Beberu
JF-Expert Member
- Jan 26, 2017
- 4,548
- 9,740
Kwa hio mkuu tufungie wote waliohusika kuandaa ule wimbo?Ukijipa muda wa kutulla hata kidogo tu utagundua mwanzoni na mwishoni mwa ile video kuna jina la Jowzey, huyo ndiye Director anayeelezewa kwenye hoja ya thread hii.
Shida yako nimejua iliko hadi inakuwa shida kwako kuelewa mipaka ya haki bunifu kwenye sanaa. Usisome ili kupata pa kuboshana, soma kwa kuelewa.
Ni kama utavyonunua jezi kwa hela zako ila ukiivaa tu, mtaani utaambiwa umevaa jezi ya Yanga au ya Simba, hakuna atakayesema ni yako.
Huo wimbo unaosema ni wa msanii, bado hauhamishi haki ya publisher ya aliyetengeza midundo, na Cosota ikikokotoa mirahaba hapewi zote msanii zinagawanywa kwa walioshiriki kukamilisha hiyo sanaa.
Hakuna hela ya kununua haki bunifu, anacholipia msanii ni studio time tu, hauziwi haki bunifu. Twende taratibu utaelewa tu.
Ova
Wasanii,
Dancers
Video vixens
Director
Transporters
Watu wa mavazi
Wabeba vyakula et al
Nyumba ni ya familia ila ikipata shida ni ya kwako wewe ambae jina lipo kwenye sheria, nyumba sio ya fundi hata siku moja