Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ina maana hujasoma threadLissu anataka Samia aongezewe muda?
Hii mbona kama sio bahati mbaya, kuna nini nyuma ya pazia?
Kama baada ya miaka 2 Watanzania watakuwa na katiba bora inayoweza kubadilisha siasa za Tanzania kuwa bora zaidi, pesa na kiinua mgongo cha hao wabunge unaowazungumzia ni jambo dogo sana.Mimi nikiwa Mbunge najua siwezi kurudi au sina mpango wa kugombea tena nitakuwa wa kwanza kuunga mkono hoja ya Lissu!!! Miaka miwili ya ziada si pesa haba, na kiinua mgongo kinaongezeka!!!
Mimi ningekuwa Samia, napewa miaka miwili ya ziada, ningekubali haraka sana. Kisha Reforms zikisha kamilika nawaachia CCM lichama lao nasema mie sigombei tena nimechoka nataka kuishi muda mrefu! 😀Huo ni mtego. Wenye chama watahamasisha mwisho wa siku utashangaa wanakataa kuongezewa muda ila wasio na sauti kwenye chama moyoni wanatamani kuendelea kuvuta posho.
Ni kweli 100% Mkuu. Hakuna gharama kubwa ya kununua demokrasia ya kweliKama baada ya miaka 2 Watanzania watakuwa na katiba bora inayoweza kubadilisha siasa za Tanzania kuwa bora zaidi, pesa na kiinua mgongo cha hao wabunge unaowazungumzia ni jambo dogo sana.
Jeshi ndio Dola hawawezi kubali kuvunja katiba wakati mhusika walishamueleza akashupaza shingo na kusema katiba ni kijitabu tu!!Ila mimi naona yanazungumzika tu na jeshi kukaa pembeni ikiwa na wao wanaona kabisa lengo ni kuleta utulivu.
Wanasheria tusaidieni bunge haliwezi kufanya mabadiliko ya katiba ili waongezewe muda pamoja na rais ili wapate muda wa kufanya reforms na maridhiano?
Ukitafakari sana, bila kuwa na utando wa kishabiki kichwani, Lissu anaongea kitu cha maana na hapa tayari ameonyesha ku-compromise na CCM.
Pendekezo lake la "No Reforms na Elections" kwa alivyofafanua na nikamuelewa, anasema kwamba, Chadema wako tayari CCM iendelee kuwa madarakani kwa muda ulioongezwa, yaani Samia na Wabunge waendelee kuwa madarakani, hadi Reforms zikamilishwe. Zikishakamilishwa basi ndipo sasa ipangwe Bunge livunjwe lini na Uchaguzi Mkuu ufanyike lini, labda October 2026 badala ya October 2025, au hata October 2027. Yaani Wabunge na Raisi waongezewe kipindi cha mwaka mmoja, hadi miwili ikibidi, ili kufanya Reforms.
Sasa mimi nadhani kwa mtu mwenye kufikiri, hili si wazo baya, ni wazo la mtu mwenye akili na alie tayari kutafakari. Amesha-compromise.
Kwa upande wa pili ina make sense. Kwa nini uingie kwenye uchaguzi ambao unajua unafanyika katika misingi mibovu? Ni vema uahirishe uchaguzi ili urekebishe hiyo misingi mibovu kwanza.
Na hii ni lojiki ya kawaida ya maisha ya kila siku. Nikitaka kusafiri kesho, huku nikitambua gari nitakayotumia ni mbovu itanikwamisha njiani, basi ni vema nicheleweshe safari ili gari irekebishwe kuliko kusema ngoja niende tu nitafanya cha kufanya huko mbele. Unaweza ukafia njiani.
Sasa CCM msipoelewa hili nyie ni wakorofi na mnafanya makusudi kwa sababu hamtaki Reforms
Hebu Wasira katika busara za uzee wake atuambie ubaya wa hili wazo ni nini?
Kwa hiyo atafanya nini?Mafisiem yanahaha na kutapatapa halafu yanajifanya kama vile ushindi wa Lissu hauna impact yoyote kwao, eti sasa hivi ndio yanauliza kwani hata akiwa mwenyekiti atafanya nini, kama yanajua hatafanya kitu mbona yamechukia yeye kushinda na yalikuwa yanatamani Mbowe ndio aendelee
Hapana, bila shaka uko CCM, na unataka mbebwe na mifumo mibovu iliyopo mpate miaka mingine mitano sio miwili tuUshauri wa kipumbavu sana, hawajajiandaa kwa uchaguzi wanataka muda, hatuwapumzishi, ni mchaka mchaka tu
Ndio maana nikasema labda CCM wawe wakorofi tu wakatae hili wakijua mifumo mibovu ya uchaguzi ni kwa faida yaoCcm hawana utashi I a kufanya Hilo jambo
💯👌Nadhani ameelewa inabidi Chadema wa-sacrifice kitu ili kupata kitu. Kumwongeza Samia na Wabunge miaka hadi miwili ili kupata kitu cha kudumu kwa ajili ya Watanzania wote naona ni wazo linaloweza kutoka kwa mzalendo wa kweli tu, anaeweka maslahi ya taifa mbele.
Ndio maana nikasema labda CCM wawe wakorofi tu wakatae hili wakijua mifumo mibovu ya uchaguzi ni kwa faida yao
Sawa kabisa. Na unaona, TLS hajasema tufanye serikali ya mseto wakati wa Reforms, anasema wao waendelee tu kuwa madarakani, ili watu wasije wakasema mnachotaka ni madaraka tu!Inamaana kabla ya kufanya reform, kwanza mjadala uwe ni serikali iliyopo iongezewe muda mpaka lini.
Huu mtego ukikubalika na Ccm ujue CHADEMA wajipange kwa 2035 sio 2025 wala 2030.
TAL namkubali sana, ila hiyo nafasi haiitaji mihemko, haraka wala hasira, inahitaji akili zake na za wengine ziunganishwe pamoja ndo zitumike. Akitumia akili yake mwenyewe hata iwe kubwa kiasi gani atafeli.
AchalisuphobiaLissu anataka Samia aongezewe muda?
Hii mbona kama sio bahati mbaya, kuna nini nyuma ya pazia?
Nikuulize, haya maamuzi ya maandamano ili kupeleka mbele uchaguzi ni maamuzi ya chama kupitia TAL au maamuzi ya TAL kupitia chama?Sawa kabisa. Na unaona, TLS hajasema tufanye serikali ya mseto wakati wa Reforms, anasema wao waendelee tu kuwa madarakani, ili watu wasije wakasema mnachotaka ni madaraka tu!
Naanza kuelewa kwa nini JK alisema ni afadhali Gr. Slaa awe raisi na sio TLS kuwa mbunge, kwa sababu TLS anafanya CCM walale na viatu!
Mie nadhani wazo kama hili likikataliwa na CCM bila sababu za msingi, basi kinachobaki ni kuwaambia JWTZ washike nchi kwa miaka miwili ili Reforms zifanyike chini ya utawala wa kijeshi. Muda wa kubembelezana ifikie wakati ukomeKwa wale wasiopenda mabadiliko hii hoja hawataki kuisikia kabisa mana ni mtego. Yaano waongezewe muda wakati wakijua kabisa watajishtaki kwa kushindwa kufanya reforms. Ngoja tusubiri tuone