Mwanzoni ulipoingia madarakani, ulikuwa ukienda vyema. Kwa hilo pongezi ulizipata na matumaini mema yakaanza kurejea.
Pote palipokwenda kombo kukiwemo:
1. maongezeko ya kodi na tozo mbalimbali katikati ya janga la Corona,
2. kutozingatiwa kikamilifu kwa mapendekezo yakiwamo ya tume mbalimbali na wenye dhamana akiwamo CAG,
3. kuwepo kwa ubaguzi mbele ya sheria ambapo vigogo ni daraja tofauti, kodi hamlipi, chanjo mmepata, sheria nyingi haziwahusu,
5. kutokuzingatiwa kwa utawala wa sheria.
Ikiaminishwa kuwa hayo yalikuwa ni mapungufu ya watendaji wako tu. Ukisifiwa kwa kuyaweka maslahi zaidi ya taifa mbele dhidi ya mengine yote.
Wapo waliokuwa na mashaka nawe wakikuelezea mithili ya mama wa kambo:
Ni wazi kuwa vitimbi vyote vya polisi Mwanza na ukimya wako, ni kwa sababu yote ni kwa maelekezo yako.
Umeonyesha katika wanao kumbe kuna yatima pia.
Leo mnakamata watu na kuwapekua mkitafuta vifaa vya kutengenezea katiba mpya.
Yaani mnatafuta computer, karatasi, kalamu na vichwa vya watu.
Ujumbe utakuwa umefika.
Yatima hawako salama tena.