Anayefahamu kijijini wanakouzwa mashamba Kati ya laki 2 Hadi 5 anijuze popote Tanzania

Kweli mkuu unaweza ukaingia nao mkataba wa mwaka 1 wanalima mwisho wa mwaka unawalipa.
Tuliwai kufanya ivo tulipata vijana kutoka kigoma wakaja njopeka (nyamalonda ) mpimio kulima.
Sio lazima utumie wa hapo, unaweza chukua vibarua mikoa mingine hasa dom na kigoma ukawapeleka wakafanya kazi yako vizuri tu
 
Karibu HANDENI utapata mengi tu
 
Mkuu karibu Morogoro Mikese, shamba lipo ukubwa hekari 140, shamba lipo KM 7 kutoka ilipo mizani ya mikese morogoro, barabara inapitika muda wote, shamba limesafishwa na linalimika kwa trekta
 
Pwani Mkuranga Kata ya Mkamba mashamba yanapatikana ardhi ina rutuba huitaji mbolea
 
Asante Dodoma Wilaya gani na kijiji kipi na wanauza Kwa bei Gani?
Wilaya zote ni karibu vijiji vyote,isipokuwa kuna Kijiji Kimoja kinaiwa wotta_Mpwapwa wagumu kuuza.Bei ni kuanzia laki na nusu inategemea na muuzaji.Huko wotta ni watu waliohamia Toka Iringa kutokana na vita vya wajerumani na Wanyalukolo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…