Anafungiwa msanii, but not video director na crew nzima. Basata kama shule hawana

Basi nimeshamaliza. Sisi watu wazima tulifundishwa zamani kuwa si sahihi kumwambia mtu mzima uwongo❌ ( iandikwe uongo✅) na wanaonifahamu watanishangaa sana kuona nabishana nawe. Its ok. You are right.
sorry aisee.

ila sio makosa kujua jambo kwa udogo hasa haya mambo ya sanaa. sheria zake. ngumu kueleweka.
 
Umesema kitu kikubwa sana Mkuu, lakini tatizo kubwa la pale Basata linatokana na kanuni pamoja na mfumo wake utendaji wa utekelezaji wa majukumu yake.

Kwa ilivyo Basata, haiwezi kuwa na watumishi ambao ni wataalam wa masuala ya video (picha jongefu) ambao wangeweza kuliona hili uliloliona hapa.

Kikanuni, Basata wanahusika na sanaa nyingine pamoja na sanaa zilizo kwenye picha mnato na sio picha jongefu (video). Wahusika wa video ni Bodi ya Filamu.

Hivyo, hili ndilo limesababisha kuwa na makosa haya ya kumwacha huru aliyelitengeneza kosa ambaye ni mtengenezaji wa video ya wimbo huo, ambaye sio Whozu, Mboso wala Nenga.

Ova
 
so ideal bodi ya filamu na basata should be one organisation working together. aisee umenifungua macho bongo kuna mapicha picha sana
 
Sieleweshwi na wapumbavu mimi. Idea ya wimbo + wimbo ni wangu, video ni Yangu, Location nachagua mimi, wewe kazi yako ni kushuti tu. Then afungiwe Director? Achana na matako tumia kichwa kufikiri POPOMA
Japo naona umejadili kwa shari, lakini acha niseme jambo kwenye hili ili kusaidia wengine ikiwa wewe utachagua kutoelewa kwa kiburi au udhaifu wako wa kuelewa.

Suala hilo la kutajwa Director ndiye mwenye kazi bunifu ya picha jongefu, ni la kitaaluma zaidi kuliko mazoea. Kama ilivyo kwenye filamu, licha ya kulipwa kwa kazi hiyo.

Ndiyo maana tunaona kwenye credit za filamu husemwa; 'A David Tony Film', licha ya huyo Director David Tony kulipwa na executive producer kwa ajili ya kazi hiyo.

Ova
 
Msanii pekee ndiye yuko accountable na kazi yake 100%...

Director ukimpelekea kazi yako, unapaswa kumueleza na "DOs & Dont DOs".

Msanii ndiye anapaswa kumuelekeza director vinavyotakiwa na visivyotakiwa kulingana na cheria na taratibu za BASATA...

Na msanii hakatazwi kukataa baadhi ya scene ambazo anaona zimeenda kinyume na taratibu za kazi yake...

Na msaanii ndiye anayepost video yake kwenye platforms mbalimbali...

Hivyo hata useme vipi, hata ubishe vipi, hapa directors hawana kosa, hawako responsible kabisa na outcomes za kazi walizofanya as long as wewe kama msanii umeshaipokea kazi na ukairidhia....
 
Hata kwenye Video za wimbo aliyeandaa hutajwa. Umiliki wa Video ni wa Msanii husika, hakuna utaalamu wowote hapo. Msanii ndio huandaa maudhui na namna gani anataka kuwasilisha ujumbe kwa hadhira yake, hakuna msanii bongo hii anapangiwa namna gani video yake iwe, zaidi ya kushauriwa na anaweza kukataa.

Afu mm sio MBUGILA, nimetembea sana dunia hii. Sheria za Bongo ziko wazi, mmiliki wa Nyimbo ni Msanii husika.
Msanii ndio hupandisha hiyo video kwenye Platform zote azijuazo yeye.
 
so ideal bodi ya filamu na basata should be one organisation working together. aisee umenifungua macho bongo kuna mapicha picha sana
Kuna mambo mawili, wafanye kazi pamoja au Basata wajue mipaka iliyopo ya majukumu kati yao na Bodi ya Filamu.

Ujue, zamani taasisi hizi zilikuwa mbalimbali, lakini sasa serikali imeamua ofisi zao ziwe katika eneo moja ili kujenga ukaribu wao kwa kushirikiana.

Nina uhakika kama Bodi ya Filamu ingechukua hatua kwa wimbo ule, nina uhakika kabisa hili kifungo kingeenda kwa Director wa ile video.

Basata hawana hata vifaa vya kukagulia picha jongefu, lakini Bodi ya Filamu wanavyo na wanafanya kazi hiyo kila siku.

Bodi ya Filamu hukagua kila kipindi cha maigizo ambacho unakiona kwenye TV zetu na mitandaoni.

Ova
 

Ukijipa muda wa kutulla hata kidogo tu utagundua mwanzoni na mwishoni mwa ile video kuna jina la Jowzey, huyo ndiye Director anayeelezewa kwenye hoja ya thread hii.

Shida yako nimejua iliko hadi inakuwa shida kwako kuelewa mipaka ya haki bunifu kwenye sanaa. Usisome ili kupata pa kuboshana, soma kwa kuelewa.

Ni kama utavyonunua jezi kwa hela zako ila ukiivaa tu, mtaani utaambiwa umevaa jezi ya Yanga au ya Simba, hakuna atakayesema ni yako.

Huo wimbo unaosema ni wa msanii, bado hauhamishi haki ya publisher ya aliyetengeza midundo, na Cosota ikikokotoa mirahaba hapewi zote msanii zinagawanywa kwa walioshiriki kukamilisha hiyo sanaa.

Hakuna hela ya kununua haki bunifu, anacholipia msanii ni studio time tu, hauziwi haki bunifu. Twende taratibu utaelewa tu.

Ova
 
[emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
 
well said
 
yaani mleta hoja unataka had mfanya usafi WA studio afungiwe au sio! hopeless kabisa. ndio maana kingereza kingi ili kuficha ujinga wako.
 
Ila wakiibiwa kazi zao ma"director" hawahusiki.

Au ndio kusema msanii akishatunga wimbo akili zinapotea, na baada ya hapo anafanya lolote analoongozwa hata la kijinga?

Wakubali kukosea, ndio uwajibikaji wenyewe.
 
yaani mleta hoja unataka had mfanya usafi WA studio afungiwe au sio! hopeless kabisa. ndio maana kingereza kingi ili kuficha ujinga wako.
credited members 🙄🙄. akili yako ni tope. shule muhimu na toka nje ya tz kidogo. ujui chochote aisee
 
Ila wakiibiwa kazi zao ma"director" hawahusiki.

Au ndio kusema msanii akishatunga wimbo akili zinapotea, na baada ya hapo anafanya lolote analoongozwa hata la kijinga?

Wakubali kukosea, ndio uwajibikaji wenyewe.
wote wamekosea sio mmoja tu.
 
Piga picha za uchi alaf tuta muwajibisha mpiga picha wako
 
pinga upuuz wa BASATA,BASATA ni upuuz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…