Anayejua Rais Samia anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani.

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari.

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena.

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
Tulishapotea tayari kabisa
 
1.Udini!!
2. Watu wasio na uwezo wa kutafsiri na kufikiri Kwa kina,wamejaa kwebye mfumo wa serikali.
3. Jinsia ile imejaa Kila Kona,kuja kuwaindoa sijajua tutatumia njia Gani.
 
Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani.

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari.

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena.

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
yaani kua watu wanaishi kwa akili za kuazima kweli yaaani anayofanya ssh huyaoni chizi kweli wewe
 
Samia shida yake kubwa anakosa Ile ruling power

Hana ushawishi wa kimamlaka

Rais lazima uchuje kila unachoambiwa sio kila ushauri ni ushauri mzuri

Unatakiwa uwe unpredictable ushauri mwingine unapiga chini

Pia Rais Bora ni yule anayesimama na wanachi hasa wa chini maana hao ndio wapiga kura

Mafisadi uwa hayapigi kura

Rais amefeli hapo amekumbatia kundi la wanyonyaji na kuuacha umma!!!
Ruling power anayo. Hakuna rais anayeikosa hiyo kauli thabiti yenye kuheshimiwa.

Tatizo akiitumia hiyo nguvu wengi tutaishia kuanzisha nyuzi za kulalamika humu humu jamvini.

Huwa tunapenda kusema kwamba SSH alimuua Mzee wa CHADEMA, nguvu ya mamlaka ya Rais ni kubwa sana.
 
Machawa hawataki kusikia huu ukweli

Ila Rais Samia ni Rais legelege kuliko Marais wote tuliowai kuwa nao ndio maana Taifa linakaribia kuanguka.

Mzimu wa repoti ya CAG na madudu yake mwaka 2021 tuliaminishwa madudu ni ya Magufuli!!

Je mwaka 2022/2023 madudu haya ni ya Nani?

Uozo kila Kona madudu na pesa kuchotwa!!

Bado mzimu wa Ngorongoro, Bandari ya dar, bandari ya bagamoyo, ujenzi wa Kijiji Cha kizimkazi, mikopo yenye riba Kali

Sasa tunadaiwa trion 100 bila Jambo lolote la maana toka Uhuru.

Vyote tulivyotumia kukopea pesa Sasa vinatia hasara taifa kwa sababu ya usimamizi mbovu!!

TANESCO, TCCL, ATCL, TRC Ni madudu matupu!!

Ulegelege wa Samia unakuja kwa yeye kutochukua hatua haraka na kuwafyeka wezi waliomzunguka to sad indeed !!!
 
TRC ina madudu gani? Mitegemea mabilioni ya kununua treni na kuijenga yarudi ndani ya mwaka mmoja wa kuoperate?
 
Hakuna report ya CAG katka historia ya nchi hii ambayo haikuwahi kuonyesha madudu, kama ni kulaumu basi kila kiongizi alaumiwe
 
Machawa hawataki kusikia huu ukweli

Ila Rais Samia ni Rais legelege kuliko Marais wote tuliowai kuwa nao ndio maana Taifa linakaribia kuanguka.

Mzimu wa repoti ya CAG na madudu yake mwaka 2021 tuliaminishwa madudu ni ya Magufuli!!

Je mwaka 2022/2023 madudu haya ni ya Nani?

Uozo kila Kona madudu na pesa kuchotwa!!

Bado mzimu wa Ngorongoro, Bandari ya dar, bandari ya bagamoyo, ujenzi wa Kijiji Cha kizimkazi, mikopo yenye riba Kali

Sasa tunadaiwa trion 100 bila Jambo lolote la maana toka Uhuru.

Vyote tulivyotumia kukopea pesa Sasa vinatia hasara taifa kwa sababu ya usimamizi mbovu!!

TANESCO, TCCL, ATCL, TRC Ni madudu matupu!!

Ulegelege wa Samia unakuja kwa yeye kutochukua hatua haraka na kuwafyeka wezi waliomzunguka to sad indeed !!!
Tanzania Maris wa maana na wenye Akili na wamefanya makubwa yaliyobakia Historia na hata kuiheshimisha nchi walikuwa ni Mahayati Nyerere, Mkapa na Magufuli waliobaki ni bure kabisa.

Nimemaliza.
 
31 March 2025
Kutaka urais 2025 ndiko kumesababisha yote, yaani kushindwa kutekeleza 4R zake alipoanza vizuri 2021

View: https://m.youtube.com/watch?v=Ku52ZOjs0oQ

Alikuwa na nafasi ya kuwa rais wa muhula mmoja akastaafu kwa heshima kama Nelson Mandela wa South Africa.

Mheshimiwa wetu angesikilliza ushauri wetu, kwa kutengeneza katiba mpya na kujenga mifumo ya reforms (mabadiliko) na kuisimamia katika miaka minne kisha kutogombania 2025, jina lake mheshimiwa lingebakia katika legacy ya kuwa rais aliyetengeneza mfumo wa haki na katiba mpya, jambo lililowashinda watangulizi wake.

Lakini mheshimiwa hakutaka kutusikiliza ushauri wetu baada ya wenzake ndani ya chama dola kumyumbisha na kumtisha kuwa jambo kuu kwa Tanzania ni CCM kubaki madarakani na siyo mifumo ya haki kupitia reforms za 4R

Kule nchini South Africa mheshimiwa Nelson Mandela jina lake linaendelea, kuimbwa kukumbukwa na kuwa mfano wa utawala bora kwa kuwa aliamua kuwa rais wa muhula mmoja aliyekataa kuendelea kuwa rais

Rais Samia Hassan naye angefuata 4R na kuendesha Reforms (mabadiliko) ya katiba, mifumo na sheria hakika jina lake lingebaki likiimbwa kuwa alikuweko rais shujaa wa haki na mifumo thabiti tena wa jinsia ya like aliyeweza kufanikiwa kuliweka taifa katika mstari wa haki na kufanikiwa hilo kuliko viongozi waliomtangulia ...
 
Anapiga hizi kelele akiwa Uingereza mwaka wa nne hivi sasa, yale yale ya mbwa koko anabweka huku anakimbilia getini.
 
Yuko kwenye right track,ila machawa wanamuharibia sana,i can see her vision...
 
Amani ni tunda la haki.

Kwa muda mrefu Tanzania imekuwa nchi yenye utulivu bila amani ya kweli. Utulivu umetokana na uvumilivu wa wananchi. Lakini ukweli ni kuwa uvumilivu una mwisho.

HAKI ndiyo hakikisho la kudumu la Utulivu na amani ya kudumu.

Mwalimu Nyerere alitamka kuwa kuwa tuna katiba ya hovyo ambayo Rais akikosa hekima na huruma anakuwa dikteta, na katiba isimzuie.

RAIS Mkapa, katika kitabu chake alitamka kuwa aliiba hela ya Serikali kuipatia CCM. Katiba kwa kuwa ni ya hovyo, haikumzuia wala kumwadhibu yeye na CCM yake. Mkapa akakiri kuwa nchi hii haina uchaguzi huru, wa wazi, na wa haki. Akasema kuwa angetamani Tanzania iwe nchi yenye chaguzi huru na za haki.

Licha ya wakuu hawa wa nchi kukiri ushetani wa katiba yetu, sheria mbaya za uchaguzi, na Taifa kutokuwa na Tume huru inayoweza kusimamia uchaguzi huru na wa haki, CCM ya sasa, Rais wa sasa na Serikali yake, wamegoma kabisa kuiondoa nchi kutoka kwenye udhulumaji wa haki za wananchi.

Siku zote, mtu anayegandamiza haki za watu, anaanzisha na kupalilia kuondoka kwa amani na utulivu, kwa sababu uvumilivu wa mwanadamu una kikomo.
Ni vema sasa, tukawatangaza kwa uwazi maadui wa amani na utulivu wa nchi yetu:
1. RAIS SAMIA
Huyu ndiye kiongozi wa nchi ambaye kama angekuwa na upendo na uzalendo kwa Taifa hili, alitakiwa kufanyia kazi maneno ya Mwalimu Nyerere na Mkapa, lakini ameungana na waovu maadui wa Taifa hili, kuhakikisha tunaendelea kuwa na katiba ya hovyo, tunakosa Tume huru ya uchaguzi, na kuhakikisha tunaendelea kuwa na sheria na kanuni za hovyo za uchaguzi.

2. CCM
Hiki chama ndicho kilichoandaa katiba ya hovyo na sheria na kanuni mbaya za uchaguzi. Hiki chama ndicho huwa kinashinikiza polisi, TISS na wasimamizi wa uchaguzi kufanya uovu.

3. BUNGE BANDIA LA CCM
WAkati wa mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, wananchi na taasisi mbalimbali zilitoa mapendekezo mazuri sana ambayo yangezifanya chaguzi zetu kuwa huru na za haki. Lakini wabunge wale bandia, waliungana kuyakataa mapendekezo yote ya wananchi na taasisi mbalimbali, wakatengeneza sheria za kishetani, na Rais Samia akazikubalia, ikiwa ni pamoja na yeye Rais Samia kung'ang'ania kuunda Tume ya uchaguzi inayowajibika kwake.

4. BARAZA LA MAWAZIRI
Baraza la mawaziri, kikatiba ndiyo baraza la ushauri la Rais. Hivyo Rais kusaini sheria ile ya kishetani ya uchaguzi, maana yake Baraza la mawaziri liliridhia.

Licha ya uovu huu mkubwa wa Rais Samia, Wabunge, CCM na Mawaziri, kwa upande mwingine, kuna watu au taasisi ambazo majina yao yanastahili kuandikwa kwa wino wa dhahabu kwa sababu wakati wote wamepinga uovu na kutoa ushauri ili nchi iwe na haki, na hivyo kuwa na amani ya kudumu:

1. CHADEMA
Licha ya vitendo viovu kabisa vya CCM vya kuhatarisha amani na utulivu, CHADEMA na viongozi wake, wakati wote imesimama na kukemea uovu kwenye demokrasia na kwenye masuala yote ya kupora haki za wananchi. Wameyatenda hayo yote bila ya kubeba rungu, panga au bunduki. Wakati wote wamehamasisha majadiliano ya kitaifa, lakini Rais Samia na CCM wameziba masikio na kutumia nguvu ya polisi. Dhamira njema ya CHADEMA inajibiwa kwa utekaji, uuaji na hata kesi za kubambikiziwa

2. TEC na Shura ya Maimam
Hizi taasisi mbili za kidini, hakuna hata wakati mmoja zilipokosa kukemea uovu wakati wa uchaguzi. Pia wakati wote ilipotokea nafasi ya kutoa maoni na ushauri namna ya kuifanya Tanzania ya haki na demokrasia ya kweli, walifanya hivyo bila ya unafiki wala woga.

3. TLS
Hii taasis ya wasomi wa sheria, wakati wote wameonesha ubovu wa katiba na sheria zetu katika kulinda mamlaka ya wananchi, katika kuwapata viongozi wanaowataka. Hata kwenye mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, walipeleka maoni yao, lakini lile bunge la waovu lilitatupilia mbali maoni mazuri yote toka kwawadau wote.

4. Jaji Warioba, Prof. Shivji, Joseph Butiku
Hawa wote ni wanaCCM, lakini ni wanaCCM wanaoipenda Tanzania. Hawa wakati wote wameweka bayana misimamo yao dhidi ya ugandamizaji wa haki za wananchi katika kuwapata viongozi wanaowataka.

5. Jaji Nyalali
Huyu kwenye report yake kuhusu katiba na sheria mbalimbali, aliweka bayana ubovu wote wa katiba na alitoa mapendekezo ya kufutwa sheria zote mbaya na zilizo kinyume cha haki za binadamu, lakini CCM aliyatupilia mbali hayo mapendekezo, na kuendelea kukumbatia uovu.

7. Mwalimu NYERERE RIP
Huyu licha ya kuiongoza Tanzania ya chama kimoja, angalo mwishoni aliweza kutamka wazi kuwa katiba ya nchi yetu ni mbaya, na hivyo inahitaji mabadiliko.

8. BENJAMIN MKAPA
Licha ya yeye kufanya uovu kama ule wa kuiba pesa na kuipatia CCM, licha ya yeye kuwa tunda la uovu wa CCM, lakini mwishowe alikiri wazi kuwa katiba yetu ni ya hovyo, sheria zetu za uchaguzi ni mbaya, na Tume yetu ya Uchaguzi siyo huru. Kwa kuyakiri tu hayo, anastahili kukumbukwa kwa wema.

9. Nape NNAUYE
Nape na January ni miongoni mwa waliwahi kudhulumu haki za Watanzania kwa kiwango kikubwa sana. Lakini sijui kama ni kwa dhamira njema au kwa bahati mbaya iliyo njema, alitamka wazi kuwa Watanzania huwa hawawachagui wabunge, madiwani, wala Rais, bali wale ambao huwa wamepachikwa kuhesabu kura.

Hawa watawala wa sasa wote, kuanzia Rais, mawaziri, wabunge na viongozi wa CCM, majina yao yatunzwe vizuri sana ili hata vizazi vingi vijavyo waje wasome na kuwatambua watu hawa waliowahi kuwa maadui wakuu wa Taifa, waliotumia nguvu zao zote kuulinda ugandamizaji wa haki za Watanzania katika kuwapata viongozi wanaowataka.

Ikiwezekana hata watu wa dini wangeendesha ibada maalum ya kuomba mkono wa Mungu uwafikie watu hawa ili waujutie uovu wao, na kisha wabadilike, ili wasibakie kwenye utawala wa shetani maisha yao yote ya kuwepo kwao hapa Duniani.
 
Back
Top Bottom