Anayeijua nguvu ya CCM, Hawezi kupoteza muda kujibizana mitandaoni

Anayeijua nguvu ya CCM, Hawezi kupoteza muda kujibizana mitandaoni

downloadfile-25.jpg
 
Hakuna Silaha hatari kama mitandao...

Mitandao inaweza kumobilize majeshi bila command ya mkuu wa majeshi, nyie endeleeni kupuuzia mitandao
 
CCM wapo mpaka kwenye mashina huko vijijini, wanafanya mikutano na wananchi kila siku. Vigumu sana kuwashinda ikiwa CHADEMA na vyama vingine hawana uwezo wa kufika Tanzania nzima na kufanya siasa haswa katika miaka ile isiyokuwa na uchaguzi.

Kukuza mtandao wa vyama vya siasa itakuwa njia sahihi ya kuwa na vyama vyenye kuweza kupambana na CCM na kuitoa madarakani. Kusema wanaiba kura ni sawa na kukata tawi la mti wakati shina bado lipo.
Acha ujinga labda hawafiki kijijini kwenu, kama CCM wapo kila kona wanaogopa nini tume huru ya uchaguzi wanategemea polisi na tume fake ya uchafuzi?
 
Mara nyingi huenda sieleweki kwenye baadhi ya misimamo ninayoichukua hususani kwenye mambo ya kitaifa ya kisiasa. Mathalani mambo yanayolalamikiwa na wapinzani wa CCM.

Uzoefu wangu wa siasa za CCM, kwa yale niliyoyaona kwa macho, CCM haitegemei siasa za majukwaani hata kidogo kushinda uchaguzi. Ushindi wa CCM huwa unategemea vitu viwili vikubwa, UWT na Mabalozi.

Kwamsiofahamu, akina mama kupitia UWT huwa wanapitiana nyumba kwa nyumba kwenda kuwapigia kura wagombea wa CCM. Kwenye mchakato huu, kinachowaunganisha ni uwenzetu, hawashauriki, hawaambiliki kwenye lao. Kwakifupi ni kuwa, waweza kuwa mgombea, na mkeo akasombwa na wenzake kupigia kura CCM.

Nguzo ya pili ni hawa mabalozi. Yes, hawa mabalozi wa nyumba kumi kumi. Hawa watu kwa wananchi wa kawaida huwa wameaminiwa kuwa ndio viongozi wao wa karibu zaidi. As a matter of fact hawa ndio mashahidi wa mauziano ya ardhi, hawa ndio wasuluhishi wa migogoro ya ndoa, hawa ndio waratibu wa ulinzi na usalama kwenye maeneo yao. Wakati wa uchaguzi, mabalozi ndio wahamasishaji wakuu wa upigaji kura. Ahsubuhi ya siku ya kupiga kura, balozi hupita nyumba zote anazoamini ni za wana CCM, anaongozana nao kwenda kukipigia kura chama chao.

Kwa wanao lijua hili, nielezeni, upinzani wa Tanzania, una miundombinu gani ya kuwasaidia kushinda chaguzi zaidi ya malalamiko ya kuibiwa kura ambazo hatuna hata uhakika kama kweli huwa zinaibiwa?
Sio kweli
 
Acha ujinga labda hawafiki kijijini kwenu, kama CCM wapo kila kona wanaogopa nini tume huru ya uchaguzi wanategemea polisi na tume fake ya uchafuzi?
Ujinga mnao nyinyi mnaodhani mnaweza kupambana na chama kilichoanza kujenga mashina miaka ya 1977.

Tengenezeni mitandao mipana inayosambaa nchi nzima, vinginevyo mtaendelea kujibu hoja kijeuri kila kipindi cha uchaguzi kinapofika.
 
Back
Top Bottom