Anachosema Lissu ni kwamba, Bunge lisivunjwe mwezi wa sita, Rais na Wabunge waendelee hadi Reforms zikamilishwe, ndio uchaguzi mkuu ufanyike

Anachosema Lissu ni kwamba, Bunge lisivunjwe mwezi wa sita, Rais na Wabunge waendelee hadi Reforms zikamilishwe, ndio uchaguzi mkuu ufanyike

Mimi nikiwa Mbunge najua siwezi kurudi au sina mpango wa kugombea tena nitakuwa wa kwanza kuunga mkono hoja ya Lissu!!! Miaka miwili ya ziada si pesa haba, na kiinua mgongo kinaongezeka!!!
Kama baada ya miaka 2 Watanzania watakuwa na katiba bora inayoweza kubadilisha siasa za Tanzania kuwa bora zaidi, pesa na kiinua mgongo cha hao wabunge unaowazungumzia ni jambo dogo sana.
 
Huo ni mtego. Wenye chama watahamasisha mwisho wa siku utashangaa wanakataa kuongezewa muda ila wasio na sauti kwenye chama moyoni wanatamani kuendelea kuvuta posho.
Mimi ningekuwa Samia, napewa miaka miwili ya ziada, ningekubali haraka sana. Kisha Reforms zikisha kamilika nawaachia CCM lichama lao nasema mie sigombei tena nimechoka nataka kuishi muda mrefu! 😀
 
Kama baada ya miaka 2 Watanzania watakuwa na katiba bora inayoweza kubadilisha siasa za Tanzania kuwa bora zaidi, pesa na kiinua mgongo cha hao wabunge unaowazungumzia ni jambo dogo sana.
Ni kweli 100% Mkuu. Hakuna gharama kubwa ya kununua demokrasia ya kweli
 
Ila mimi naona yanazungumzika tu na jeshi kukaa pembeni ikiwa na wao wanaona kabisa lengo ni kuleta utulivu.

Wanasheria tusaidieni bunge haliwezi kufanya mabadiliko ya katiba ili waongezewe muda pamoja na rais ili wapate muda wa kufanya reforms na maridhiano?
Jeshi ndio Dola hawawezi kubali kuvunja katiba wakati mhusika walishamueleza akashupaza shingo na kusema katiba ni kijitabu tu!!

Hilo ccm hawawezi kulikubali hilo!!
 
Ukitafakari sana, bila kuwa na utando wa kishabiki kichwani, Lissu anaongea kitu cha maana na hapa tayari ameonyesha ku-compromise na CCM.

Pendekezo lake la "No Reforms na Elections" kwa alivyofafanua na nikamuelewa, anasema kwamba, Chadema wako tayari CCM iendelee kuwa madarakani kwa muda ulioongezwa, yaani Samia na Wabunge waendelee kuwa madarakani, hadi Reforms zikamilishwe. Zikishakamilishwa basi ndipo sasa ipangwe Bunge livunjwe lini na Uchaguzi Mkuu ufanyike lini, labda October 2026 badala ya October 2025, au hata October 2027. Yaani Wabunge na Raisi waongezewe kipindi cha mwaka mmoja, hadi miwili ikibidi, ili kufanya Reforms.

Sasa mimi nadhani kwa mtu mwenye kufikiri, hili si wazo baya, ni wazo la mtu mwenye akili na alie tayari kutafakari. Amesha-compromise.

Kwa upande wa pili ina make sense. Kwa nini uingie kwenye uchaguzi ambao unajua unafanyika katika misingi mibovu? Ni vema uahirishe uchaguzi ili urekebishe hiyo misingi mibovu kwanza.

Na hii ni lojiki ya kawaida ya maisha ya kila siku. Nikitaka kusafiri kesho, huku nikitambua gari nitakayotumia ni mbovu itanikwamisha njiani, basi ni vema nicheleweshe safari ili gari irekebishwe kuliko kusema ngoja niende tu nitafanya cha kufanya huko mbele. Unaweza ukafia njiani.

Sasa CCM msipoelewa hili nyie ni wakorofi na mnafanya makusudi kwa sababu hamtaki Reforms

Hebu Wasira katika busara za uzee wake atuambie ubaya wa hili wazo ni nini?

Ccm hawana utashi I a kufanya Hilo jambo
 
Mafisiem yanahaha na kutapatapa halafu yanajifanya kama vile ushindi wa Lissu hauna impact yoyote kwao, eti sasa hivi ndio yanauliza kwani hata akiwa mwenyekiti atafanya nini, kama yanajua hatafanya kitu mbona yamechukia yeye kushinda na yalikuwa yanatamani Mbowe ndio aendelee
Kwa hiyo atafanya nini?
 
Ushauri wa kipumbavu sana, hawajajiandaa kwa uchaguzi wanataka muda, hatuwapumzishi, ni mchaka mchaka tu
Hapana, bila shaka uko CCM, na unataka mbebwe na mifumo mibovu iliyopo mpate miaka mingine mitano sio miwili tu
 
Inamaana kabla ya kufanya reform, kwanza mjadala uwe ni serikali iliyopo iongezewe muda mpaka lini.

Huu mtego ukikubalika na Ccm ujue CHADEMA wajipange kwa 2035 sio 2025 wala 2030.

Swali: Huu ni msimamo wa Chama baada ya kujadiliana au ni akili ya TAL pekeyake?

TAL namkubali sana, ila hiyo nafasi haiitaji mihemko, haraka wala hasira, inahitaji akili zake na za wengine ziunganishwe pamoja ndo zitumike. Akitumia akili yake mwenyewe hata iwe kubwa kiasi gani atafeli.
 
Nadhani ameelewa inabidi Chadema wa-sacrifice kitu ili kupata kitu. Kumwongeza Samia na Wabunge miaka hadi miwili ili kupata kitu cha kudumu kwa ajili ya Watanzania wote naona ni wazo linaloweza kutoka kwa mzalendo wa kweli tu, anaeweka maslahi ya taifa mbele.
💯👌
 
Inamaana kabla ya kufanya reform, kwanza mjadala uwe ni serikali iliyopo iongezewe muda mpaka lini.

Huu mtego ukikubalika na Ccm ujue CHADEMA wajipange kwa 2035 sio 2025 wala 2030.

TAL namkubali sana, ila hiyo nafasi haiitaji mihemko, haraka wala hasira, inahitaji akili zake na za wengine ziunganishwe pamoja ndo zitumike. Akitumia akili yake mwenyewe hata iwe kubwa kiasi gani atafeli.
Sawa kabisa. Na unaona, TLS hajasema tufanye serikali ya mseto wakati wa Reforms, anasema wao waendelee tu kuwa madarakani, ili watu wasije wakasema mnachotaka ni madaraka tu!

Naanza kuelewa kwa nini JK alisema ni afadhali Dr. Slaa awe raisi na sio TLS kuwa mbunge, kwa sababu TLS anafanya CCM walale na viatu!
 
Sawa kabisa. Na unaona, TLS hajasema tufanye serikali ya mseto wakati wa Reforms, anasema wao waendelee tu kuwa madarakani, ili watu wasije wakasema mnachotaka ni madaraka tu!

Naanza kuelewa kwa nini JK alisema ni afadhali Gr. Slaa awe raisi na sio TLS kuwa mbunge, kwa sababu TLS anafanya CCM walale na viatu!
Nikuulize, haya maamuzi ya maandamano ili kupeleka mbele uchaguzi ni maamuzi ya chama kupitia TAL au maamuzi ya TAL kupitia chama?

Unajua, TAL hata awe na akili kuliko binadamu wote, linapokuja suala la maamuzi bila kushirikisha akili za wengine kuna Tundu hataziona na atapigiwa hapo hapo kwenye hilo tundu.
 
Lissu,Lissu,nchi hii haiongozwu na hao watu unaowaona kwenye TV.
Kwa hiyo hauna sababu ya kuhofu kuhusu Uchaguzi Mkuu.
 
Kwa wale wasiopenda mabadiliko hii hoja hawataki kuisikia kabisa mana ni mtego. Yaano waongezewe muda wakati wakijua kabisa watajishtaki kwa kushindwa kufanya reforms. Ngoja tusubiri tuone
Mie nadhani wazo kama hili likikataliwa na CCM bila sababu za msingi, basi kinachobaki ni kuwaambia JWTZ washike nchi kwa miaka miwili ili Reforms zifanyike chini ya utawala wa kijeshi. Muda wa kubembelezana ifikie wakati ukome

Traole wa Burkina Faso anakuja Tanzania, labda awanong'oneze neno wanajeshi wetu
 
Back
Top Bottom