Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Mara nyingi huenda sieleweki kwenye baadhi ya misimamo ninayoichukua hususani kwenye mambo ya kitaifa ya kisiasa. Mathalani mambo yanayolalamikiwa na wapinzani wa CCM.
Uzoefu wangu wa siasa za CCM, kwa yale niliyoyaona kwa macho, CCM haitegemei siasa za majukwaani hata kidogo kushinda uchaguzi. Ushindi wa CCM huwa unategemea vitu viwili vikubwa, UWT na Mabalozi.
Kwamsiofahamu, akina mama kupitia UWT huwa wanapitiana nyumba kwa nyumba kwenda kuwapigia kura wagombea wa CCM. Kwenye mchakato huu, kinachowaunganisha ni uwenzetu, hawashauriki, hawaambiliki kwenye lao. Kwakifupi ni kuwa, waweza kuwa mgombea, na mkeo akasombwa na wenzake kupigia kura CCM.
Nguzo ya pili ni hawa mabalozi. Yes, hawa mabalozi wa nyumba kumi kumi. Hawa watu kwa wananchi wa kawaida huwa wameaminiwa kuwa ndio viongozi wao wa karibu zaidi. As a matter of fact hawa ndio mashahidi wa mauziano ya ardhi, hawa ndio wasuluhishi wa migogoro ya ndoa, hawa ndio waratibu wa ulinzi na usalama kwenye maeneo yao. Wakati wa uchaguzi, mabalozi ndio wahamasishaji wakuu wa upigaji kura. Ahsubuhi ya siku ya kupiga kura, balozi hupita nyumba zote anazoamini ni za wana CCM, anaongozana nao kwenda kukipigia kura chama chao.
Kwa wanao lijua hili, nielezeni, upinzani wa Tanzania, una miundombinu gani ya kuwasaidia kushinda chaguzi zaidi ya malalamiko ya kuibiwa kura ambazo hatuna hata uhakika kama kweli huwa zinaibiwa?