Anachosema Lissu ni kwamba, Bunge lisivunjwe mwezi wa sita, Rais na Wabunge waendelee hadi Reforms zikamilishwe, ndio uchaguzi mkuu ufanyike

Mimi nikiwa Mbunge najua siwezi kurudi au sina mpango wa kugombea tena nitakuwa wa kwanza kuunga mkono hoja ya Lissu!!! Miaka miwili ya ziada si pesa haba, na kiinua mgongo kinaongezeka!!!
Kama baada ya miaka 2 Watanzania watakuwa na katiba bora inayoweza kubadilisha siasa za Tanzania kuwa bora zaidi, pesa na kiinua mgongo cha hao wabunge unaowazungumzia ni jambo dogo sana.
 
Huo ni mtego. Wenye chama watahamasisha mwisho wa siku utashangaa wanakataa kuongezewa muda ila wasio na sauti kwenye chama moyoni wanatamani kuendelea kuvuta posho.
Mimi ningekuwa Samia, napewa miaka miwili ya ziada, ningekubali haraka sana. Kisha Reforms zikisha kamilika nawaachia CCM lichama lao nasema mie sigombei tena nimechoka nataka kuishi muda mrefu! 😀
 
Kama baada ya miaka 2 Watanzania watakuwa na katiba bora inayoweza kubadilisha siasa za Tanzania kuwa bora zaidi, pesa na kiinua mgongo cha hao wabunge unaowazungumzia ni jambo dogo sana.
Ni kweli 100% Mkuu. Hakuna gharama kubwa ya kununua demokrasia ya kweli
 
Wabunge hawa hawa wa chama kimoja? Haya ngoja tuone
 
Jeshi ndio Dola hawawezi kubali kuvunja katiba wakati mhusika walishamueleza akashupaza shingo na kusema katiba ni kijitabu tu!!

Hilo ccm hawawezi kulikubali hilo!!
 

Ccm hawana utashi I a kufanya Hilo jambo
 
Kwa hiyo atafanya nini?
 
Ushauri wa kipumbavu sana, hawajajiandaa kwa uchaguzi wanataka muda, hatuwapumzishi, ni mchaka mchaka tu
Hapana, bila shaka uko CCM, na unataka mbebwe na mifumo mibovu iliyopo mpate miaka mingine mitano sio miwili tu
 
Inamaana kabla ya kufanya reform, kwanza mjadala uwe ni serikali iliyopo iongezewe muda mpaka lini.

Huu mtego ukikubalika na Ccm ujue CHADEMA wajipange kwa 2035 sio 2025 wala 2030.

Swali: Huu ni msimamo wa Chama baada ya kujadiliana au ni akili ya TAL pekeyake?

TAL namkubali sana, ila hiyo nafasi haiitaji mihemko, haraka wala hasira, inahitaji akili zake na za wengine ziunganishwe pamoja ndo zitumike. Akitumia akili yake mwenyewe hata iwe kubwa kiasi gani atafeli.
 
💯👌
 
Sawa kabisa. Na unaona, TLS hajasema tufanye serikali ya mseto wakati wa Reforms, anasema wao waendelee tu kuwa madarakani, ili watu wasije wakasema mnachotaka ni madaraka tu!

Naanza kuelewa kwa nini JK alisema ni afadhali Dr. Slaa awe raisi na sio TLS kuwa mbunge, kwa sababu TLS anafanya CCM walale na viatu!
 
Nikuulize, haya maamuzi ya maandamano ili kupeleka mbele uchaguzi ni maamuzi ya chama kupitia TAL au maamuzi ya TAL kupitia chama?

Unajua, TAL hata awe na akili kuliko binadamu wote, linapokuja suala la maamuzi bila kushirikisha akili za wengine kuna Tundu hataziona na atapigiwa hapo hapo kwenye hilo tundu.
 
Lissu,Lissu,nchi hii haiongozwu na hao watu unaowaona kwenye TV.
Kwa hiyo hauna sababu ya kuhofu kuhusu Uchaguzi Mkuu.
 
Kwa wale wasiopenda mabadiliko hii hoja hawataki kuisikia kabisa mana ni mtego. Yaano waongezewe muda wakati wakijua kabisa watajishtaki kwa kushindwa kufanya reforms. Ngoja tusubiri tuone
Mie nadhani wazo kama hili likikataliwa na CCM bila sababu za msingi, basi kinachobaki ni kuwaambia JWTZ washike nchi kwa miaka miwili ili Reforms zifanyike chini ya utawala wa kijeshi. Muda wa kubembelezana ifikie wakati ukome

Traole wa Burkina Faso anakuja Tanzania, labda awanong'oneze neno wanajeshi wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…