basha wake kapata teuzi.

Tutakomaaaa mwaka huu, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Duuuuuh upande wa mwenezi sijaona mtu mwenye kujipamba ccm na kuwafanya watanzania waiamini na kuweza kuipa kura tena
 
sijawahi mwelewa makala, zaidi ya kuona midomo ikicheza cheza tu. Ila salute sana kwa Mongera, Hapi...kazi naimani itapigwa sana kama ushirikiano utakamilika toka kwa mkuu wa nchi
 
Kwa hiyo Ali Happy alikuwa analima na drones? Mbona tulikuwa tunamuona anabeba kwenye mandoo machakavu na sio kutumia scavator?
Ngumu kuelewa

Ukishafika level ya juu au kati wkenye kilimo, hulazimiki kuwa na mundu, singe na ndoo site

Unatakiwa kuwa na strong team on the ground
 
CCM ni Chama kinachofuata ushauri wa wanachama wake,nadhani ni vizuri kwa vyama vingine kuiga mfano huu.
Yawezekana Mbinu ya kufuata ushauri ni mojawapo ya sababu ya CCM kuendelea kubaki madarakani.
Nawapongeza wote walioaminiwa na kuteuliwa na Chama,lakini ni muhimu kwao kuona teuzi hizo sio za kudumu bali ni Chama kinachopaswa kudumu.
Muda wowote nafasi zao zinaweza kuwa za wengine kwa nyakati ambazo Chama kitahitaji kujibalidisha kutokana na maoni ya wanachama.
 
" afadhali angebaki tu Makonda" ndio sentensi inayotamba mitandaoni usiku huu

Sijajua Wana CCM walitaka ateuliwe nani? Pascal Mayalla au nani?!!!

Mlale Unono 😀😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…