Ananiambia nijipange kwao Mahari huwa ni kubwa. Nimempa assignment

Ananiambia nijipange kwao Mahari huwa ni kubwa. Nimempa assignment

Ndio 6M kwakuwa mahari hailipwi yote kwa mara moja unaweza kukubali mahari ya 6M lakini ukaoa na kuishi na mkeo hata miaka 50 na hiyo mahari haijaisha na hakuna kesi mahakamani wala kanisani/msikitini.
Jiamini kijana wangu.
Mimi nishakuwa mtu mzima, sio kijana tena. Na nimeshapokea mahari ya mtoto wa kaka yangu, so nina uzoefu kidogo kwenye issues za mahari.

Mahari haimalizwi yote, ila kwa tamaduni yetu kuna vitu ni lazima ulipe ili hiyo mahari ihesabike, sasa 6m unakuja na 1m nani akuelewe.

Watu waweke mambo yaliyoko kwenye uhalisia wa maisha ya wengi. Huwezi kumpa kijana anaanza maisha wazazi hawana uwezo eti alipe 6m, utakuwa hutumii akili, huwatakii watoto wako waanze maisha ya ndoa vizuri. Mahari should be reasonable.
Hata hivyo siafiki mahari kwa mwanamke ambaye hakuwa bikra.
 
sasa unacholalamikia na kulialia kuhusu mahari ni nini ikiwa unajua wapi utaoa burebure kama vile unachukua changudoa?
Kuna changudoa wa bure?? Anayeuza ni changudoa.
Anayeuzwa ni ng'ombe
Mke anapatikana bure
 
Ungejua nafasi yako kama mwanaume unayetegemea kuanzisha familia itakayokutegema kama mkuu wa kaya kuna vitu ungevitazama kwa jicho la tofauti sana.

Yaani umemchambua binti watu kiasi hicho!? Hapo kisa sio mahari tuu! Hayo maneno yameonyesha ulivyo na roho chungu na mbinafsi.

Kama hakufai si umwache? Au ukiambiwa umwoe bila mahari ndio unamwona mwanamke bora??

Tafuta wakubwa wakueleze maana ya mahari watakuambia Mahari ni kipimo cha kujua kama mwanaume yuko tayari kubeba jukumu la ndoa na familia.

Halafu ukiwa mwanaume ukapangiwa mahari kitendo cha kuikubali tuu ni alama tosha kwamba wewe ni mwanaume mwenye kujielewa, mpambanaji na mpiganaji. Mahari unaweza kulipa yote mahari unaweza lipa kwa awamu.

Halafu, Kama mahari imekushinda utaweza kulea mke na watoto?
Million 6 kwa binti asiye bikra ni matani hayo...hata million 2 ni basi tu!!
 
Million 6 kwa binti asiye bikra ni matani hayo...hata million 2 ni basi tu!!
Yaan kwanza kwann mthaminishe binadamu na hela?? Utu uko wapi??
Thaman ya binadamu ni kubwa haina kifani (priceless) hivo haipaswi kuthaminishwa kwa mahari maana ile sio bidhaa.

Nyie mtaanza kwa kusema asiye bikra ni milion mbili
Mtakuja kusema akiwa mweupe milion 3
Mtakuja tena akiwa mfupi milon 1
Mtasema tena akiwa kilema laki 2
Mtakuja tena akiwa kabila fulan efu50
 
usitufokeee waoaji ni sisi watoa mahali ni sisi tushasema hatutoi mahari kubwa bora nikanunue IST itanifariji kuliko kununua redio ndani kila wakat mikelele tuuh
Sema wewe kalaghabaho huoi kwa mahari inayotosha kununua
Wanaume wanaoa kwa mahari pamoja na zawadi za mamilioni magari na nyumba😂😂😂

Tafuta pesa buana acha unyonge
 
Mimi nakataa mahari. Nitatoa zawadi inaweza kuwa in terms of money au goods. Sioni mimi nalipia nini? Angalau hata ningemkuta bikra. Hakuwa bikra kabisa.
Mahari ni muhimu na ndio msingi wa posa, hizo zawadi ni wewe tu upendo wako kwa wazazi na walezi wa mkeo mtarajiwa.

Zawadi hutolewa wakati wa kupeleka barua ya posa.
 
Mahari ni kipimo cha kujua kama mwanaume yuko tayari kubeba jukumu la ndoa na familia.
Hoja mfu. Kuna watu wanatoa magari shilingi elfu 50. Na wapo waliobeba bure na ndoa zao ziko imara na zina amani.

Acheni kuwageuza mabinti zenu kuwa vitega uchumi. Yaani wewe mzazi umeshindwa kupambana utoke kimaisha unataka kutokea kupitia mahari??
 
shukrani au zawadi ndio mil 6 pesa haitafutwi ili ikatawanywe hovyo, mi sikatai suala la mahari lakini isiwe ya kukomoa
Na ndio ukiona wa milioni6 humuwezi katafute wa laki, kwani si wapo??
Lawama za nini!?
 
Hoja mfu. Kuna watu wanatoa magari shilingi elfu 50. Na wapo waliobeba bure na ndoa zao ziko imara na zina amani.

Acheni kuwageuza mabinti zenu kuwa vitega uchumi. Yaani wewe mzazi umeshindwa kupambana utoke kimaisha unataka kutokea kupitia mahari??

Na wapo wanalipiwa mahari na wanaume wenzao
Hizi lalama za wanaume zinawaingiza kwenye laana

Tafuta wa elfu50 unayemmudu. Wa milioni6 waachie wanaoweza😂
 
kwenye Familia yetu dada zangu [zaidi ya 5] washaolewa na hakuna alieolewa na mahari chini ya millioni 5 Cash.!! Ukijumlisha na kishika uchumba ni zaidi ya 6M, apo bado elfu 10 kumi za vijana zaidi ya 10, Blanket Kubwa la Wazazi, Vitenge vya Mashangazi zaidi ya 5, Sufuria Kubwa la Kupikia n.k

mtoa Mada njoo apa ututhibitishie kuwa wewe sio Upinde otherwise.. Man Down.!!! Need Back up
Na Wewe unaolewa kwa tsh ngapi? Wazazi wako nao mahari yao mtu akitaka kuwaoa tsh ngapi? Maana naona mnafanya biashara sana ya utumwa.
 
Watu wa jf bwana, its like we live in a different planet. Kwamba 6m kwenu ni pesa ya mboga tu? Kwamba anayetoa mahari ya 2m na anayetoa ya 10m mmoja ana thamani kuliko mwingine? Sasa kumbe kula na kunywa kushukuru wazazi kwa malezi kuna thamani tofauti?

You guys amuse me!!,

Milioni 2, au 10 au milioni6 utaona thamani yake kutokana thamani unayoitaka na uwezo wako
Ndio maana nimesema sio lazima uende huko kwa milioni 6 au 10. Unaweza kwenda kwa mahari ya elfu 50 kiroho safi tuu bila lawama
Hata wa bila mahari wale wa kuwalipia mahari wapo tena wanaume kwa wanawake😏😏
 
Milioni 2, au 10 au milioni6 utaona thamani yake kutokana thamani unayoitaka na uwezo wako
Ndio maana nimesema sio lazima uende huko kwa milioni 6 au 10. Unaweza kwenda kwa mahari ya elfu 50 kiroho safi tuu bila lawama
Hata wa bila mahari wale wa kuwalipia mahari wapo tena wanaume kwa wanawake[emoji57][emoji57]
Sioni sababu ya kuwakomoa vijana, na kusema eti kulipa mahari kubwa kunampa mtoto wa kike guarantee ya kuishi/kuhudumiwa vizuri nadhani ni mawazo potofu tu.

Kwa vile tumesema mahari ni asante na thamani ya mtoto wa kike haipimwi kwa kiwango cha pesa, mahari iwe reasonable.
 
Mimi nishakuwa mtu mzima, sio kijana tena. Na nimeshapokea mahari ya mtoto wa kaka yangu, so nina uzoefu kidogo kwenye issues za mahari.

Mahari haimalizwi yote, ila kwa tamaduni yetu kuna vitu ni lazima ulipe ili hiyo mahari ihesabike, sasa 6m unakuja na 1m nani akuelewe.

Watu waweke mambo yaliyoko kwenye uhalisia wa maisha ya wengi. Huwezi kumpa kijana anaanza maisha wazazi hawana uwezo eti alipe 6m, utakuwa hutumii akili, huwatakii watoto wako waanze maisha ya ndoa vizuri. Mahari should be reasonable.
Hata hivyo siafiki mahari kwa mwanamke ambaye hakuwa bikra.
Hao mabikra miaka hii HAWAPO don't waste your time.
Bikra zimebaki chache sana kwa watoto chini ya miaka 10.
Niamini mm nina umri wa zaidi ya 60+ (mstaafu)
 
Back
Top Bottom