Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Best kuna watu wanaokota hela siku hizi zimezagaa mitaani hawatakuelewa. Wamelewa wanatema matusi hao hatari. Huhuhu
 
Hata timu ikishambulia kuna wakati huwa inashambuliwa pia, counter attack huwa hazikosekani mkipoteza mpira, muhimu ni kuhakikisha mabeki wako kwenye nafasi zao muda wote.
 
Nyumbu mama yako aliyekunyima malezi bora
 
Ina maana watu hawataki kuwekeza kwenye mahotel Dodoma?
 
Jamani nchi sio ya Samoa peke yake. Bali ni yetu sote. Tulianza utawala wa nchi yetu ndicho sivyo, kwa kuukumbatia mfumo wa Wakoloni - POLISI, MAHAKAMA NA JELA. Hivyo tumakuwa watwana katika nchi yetu. Tunsongozeka kwa sera ya chama tawala, badala ya SERA YA TAIFA.

Je! Baada ya miaka yake 10, tumlaumu Samia kwa lipi? Wakati ni huu. Marais Watano wamemtangulia, kodi wanalipa walioko mashambani, lakini barabara, mahosipitali, mashule, mahoteli na ufahari yanajengwa MIJINI.

Wanafunzi shuleni wanafundishwa kuwa sisi wanadamu tumetokana na manyani. Ni uzao wa manyani. Vile kijana mweusi akitua uwanjani ulaya, waulaya humdhihaki kuwa ni NYANI; TUNAKASIRIKA. Wapi na wapi? Syllabus inafunzwa hivyo. Sasa wanasiasa wetu wanalalamika nini, UN NY kwenye mkutano wa umoja wa mataifa, wazungu huwatoroka na kwenda kula , hawasikilizwi wakitoa hotuba zao. Kwani nyani ataema nini? Huwenda Raisat Samia jinsia nyingine, ayaone hayo arekibishe syllabus. Agundue pia mihimili ya nchi mitatu tuliyo nayo, miaka 60 baada ya uhuru wa Bender's ni SHIDA. Wao UK mihimili yao mitatu ni buckingharm palace, lambath palace na jumba la bunge 10 down street (amrisha kumi za Mungu chini mtaani)

WAO ULAYA NCHI ZAO ZINA DINI. ZINA UFALME -WHY?

SAMIA AONE MALKIA WA UK 70 YEARS KAFANYA NINI KWA NCHI YAKE ILIYO MASIKINI WA KUTUPWA?

WAO WAZUNGU WANA MAMBO WANAYO FANYA JUU YA MEZA, .NASI HUYAIGA KIBUBUSA. KUMBE WANAYO WANAYOFANYA CHINI YA MEZA.

JAMANI TUNATAKIWA KUANZA UPYA. TUJIPANGE - IKO WAPI ELIMU YA KUJENGA NCHI.

JAMANI, JAMANI UVYAMA TUACHE. WENZETU WAMETUZUNGUKA.
 
We huioni?
 
Tumepotezwa sana. Na sio Raisat Samia kutupoteza, LA.

Magufuli aliliona hilo LA kupotezwa. Akalijua na kabla ya kulifahamu, RAIA tukasikia kafariki kwa ugonjwa wa moyo.

Je! Raisat Samia tulipo potezwa atapafahamu? Ama naye ataendeleza kuteua wasimamizi wa UFISADI nchini mwetu?

UFISADI UKO WAPI?

Miaka siti, tunasimamiwa na mabaraza ya mawaziri. Wizara kuwa ndio kapu lenye matundu chini. Kila mwaka mabilioni ya pesa za wanyonge humwaga humo. Naye katibu mkuu kupitia idara ya manunuzi huagiza Mali kutoka viwandani ulaya na sasa brics. Mali zinazoliwa na kutu kwa ajili yao na ofisi zao. Huu ukitaka kujua, ndio UFISADI. Nao unaendelezwa mikoani na wilayani. Pesa ya bajeti nadra kufika kwa walengwa.

Kwa nini bunge LA bajeti lisidhinishe fedha kwenda kwa Madiwani, ambapo ndipo watu walipo? Kwani Mji mkuu wa nchi na miji mijuu ya ikoa na wilaya, ndio watu walipo? Kama watu wako kwa Diwani, kwa nini bajeti isipelekwe huko kama Waingereza walivyo?
 
Anaendekeza udini tu kashafeli, atambue kwamba yeye hajachaguliwa na wananchi, wananchi walimchagua magufuli sio yeye. Yeye ni rais aliyetokana na zao LA katiba yetu . Naona ummy anataka kufungua madrasa tamisemi
 
ELIMU YA KUJENGA NCHI:

Elimu ya kujenga nchi ndio roadplan yetu. Tusipoteze lengo LA suala letu Muhimu.Tulishaona kuwa Raisat Samia karithi Urais hali a kuwa nchi na watu wake TUMEPOTEA njia. Kwani kama taifa hatina Dira. Leo nchi unaongozwa kwa sera cha chama tawala. Ina maana kesho chama tawala kikiwa tlp, sera za tlp ndizo ziitakazo fuatwa. Na katiba za vyama vyetu vya siasa,vinadai kuwa hazina DINI.

VYAMA NA SERIKALI HAVINA DINI:

Hayati Magufuli akaliona hilo. Na yeye kama Rais akaja na kauli inayokiri kuwa Mungu Yupona TUMUWEKE MBELE. Nchi nzima mvua kwa miaka matano ya uongozi wake, ZIKANYESHA. Na chakula kwa wingi tukavuna na mazingira ya kijani kibichi tukaanza kuyazoea. Lakini ma malaika walipomnyakuwa, na Raisat Samia akatanguliza Jamhuri mbele badala ya Mungu, mvua zikakata na mazao sehemu nyingi yamekauka.

Kwa hiyo tunajifunza kuwa serikali, chama tawala na katiba, kutokuwa na dini ya taiga, hapo TUMEPOTEA.

Zingatia nchi za ulay, uarabuni, Asia, sote zina state religion. Kwa mimi sisi tuwe tofauti?

Waingereza ni Waanglikani
Warusi ni Mathodox,
Wachina ni Mabudha,
Wairani ni Mashia,
Wshindi ni Mahindu,
Wajerumani ni Waprotestant,
Wsitaliano, Waskandernavia, Wareno n.k ni Wakatoliki,
Waturuki ni Masuni,
Wasaudia ni Manswar; tunaona?

Keifa sisi mbona tuwe ni nchi tusio na DINI kitaifa?

Nchi zetu Baran'tu (AFRIKA), ni makoloni ya hawa wazungu ambao nchi zaho wana dini. Nasi tumejikuta wametushikisha dini za mataifa yao kama dhehebu au taasisi na au shirika; kwa namba yenye kutugawa tuwe makundi yasiyo patana. Haya wazungu walifanikiwa baada ya kuibomoa SERA YA MATAIFA YETU-
1) MILA
2) DESTURI na
3) JADI
iliyokuwa rafiki wa Mazingira. Jamii zetu zikawa na dini ile ile iliyoletwa na MANABII WA MUNGU -amrisha hizi 10-
1) Mungu ndiye kila kitu
2) Sharia, hukumu na Amri za Mungu ndivyo itikafi yetu,
3) Mila ya baba wa imani[kinyamkera] kusimikwa,
4) Jamii kuenzi MIIKO
5) Wazazi kuheshimiwa
6) Usiibe,
7) Usiseme uongo
8) Usizini,
9) Usiue na
10) Usitamani vya jirani, bali umpende kwa hali sote.

Hivyo ndivyo Wazungu waliwakuta Babu zetu wamesjika na kuzienzi AMRI KUMI ZA MUNGU. Leo wametufunza neno lao LA UPAGANI. Kumbe wako ndio wapagani. Nasi ni sana wa Mungu ASILI. Hakika wametushikisha UPOTOFU-
1) KATIBA isiyo na dini,
2) SETIKALI haina dini, na
3) MAHAKAMA yenye sheria za taifa lao;
kuwa ndivyo sera ya taifa letu. HAKIKA TUMEPOTEA.

SERA YA TAIFA LAO:

Wao Waingereza (mabwana zetu) wanaongozwa kwa MAJUMBA matatu~
1) Buckingham Palace alipo Malkia na ndiye Mkuu wa Kanisa, KWA HIYO DINI WAMEIWEKA MBELE.
2) Lambuth Palace alipo Askofu mkuu wa Kantibury, Yeye ni namba mbili baada ya Malkia. DINI WAMEOWEKA MBELE, na
3) Jumba la Bunge alipo Waziri Mkuu shahidi (JUMBA HILI MLANGONI LIMEANDIKWA 10 DOWN STREET [YAANI AMRI 10 ZA MUNGU ZISIMAMIWE CHINI MITAANI]), kuwa ndiyo dini waliyoishika.

Niambieni! Kwa nini utajiri wetu usimwagikie kwao walipokinga KAPU lao ~ utajiri wa pamoja {COMMONWEALTH}?????????????????????????????????????????????????????????

Je Sisi!??!!

Tunaongozwa kwa Majumba manne.
1) Ofisi ya Bakwata alipo Mufti asiye na amri wala hukumu na wala Haki
2) Kanisa Katoliki alipo askofu mkana sharia,
3) ikulu isiyo na dini
4) jumba la bunge la kutinga sheria,
Mufti na Askofu ni mahadimu kiimani. Tutegemee nini?
HAKIKA TUPO MBALI MNO NA UKWELI WA MAISHA.

MAISHA NI NINI?

Bila elimu hatuwezi kuchomoka walipo tunasa wazungu wakoloni......

Lakini Leo MALEZI kwa jamii zetu hayapo. YAMEFUTWA MNO........

ITAENDELEZWA
 
Urais ni taasisi. Tutamani taasisi yetu hii IJITAMBUE, IBADILIKE NA IACHE MAZOEA.

Tunameza doz tukitaraji tupone.
NIAMBIE.
 
Kweli tuko mbali mno. Tanganyika, yaani Tanzania bara, inatawaliwa na Muingereza. Bado sisi ni Koloni lake chini ya UKOLONI MAMBO LEO. Ndio maana Spika na Ujanja wake anaingizwa na kutolewa bungeni akiongozwa na ALAMA YA UTAWALA WA MALKIA Elizabeti -Heshima ya Malkia (SIWA).

Neno Tanganyika ni maneno mawili yenye maana kwa Wazungu. TANGA kwa maana ya kitambaa cha kukinga upepo baharini chenye kusukuma jahazi (sail). NYIKA kwa maana ya sehemu tambarare yenye kutanda NYASI (grassland).

Kwa hiyo jina hili TANGANYIKA kwao ni password - kutweka tanga nyikani, maana yake ni gateway to the hinterland (lango la kuingia ndani barani kwetu). Hapa walipo penya Tanganyika, wakaweza kukamata maeneo pande zote zingine.

Ajabu! Mtakatifu Nyerere naye akaendeleza umuhimu wa eneo tulipo, kuweza kusaidia kukomboa maeneo mengine kufikia UHURU WA BENDERA.

SASA:

Sasa ni zamu yetu tuone ni vipi tukwamuke kiuchumi, tamaa ya UMAGUFULI? Kasi hii isizimike hata akiwemo Mzanzibari. Muhimu ni kuwa na UONI (VISION). Uoni wa mrithi wa Magufuli na UTASHI wake vikijengeka kwenye KHULKA KUNJUFU, tutajitambua. Ndugu zangu acheni utani. Magufuli alisema hii ni vita ya UCHUMI. ULAYA MASIKINI INATEGEMEA KULALA KWETU WAZIDI KUZOA MALI NA UTAJIRI WETU. Tukianza uzanzibari na utanganyika, tutatoka kweli?

ZANZIBAR ni maneno mawili. ZENJ KWA MAANA YA WASHENZI NA BAR ni KISIWA. Kwa hiyo
Wazungu walikiita Zenjibar (Zanzibar) kwa maana KISIWA CHA WASHENZI.

Jamani, tuache utani. Tusome waliyofanyiwa Wahindi wekundu barani mwao........
 
We know there is puppet, the next objective is to know the puppeteers. time will provide us with an answer
 
Kwa makato haya ya huduma za kifedha za simu, hakika tumepotea.
 
Wanakata hayo ili wapate fedha za kulipia mradi huu wa wazungu (serikali kuu). Mawizara 23 Mji mkuu na kurejelewa mikoani na wilayani.

Lakini Taasisi yetu ya urais ingekuwa HURU, mji mkuu Dodoma zikawepo ofisi ya Rais, waziri mkuu, waziri wa fedha, madini, mafuta na gesi, na waziri wa hazina tu basi. Fedha ya bajeti ingewezesha serikali kuendeleza nchi na wananchi.

Na vile vile ofisi za mkuu wa mkoa na wilaya (kurugenzi) kuondoshwa ikabaki ofisi ya Mbunge, , trafa, diwani, amiri wa kijiji na amiri wa kitongoji/mtaa basi. Umangi meza ukafutika. Wasomi wetu wawe ni wajasiria Mali na sio wasaka ajira licha ya ajira kutokuwepo.

Ikulu ijitambue na hivyo kutekeleza madaraka VIJIJINI. Nguvu zote kuelejezwa vijijini, ni miaka mi3 tu tutajikuta NCHI uchumi wa kwanza na sio kilemba walichotuvika cha uchumi wa kati chini.

Ndugu zangu HOJA tuchangie kizalendo zaidi. Nchi ni yetu, lakini twapangiwa hili tufanye, lakini kile tusifanye. Yeye Samia tumzingire asiwe mshumaa. Tusipofanya hivyo, vizazi vyetu pindi 2045 ikijaliwa kufika, vitahilikishwa kwa risasi za rashasha, kwa usimamizi wa UN KIINI KIPYA (UN NEW YORK). KISINGIZIO NI MAGAIDI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…