Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Nitafute nikufafanulie maana inaonekana HUJUI KABISA

Halafu we Mwigulu acha utoto we dogo, umeleta uzi hapa jukwaani kwa mbwembwe na ukasema utatoa majibu, saa unataka watu wakufuate ukatolee majibu pembeni!

Kwanini badala ya kuleta uzi hapa usingewaalika watu huko pembeni ukawajibie huko? Huna uwezo wa kujibu maswali ya msingi, na sio ww tu, ni kuanzia mwenyekiti wako mpaka wanaccm wenzako wote. Ndio maana mnaishi kwa kujipendekeza ili mpate ulaji.
 
Wakati unamwita Abdul ni Kinyago ulikuwa unajua kuna kwenda Mbinguni?

Unaweza kuongeza hata unywele tu kwenye mwili wa Abdul?

Vipi ulishatubu juu ya hili?

Wakati fulani ukiwa Waziri wa internal affairs ulisema miili iliyokutwa baharini ni ya wahamiaji haramu

Ni wapi kwenye dunia hii muhamiaji haramu adhabu yake ni kifo?
Kesho Siku ya IBAADA KATUBU KWANZA NDIO UWATAZAME WENGINE. MAANA MBINGUNI HATUTAKWENDA KWA KUWAHUKUMU WENGINE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweliii... Maxence Melo NAUNGA MKONO HOJA
Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara,Harmonise,Diamond na Mwigulu na wengine
 
Akikujibu ni-Tag
 
Unazungumziaje swala la wapinzani kuhamia ccm na kupewa kipaumbele huku vijana wa ccm wakibaki bila teuzi...?

Sent using Jamii Forums mobile app
HATUKO CCM KWA AJILI YA UTEUZI. UTEUZI NI KWA AJILI YA KAZI. KAMA HATA KUNA MTANZANIA YUKO UPINZANI HATA HAJAHAMIA CCM ILA ANAFAA KWA UTEUZI ATEULIWE TU. ATAWASAIDIA CCM NA UPINZANI
 

Huna majibu ya tatizo la ajira ww na hao wenzako mliokaa kujadili, sana sana mlikuwa mnapiga porojo ili mpate maneno ya kuuza kwa wananchi wenye uelewa finyu. Nyie wenyewe bado mnanyenyekea ajira zilizopo, mtawezaje kupata ufumbuzi wa ajira mpya? Kwa ujumla uwezo wenu sio wa kupata ufumbuzi wa tatizo la ajira, bali uwezo na akili yenu upo kuifanya ccm iendelee kukaa madarakani kwa mbeleko ya vyombo vya dola.

Mfano mrahisi wa kwamba ww huna suluhisho la ajira nchi hii, ni wakati ulipokuwa waziri ulikuwa unategemea madaraka yako kuifanya Singida United kufanya vyema, ila ulipokosa uwaziri tu, tayari timu hiyo inayumba. Nilitarajia ww kama mchumi uendeshe timu hiyo Kisomi, lakini bado ni timu inayotegemea vyanzo vya unapokuwa na cheo! Katika mazingira hayo ww una jipya lipi la ajira mpya ndani ya nchi hii?
 
Mzee Lwakatare na familia yake kesho wanaenda kanisani kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kutokana yaliyotokana na kesi ya Ugaidi uliyoitunga kwa kushirikiana na Ludovic , subiri malipo ya Mungu
 

jamani watanzania wana maswali kama nini...mtamzeesha baba wa watu
 
Umeongea kwa hisia sana mkuu...pole sana[emoji848][emoji24]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kitu ambacho nimegundua mweshiwa anachagua maswali marahisi..kwa maana nyingine anapiga chabo...anasahau yale maswali magumu ni compulsory kujibu...

mweshimiwa amza yako ya kugombea nafasi ya urahisi imeishia wapi?????? umeghairi au muda bado?????????????
 
Safi sana mkuu kada mtiifu.Swali langu ni hili: Hivi kuna ukweli wowote kua ili ufanikiwe kwenye siasa asa kupitia CCM ni lazma ufanye dhuluma, visasi na fujo?

Mwisho, hivi unajua kua Mh. Lissu hakufa na kuna uwezekano mkubwa ukatangulia wewe huko?

Ahsante
 
Mwigulu; wewe ni mlezi wa Singida Utd, but una tabia ya kuchukua wachezaji wazuri wa Singida kisha unawapeleka Yanga, huoni kwa kufanya hivyo unaihujumu Singida Utd kwa kuipunguza nguvu, now iko chini kwenye nafasi za kushuka daraja?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwakua mwaka 2015 ulionyesha nia na ukaingia kwenye kinyanganilo cha uchaguzi ndani ya chama je mwaka huu 2020 utaingie tena kwenge kinyanganyilo ndani ya chama kuwanaia nafasi ya kupeperusha bendera ya chama
 
Kwanza nakupongeza kwa kuja kujadiliana hapa na kujibu maswali hilo ni jambo zuri sana tunapenda viongozi wetu muwe mnajitokeza kuweza kupeana just habar

Pia watu tujitahidi kuuliza maswali ya msingi dharau haisadii kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…