Anachokifanya Rais Magufuli kingefanywa na Rais muislam basi angekosolewa vikali

Status
Not open for further replies.
Pia tujiulize, salamu za kidini zina ulazima gani kwenye shughuli za kiserikali? Sikumbuki kuwahi kumsikia Mzee Mkapa akisalimia watu 'Bwana Yesu asifiwe', au 'As-salaam aleikum', au 'Bwana apewe sifa'
Hivi juzi kati Msajili wa vyama aliiandikia ACT Wazalendo barua ya kuwataka wajieleze kwa kutumika neno la Kidini (ALlahu Akbar wakati wa kupandisha bendera ya chama ) kwenye hafla ya kushusha Tanga na kupandisha Tanga kule Zenji.Walio sema Maneno hayo ni wafuasi tuu si Viongozi wala haikuwa Rasmi.
Hivi bado kesi ile haijamalizika ,na inatishia kukifuta ACT kwa kuchanganya dini na siasa.

Ni kweli Magufuli amezidi kujionesha ni Mkiristo sana na anaupendelea sana Ukiristo.

Jana Nimeona Hotuba yake alipokuwa akiwa hutubia wkiristo wa dhehebu la ACG kule mbeya
 
you have a point. salamu za kidini kwenye mikutano ya hadhara are very awkward. salamu ni mabibi na mabwana habari" hiyo tu inatosha
Ukweli hata Mimi salaam za kidini wanazosalimia wanasiasa kwenye mikutano ya kisiasa huwa zinanichefua Sana. Mengine ni masheitwani halafu yanasema salaam za kidini.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 

Hawawenzi kuelewa hilo. Ni muhimu kuelezana na kufundishana. Baadhi ya wenzetu hawa si wote lakini wakizazi chao ambacho kimeingia uzeeni sasa wanakuto kujiamini flani hivi walikojijengea. Unakuta mtu alisoma shule ya kanisa akapata elimu nzuri tu. Baadaye akaajiriwa serikalini kazi nzuri tu, ikamtoa kimaisha lakini bado nafsini mwake anakaubaguzi na chuki kwa Wakristo.

Ndio unakuta mambo kama yale ya UDOM enzi zile na kuna wakati moja ya majeshi yakitafuta makuruta hata darasa la saba ili mradi tu awe wa dini yetu Wakati kazi yake huyu kuruta itamuhitaji ajue aeiou za sheria.

Wakati JPM anaongea na mfalme wa Morocco hatukusikia mbona anatumia urais kwenye mambo ya dini, unafiki unafiki tu..
 
Hii mada ulitakiwa uweke angalizo la wenye akili tu na walio neutral kimawazo kuwa ndo wahusika kuchangia. Bahati mbaya wamekuja wafia dini na wajinga wajinga ambao hawajui lolote kuhusu utengamano wa kitaifa.

Mimi mkristo, zile barua za wazi kutoka TEC na wakristo wengine kipindi cha Kikwete ziko wapi leo. Ule ukosoaji kipindi kile uko wapi? Mbona sikuwahi ona matangazo kuwa Kikwete kaenda kuswali Ijumaa.
Yani Magufuli anaenda kusali nayo inakuwa headline kwenye media, kurugenzi ya ikulu nayo inasema. Hawa watu wanaolazimisha tuwaone wacha Mungu sijawahi waamini.
Mimi ni shabiki mzuri sana wa secularism. Imagine Kikwete angekuwa anavaa kanzu kama watu wa Pwani si yangetolewa matamko ya kupinga.
 
Vipi hili analosema mtoa mada kuhusu kurugenzi ya mawasiliano ya ikulu kufanya suala la mh rais kuabudu kama habari kuu, je hili kwako walionaje?
 

Uliona matangazo ya SGR ama Meli ziwa Nyasa, Victoria, Tanganyika, au Treni ya mizigo ikiwasili Arusha enzi za Mh Kikwete.? Kila jambo na wakati wake na kusudi katika kila majira.
 
Ziara ya mfalme wa Morocco ulikua ni ugeni wa kiserikali, lakini kitendo cha mheshimiwa rais kuomba msaada wa msikiti ni cha kujidhalilisha mno, hata huyo mfalme atakua alimshangaa!

Tatizo letu wakristo ndio hili, tunadhani waislam mahitaji yao ni misikiti tu.
 
Meko ni mtu ambaye ameshapoteza trust ya wananzengo kwahio ni lazima afanye vibweka kama hivyo ila si vizuri maana hata kwenye biblia imeandikwa Nyumba yangu sio pango la wezi na wanyang`anyi lakini vile vile hao wachungaji wanao mkaribisha na kumpa madhabahu wanatupa hisia za mashaka juu ya mienendo yao pengine sio mizuri ndio maana wanamruhusu Meko awamanipulate lakini kama wangekua safi wangetreat Meko kama waumini wengine na wangeiheshim madhabahu refer watu kama kina kakobe,Gwajima waliweza kunasa . Kwahio Meko haendi kwa watu safi hata siku moja.
 
Ni mkristo, siwezi kuikana imani yangu. Lakini namshukuru Mungu kuwa ukristo wangu haunitii upofu kwenye haki za wengine.

Kaka Mungu akubariki sana

Tatizo la Magufuli ana udini sana, haswa mwanzoni mwa utawala wake aliwaweka pembeni sana Waislamu.
Akaamua kuikumbatia BAKWATA ili iwe balozi wake kwa waislamu kutuliza hasira zao

Lakini hata akiondoka madarakani leo, waislamu watamkumbuka kama raisi mdini sana aliyewabagua kupita kiasi!
 

Wewe unajua wazo la kumuomba mfalme wa Morocco msikiti Mh Rais alishauriwa na nani? Kabla ya kuandika hivi. Hii si afya hata kidogo, unless uko na kazi nyingine umepewa hapa ya kutuchepusha kiana. Vinginevyo hii si nzuri hata kidogo.
 
mwarobaini_ je, umetumwa na nani hasa kuja 'Kupandikiza' hizi 'Chuki' zako za 'Kidini' hapa JF hasa kupitia tu huu 'Ufafanuzi' / 'Uchambuzi' wako?
Ni mimi mwenyewe nimesukumwa na nafsi yangu mkuu, kwakweli nimeona japo hii ni topic 'sensitive' lakini ni jambo la heri zaidi tuijadili kuliko kukaa nayo mioyoni mwetu.
 
Reactions: RTI
Wewe unajua wazo la kumuomba mfalme wa Morocco msikiti Mh Rais alishauriwa na nani? Kabla ya kuandika hivi. Hii si afya hata kidogo, unless uko na kazi nyingine umepewa hapa ya kutuchepusha kiana. Vinginevyo hii si nzuri hata kidogo.
Haijalishi kama ni BAKWATA au nani walimshauri, lakini haibadili ukweli kuwa mahitaji ya waislam nchi hii ni zaidi ya misikiti pekee.
 
Umesoma na kuuelewa uzi kweli?
 
Ni mimi mwenyewe nimesukumwa na nafsi yangu mkuu, kwakweli nimeona japo hii ni topic 'sensitive' lakini ni jambo la heri zaidi tuijadili kuliko kukaa nayo mioyoni mwetu.

Haya kila la heri, na kushauri tu lakini,sema na huo moyo wako.
 
Ni mimi mwenyewe nimesukumwa na nafsi yangu mkuu, kwakweli nimeona japo hii ni topic 'sensitive' lakini ni jambo la heri zaidi tuijadili kuliko kukaa nayo mioyoni mwetu.

Ukristo wako unaanza Kunipa mno 'Mashaka' na huenda nyie ndiyo wale wale ambao mmekuwa 'Wakristo' baada ya 'Kuoa' Wanawake wa Kikristo.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…