Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Mh kulingana na Tanzania ilipotoka, Ilipo na inapokwenda unafikiri unatosha kuwatumikia Watanzania katika nyanja ya Ubunge au hata Uwaziri?? Ni vyema ukatuambia kwanini..??
Ubunge ni Matakwa ya WANANCHI, ila nikijitathimini, nimevuka malengo, Kuna vitu Nimefanya havikwepo hata KWENYE ahadi. Ya UWAZIRI NAOMBA NISIZISEMEE MAMLAKA HUSIKA. KUNA KUTUMWA NA KUNA KUPUMZISHWA
 
Mimi bado suala la kuokota watu kwenye viroba baharini halafu mnakimbilia kusema walikuwa wahamiaji haramu kisha mnaenda kuwafukia bila hata kuchukua vipimo kuwatambua iliniuma sana, wakati huo huo tuna ndugu zetu ambao wamepotea na mpaka sasa hatujui walipo! Hili unalizungumziaje?

Mwigulu Nchemba
 
Angalau umekuwa muungwana kujibu kwa utulivu hasa zile comment zenye maudhi na kejeli,nakuomba endelea kuwepo kwa kadri iwezekanavyo
 
Hivi mshahara wa mbunge ni kiasi gani?
Mshahara wa waziri ni kiasi gani?
Mtu akihamia CCM analipwa kiasi gani?
(Unaweza kunijibu kwa Ile ID yako feki)
 
Kwa hivyo safari yako kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020, ndiyo imeanza na hoja hii? Katika yoote yanayoendelea nchini na yanayosikika kukuhusu ndiyo umeianza kihivyo?
 
Hapa Kuna TAARIFA umezitumia sio sahihi. TAARIFA zilizopo UMASIKINI UNAPUNGUA, NDIO TAARIFA MPYA KABISA, HIZI ZA 2M people kurudi kwenye UMASIKINI umezitoa wapi?
 
  • Bro Mwigulu Nchemba watuwazima wanasema muungwana akivuliwa nguo huchutama! Nafikiri uliwahi kusikia neno hili!
  • Kiukweli Watanzania wamepondeka sana mioyo kwa madudu mliyotenda kwa nafasi zenu pale mlipopewa dhamana ya uongozi.
  • Unakumbuka wazi sarakasi zilizokuwa zinaendelea wakati ukiwa naibu waziri kwenye wizara ya fedha ambapo kwa nia njema kabisa mh Rais alikupa nafasi hiyo akiamini kupitia taaluma yako ya uchumi ungeweza kumsaidia,ila unajua mlichokifanya.
  • Ndugu unakumbuka matukio mengi ya kunyamazisha na kuumiza,kutesa,na kujaribu kuwatia hofu Wananchi yametokea wakati ukiwa waziri wa mambo ya ndani. Mlifika mahali hadi mkawa mnapanga OP ambazo hata mkuu wa nchi na viongozi waandamizi wa jeshi la polisi wakiwa hawajui.
  • Ikiwa yote haya na mengine mengi yangali yanasononesha mioyo ya watanzania, kwanini unazidisha machunju kwa kujitokeza hadharani hapa?
  • Umesahau wewe ni mshiriki mathubuti wa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari na kujieleza? Maxence Melo kapata kesi ngapi zisizo na kichwa wala miguu ambazo lengo kuu ilikuwa kumtia woga ili watu wasipate panel ya kujua japo kwa uchache madudu yenu?
  • Kwanini sasa usianzishe forum yako na ukaiendesha kwa namna unavyoona inafaa kwa kuwa JF ilikumbwa na misuko suko mingi ambayo ninyi wanasiasa ndo kiini?
  • Lisu mbali na kuwa hasimu wako kisiasa,ila bado wote mnatokea Singida,huoni aibu kutotoa hata neno la pole as brothers mlotoka sehemu moja?
  • Ikiwa leo mtu yeyote anafanya jambo kwa manufaa ya taasisi fulani,whether positive au negative ni lazima Merits ama demerits ziende kwa taasisi husika, sasa hili la kuchafua mazingira nchi nzima kwa kuandika jina lako kwenye majabali wewe unalikwepa vipi?
  • Ukweli usemwe tu kwamba pamoja na mambo mengine mengi Ulikuwa blinded na ambitions kabla ya uchaguzi mkuu ulopita kiasi mkajisahau na kuanza kumhujumu aliyeshinda ili muonekane ni maprofesa wa siasa na kwamba jiwe ni Jr kwenye uongozi, akawagundua na kufyekelea mbali.
  • Mwisho kabisa kwa kuwa umeamua kuandaa uzi wa ana kwa ana na kwamba unajua maana ya ana kwa ana basi jaribu kuwa muungwana kujibu maswali unayoulizwa bila kutoa majibu ya jumla na ahadi zako za kutaka watu wakupigie kutoa ufafanuzi.
 
Mh humu jukwaani wewe ni member wa siku nyingi sana, jukwaa kwa miaka mingi mpaka leo huwa na mijadala mipana juu ya mambo ya msingi kwenye maendeleo ya nchi hii ikiwemo siasa, uchumi, madini,ulinzi, oil and gas nk.. Mh sijawahi kukuona kwenye hiyo mijadala ukitoa michango yako kama msomi wa kiwango cha PHD, vipi tatizo ni nini Mh..?
 
Usikatishwe tamaa na haters, wasikurudishe nyuma, wengi hawayajui unayoyajua, kaza mwendo utafika tu, tunakuombea na kujutakia mafanikio, kila la heri bro.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo mijadala huwa sio ya PhD
 
Ni jambo gani la tofauti ulofanya ukiwa waziri ambalo unazani utakumbukwa kwalo?

Any value addition you think you made with relevant examples.

Maana vituo vya polisi viko mbali na makazi ya watu, vyoo vya mahabusu vinanuka vibaya n.k


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo Singida ulienda kuwa hadaa raia, maana pindi ulipokua waziri ulikua na fursa moja kwa moja ya kufanya unachokizungumzia hapo baada ya kupwaya umerudi kulialia hapa hufai hata bure mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukipenda kitu sio lazima imsaidie mtu, kwani unapovaa jezi ya Chelsea au Man u huwa inatusaidia Nini hata UINGEREZA HUJAFIKA. MIMI NAJIVUNIA UTANZANIA WANGU, HIYO BENDERA YA TAIFA
Naona umemjibu vizuri huyo jamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…