Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Jamani naomba waungwana mnisaidie maana ninachokiona huyu bwana pombe amekuja kulipa kisasi kwa wapinzani, ana hasira ambayo sio ya kawaida. Kumbe walivyokua wakiikosoa serikali yeye alikua anauma meno akisema moyoni labda Siku moja nisiwe raisi, maana ikitokea nikawa raisi watakoma. Sasa kawa raisi! niambie mtanzania usiye mnafiki, unaona nini juu ya Magufuli na upinzani? Na je adhma yake itatimia?
Mheshimiwa Rais aliahidi kupambana na ufisadi na si upinzani. Mpaka sasa hivi hajawahi kupambana na upinzani kwa taarifa yako tu. Anapambana na ufisadi. Tatizo lenu hamtaki kukubali kuwa kwa sasa huwezi taja ufisadi na kuuweka kando upinzani. Mafisadi wamejaa kwenye upinzani na ndiyo maana unaona hata wale waliokuwa upinzani wakipigia kelele ufisadi wamakaa kimya kabisa. Zamani walifanya kama drama na ukizingatia serikali iliwafichia siri so walijifanya kupiga kelele za mwizii kumbe wao ndiyo wezi. Rejea zile za wezi wa mifukoni hapo kale. Mwizi akikuchomolea visenti vyako mfukoni basi na wewe ukaanza kumkimbiza na kuita mwizi nae ataita mwizi so watu watashindwa kufahamu mwizi ni yupi. Kwa sasaa Magu kakaba. No more drama. Mwizi ni mwizi. Kwa hiyo msijaribu kujifanya hamuelewi wakati mnaelewa kila kitu.
 
Wakubwa msifute huu Uzi tunataka tujadili adhma ya huyu bwana, na hatima ya Tanzania yetu. Kuna shimo refu sana liko mbele sasa sijui linammeza nani.
Uzi wako hata hivyo ni wa low level sana hata wakiufuta ni sawa tu. Unauliza kitu ambacho jibu unalifahamu.
 
Anapambana na wapinzani, na wananchi ambao hawakumchagua ana hasira mnoo
 
You
Yeye hajaandika dikteta ni nani hasa. Wewe ndiyo umeandika hadi majina na kutiririka meeeengii. Hata hivyo kwani kuna udikteta hata ule uchwara tu mkuu wangu?
You are right wachangiaji wangekuwa kama wewe hakiamungu nchi ingesonga mbele. Unaonekana mstaarabu sana
 
I believe he has better plans for Tanzania...u see,Ana hizi plans he wants to carry out in ways he thinks are 'best'..kiasi kwamba wat other ppo r tryn to tell him..he's like..They don't understand what I'm doing but they will...so all the 'negativities' and 'oppositions' around him just frustrate him..cuz all he wants now is time and space and its not wat he is getting..u see this guy is quite unique n u jus cnt figure him out cuz u re tryn to face him e way u used to face the former leaders n Dats wat frustrates you cuz u want him to face e 'negativities' the 'opposition' e situations u want him to do 'ur' way.....u see? dats y its hard to understand wea we re or wea we re heading to..but make sure u know wea u re n wea u re heading to,ur life ur business..gv to Caesar wat it belongs to him.
 
Hii aina ya uongozi wa kibabe aliyoichagua Magufuli inalizamisha Taifa.

Unapoburuza watu na kuwasweka mahabusu bila sababu yoyote ya msingi eti kisa unajivunia nguvu ya dola! kwanza huo ni ulimbukeni, alafu, unatengeneza chuki mbaya sana katika jamii maana, hao viongozi hawakutoka angani bali walichaguliwa na watu kwa mapenzi yao.

Huwezi kuwa na matazamo duni namna hii eti ukiwataifishia Mali zao, ukirundika mahabusu ndo unawashinda au unawagombanisha na watu wao, la hasha! huu ni upeo mdogo sana wa kufikiri. Hata jesi angekua na upeo mpana zaidi ya huu.

Nikukumbushe tu kwamba dunia ya sasa ni dunia habari kila mtu anaufahamu, kama unadhani unaweza kutumia style za kina nyerere za kukandamiza watu, basi unabahati mbaya sana maana utafeli vibaya zaidi ya Jes.

Na nyie ccm mnaoshabikia anachokifanya Huyu bwana nawapa pole kwasababu, hamjui kusoma alama za nyakati. "CCM inakufa kifo chepesi mno"
 
Uhakiki wa watumishi hewa utaisha ndani ya miezi miwili tu baada ya hapo watu watalipwa madai yao na ajira mpya zitatoka baada ya halo uhakiki mpaka sasa unaendelea serikali haitoi uhamisho wala kupandisha madaraja wala kulipa malimbikizo kwa watumishi wa umma wala ajira mpya hazitangazwi tena serikalini hujui kuwa miezi yako miwili ilishaisha toka mwezi wa 8/2016 wewe ni mchochezi .

Takayechaguliwa chuo kikuu atapata mkopo asimilia nyingi waliopewa mikopo ni wachache huu siyo uchochezi ?

Zipo kauli nyingi sana anazotoa za kichochezi.
hahahhhh tatizo sheria ni kauli yake na sura yake....wewe ndo unaleta uchochezi shauri yake
 
Ni bahati mbaya sana kuwa falsafa ya mheshimiwa Rais ya kuwashusha walio nacho waishi kama mashetani bila kuhakikisha wasio nacho nao wanapanda kiuchumi imepokelewa bila kuhojiwa na wananchi.
Chuki imechukua nafasi na watu wako katika furaha kuu kuona watu wenye viwanda au biashara kubwa wanabanwa na kukwama waishi kama shetani hata kama jambo hilo litakosesha ajira watanzania kwa mamia.
Tumekwama kabisa kwani asilimia kubwa ya wananchi wamejikita kwenye falsafa hiyo na hawana matamanio ya kukua kiuchumi bali kuona wengine wakiporomoka
Ni wakati sasa wa kunwambia mkuu kuwa umewapoteza direction watu wako na hawawezi kuendelea kwani matamanio yao ni kuona tuu wengine wakianguka
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom