kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Mama juzi kajisifu kukopa sana ili kukamilisha miradi aliyoanzisha Jpm, na kwamba atahakikisha hakuna hela ya mkopo inaliwa.
Watanzania tujue mabeberu walikua wanachukizwa na ari ya jpm ya kujitegemea na ile kuwafunza watanzania kwamba nchi yao ni tajiri jambo ambalo ni kweli. Aliwaonyesha mabeberu uwezo wa nchi yetu kujenga miradi kwa kujitegemea kwa kuanza na hela za ndani jambo lililowaudhi kwani aliweka mikakati kuhakikisha biashara za ndani na wawekezaji wanalipa kodi kufuatana na sheria na sio vinginevyo.
Nia ya mabeberu ilikua kutawala nchi kuhusu miradi gani tunaweza kufanyab na ipi hatuwezi au haturuhusiwi kufanya kufuatana na maslahi yao na sio maslahi ya nchi yetu. Pia ile jeuri ya kutaka kuruka kizingiti kwamba hatuwezi kujenga bila kukopa kwao kwa masharti yao iliwaudhi.
Nachotaka kusema kwa mama ni kwamba sio tu kwamba ahakikishe miradi inakamilika lakini awe alimuelewa jpm. Kwa hivyo asije ua ile fikra ya kujitegemea kwa kurukia mikopo kwa kila kitu na hasa ile isiyokua na tija bila kutumia kwa kiasi kikubwa nguvu yetu wenyewe. Atambue ubeberu moja ya nyenzo zao ni kuhakikisja tupo daima kwenye madeni makubwa yasiyolipika na hata kama yanalipika. Lazima pia kutambua mikopo ni biashara wala hakuna hisani.
Pia mama atambue vigogo wanaomzunguka wanapenda mikopo kwani ni hela ya kigeni inaingia wangependa kuipiga kwa kufanya dili mbalimbali hatimae mradi kua ghali sana au kupunguka ubora.