Waheshimiwa hebu nijuzeni kidogo,hivi huyu captain wetu wa nchi ndiye yule yule wa kipindi cha uchaguzi au kuna lijamaa limevaa ngozi ya captain?
Nakumbukuka kipindi cha kinyang'anyilo nilikuwa mkoani Mbeya,captain alipokuwa akiomba kura wananchi walikuwa wakipiga kelele za 'PEOPLE'S POWER', nilipomtazama kwa hakika niliona huruma,niliona jinsi watu walivyokuwa wakihitaji mabadiliko ya dhati na hawakuhitaji kijani kibichi kushika uskani tena. Alitia huruma,alikuwa innocent mpaka nikawaza ningekuwa na uwezo ningechapa viboko hawa wananchi.
Nakumbuka statement yake baada ya kuona upepo ukanda ule ni mgumu ikabidi nae aitikie 'PEOPLE'S POWER ila akamalizia kwa kuomba naombeni hiyo power nipeni mimi nikawaletee mabdiliko,mchuma ukawashwa wakasepa.
Jamani mimi kwa kweli sielewi,nini kinaendelea Captain wetu ni yule yule au nini kimetokea,au mimi sielewi. Sio siri nikiwaza huwa ninaumia sana.
Au anahujumiwa? Pengine ameingilia maslahi ya watu kwa uadilifu wake sasa anafanyiwa kuchafuliwa? Wateule wake wanampka mafuta kwa mgongo wa chupa? It doesn't make sense kabisa Captain ku act as if nothing wrong is happening. Captain aseme neno basi roho yangu iliridhike.
Mbona ni rahisi sana kuishika mioyo ya watu,mbele wanasema winning people's hearts. Sio siri huku mtaani ni kama captain anakuwa disqualified siku baada ya siku. Aseeme neno basi tujue ni yeye au hata yeye haelewi nini kinaendelea. Kama kuna mikono michafu ya mataifa uliyoingilia maslahi yao atuambie.
It doesn't make sense and no logic hata kidogo kutupuuza wananchi wako. Ajira hujatupa sawa tutajiari,umepunguza wafanyakazi sawa, sasa hivi waalimu wa sekondari wanarudisha shule za msingi,je hii kwako ina make sense?. Wafanyakazi ni manung'uniko tu, Mishahara ndo hivo,gharama za maisha baba zimepanda,au wateule wako hawakujuzi?
Sio siri mambo huku yako hovyo hovyo kabisa. Asiwasikilize hao watu wake wa karibu huko ambao tukilalamika wanamwambia eti tulikuwa wapiga dili eti mambo ni shwari.
Hao washauri wake vipi hawamwambii vipaumbele vya wananchi,wananchi wanataka nini,mbona kama anayoyafanya yeye ni ya kwake,mfano uwanja wa ndege chato,ni mshauri gani alimwbia apeleke uwanja wa ndege kule.?
Mimi binafsi naelewa kuwa ushindi wake aliutafuta kwa nguvu,alitumia ushawishi wa kiwango cha juu sana maana ushindani ulikuwa mkubwa,lakini je ndio ameamua kuutokomeza upinzani? Nani alimwambia upinzani unamalizwa kwa bunduki,kufungwa jera,kuporana mali na kutishana,nimwambie wananchi hawataki kaki wala kijani wanataka ile kweli,uongozi wa kweli,uadilifu,uwazi,haki na demokrasia. Yeye afanye hivo aone kama kuna mtanzania atakumbuka kama kuna makamanda,upinzani utajifia wenyewe hana haja ya kukimbizana na upinzani. Je anawatuma polisi,mahakama,tume wavunje sheria na katiba au wanamzunguka aonekane mbaya.?
Watu hubadilika lakini kama ni yeye captain basi mabadilko yake yamekuwa ya kasi sana.
Mwenye uelewa juu ya haya mabdiliko ya captain anijuze tafadhari.
Shukrani.