Hii aina ya uongozi wa kibabe aliyoichagua Magufuli inalizamisha Taifa.
Unapoburuza watu na kuwasweka mahabusu bila sababu yoyote ya msingi eti kisa unajivunia nguvu ya dola! kwanza huo ni ulimbukeni, alafu, unatengeneza chuki mbaya sana katika jamii maana, hao viongozi hawakutoka angani bali walichaguliwa na watu kwa mapenzi yao.
Huwezi kuwa na matazamo duni namna hii eti ukiwataifishia Mali zao, ukirundika mahabusu ndo unawashinda au unawagombanisha na watu wao, la hasha! huu ni upeo mdogo sana wa kufikiri. Hata jesi angekua na upeo mpana zaidi ya huu.
Nikukumbushe tu kwamba dunia ya sasa ni dunia habari kila mtu anaufahamu, kama unadhani unaweza kutumia style za kina nyerere za kukandamiza watu, basi unabahati mbaya sana maana utafeli vibaya zaidi ya Jes.
Na nyie ccm mnaoshabikia anachokifanya Huyu bwana nawapa pole kwasababu, hamjui kusoma alama za nyakati. "CCM inakufa kifo chepesi mno"