Mkuu M.N,
(a)Mbali na uvaaji wa skafu, tunawezaje kuhamasisha, kujenga na kuimarisha hisia za uzalendo nchini, hususani miongoni mwa vijana?Tofauti za kiitikadi na kifalsafa zinaweza kukwaza mchakato huo?
(b) Nini imani yako juu ya hali ya elimu katika jimbo la Iramba Magharibi na nchini kwa ujumla?Elimu imeimarika au imedhoofu, kulinganisha na mwaka 2015?
(c) Baadhi ya wanaharakati wa haki za kiraia na binadamu wanaamini ujauzito haupaswi kuwa sababu ya kuua ndoto za kielimu za watoto wa kike. Kuipa nguvu hoja yao, wanaharakati hao, wanatumia ilani ya uchaguzi ya CCM, ya mwaka 2015, uk.95 kipengele I (i,), (ii) & (iii).Tunaweza kupata mtazamo wako juu ya hili?
(d) Katika nafasi yako kama mjumbe wa Kamati ya Ushauri mkoa wa Singida, unafikiri kulikuwa na haja ya kweli ya kuwa na Wilaya na Halmashauri ya Mkalama?Kwa nini, badala yake, isingeimarishwa wilaya na Halmashauri ya Iramba ili kuokoa fedha? Kama ilikuwepo haja ya wilaya na Halmashauri mpya, Mkalama ilikuwa ni chaguo sahihi kijiografia?
Baada ya maswali hayo, nikutakie kila la heri katika harakati zako za kuwakilisha wananchi wa Iramba Magharibi.