Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Ni kufa tu. Dunia imefikia mwisho. Kirus cha covid 19 ndicho kinazungumza nasi. Sio Mungu (biblia/qur'ani) tena. Umoja wa Mataifa NY una idara 19. Na zote zinaongozwa na Wayahudi. Taifa pekee duniani lisilo na nchi. Taifa lililolaaniwa na Mungu. Viongozi wetu ndipo wanapotuelekeza kwa ajili ya uongozi na maisha.


Ah!!!!!
 
COVID 19, namba hii kujitokeza hapa ni kwa bahati au ni nini?

Aya ya kwanza kwenye Msahafu Q1:1 ina herufi 19.

Moto wa jahannam, una walinzi 19.

TUSOME:

Mimi sio shekhe bali ni mkereketwa wa Qur'ani. Hii namba kumi na Tisa iko kwenye huyu mdudu COVID 19, WHY?

Huu moto wenye walinzi 19, ni nini hasa? Kwa vile Qur'anic ni kwa nyakati ZOTE, Wakati wetu huu moto ni nini?

Lazima tujiongeze.

Ah! Mbona UN NY ina Idara 19? Bila shaka huu ndio MOTO. Upo nasi hapa duniani na tumeuelekea.
Mungu Anasema hatutalipwa ila lile tulilolifanya.

Kumbe motoni tutachomwa kwa sababu hapa duniani tulielekea jumba la UN NY na BRUSSELS, na VIENA, na PARIS, na LONDON badala ya Makka, Jetusalemu, Madina, Baghdad, Alexandria, Timbuktu, Barawa na Kilwa.

Marais wetu ili wapewe pesa wameuelekea moto (Ulaya na Marikani). Magufuli kama wachina, wajapani, wakorea, wahindi, alikataa hela zao za uchaguzi. Samia ameteleza akapokea, oh!

Mungu Anatubainishia sikia ewe Kijana wa Jana:

"Na hatukuweka walinzi wa huo moto (UN NY -umoja wa mataifa new York), ila malaika (Wakurugenzi wa kiyahudi), wala hatukuifanya idadi yao hiyo ya 19 ila kuwa mtihani kwa wale waliokufuru (walio IPA kisogo Makka na Jerusalem na kugeuza nyuso zao kuelekea New York na Brussels, ili wawe na yakini waliopea Katiba iheshimiwayo (ufu 5:1, 6, 12; Q 1:1-7), na walioamini (wazalendo -k.m Mtakatifu Magufuli, Tom Mboya, Sokoine, Jumbe, Sankara, Gaddafi, Nyerere, M.L. King n.k) wazidi katika Imani yao, wala wasiwe na shaka wale waliopewa KATIBA, wala WAZALENDO, na ili walio na ugonjwa nyoyoni mwao (MADEMOKRATI) na waliokufuru (WAKOLONI) waseme - Amependelea nini Mwenyezi Mungu kwa mfano huu? Hao wamepotea na Anawaongoza WAZALENDO. Wala hakuna ajuaye majeshi ya Mwenyezi Mungu (covid 19 kumbe ni jeshi LA Mungu) ila Yeye tu. (Katuletea jeshi hili) ni ili tukumbuke.
{Covid 19 -UN NY na idara zake 19} Ni ONYO kwa Binadamu
Q74:30-36

aaaaammmiina
 
Hata Mwendazake mlimtetea hivihivi na sasa amebaki mifupa
 
Utaratibu wa Makamu wa raisi kuwa raisi akifa raisi haufai kabisa, sahihi watu warejee kwenye uchaguzi wapate chaguo lao
 
Kuongoza watu kinyume na matendo yako upelekea watu wakadharau kila hatua unayotaka kupiga kwenda mbele lakini wasaidizi wako ufika wakati wakafanya just kutimiza wajibu wakuingia kazini na kutoka. Nadhani tumefika mahali hapo ambapo kila tunalosema siyo tunalotenda na vyote tunafanya mbele ya jamii. Naomba nieleze mambo machache ambayo yanathibisha uongozi umepoteana kwende dira na malengo

1. JPM akiwa Rais, Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, na mawaziri wengi wa Sasa pamoja na wakuu wa wilaya na mkoa walikuwa Hawa waliopo madarakani kwa Sasa. Wote kwa umoja wao walituaminishi Taifa Lina pesa na Kodi inayokusanywa nikubwa Sana. Pia walienda mbali zaidi wakatuambia Tanzania hakuna Corona na tusichukue taadhari. Nao pia wakawa mstari wa mbele kutochukua taadhari. Ikapelekea tukapoteza nafsi za watu wakiwemo viongozi wakuu wa serikali lakini msimamo ulibaki hivyo hadi alipofariki JPM. Leo Tanzania wanatangaza Kuna corona na ili tuendelee tunapaswa kutoa Kodi ya uzalendo. Watu Hawa wamesoma na Wana imani ya dini ila kwa ufupi unaweza ukasema kwao afya zao si muhimu wala afya za wananchi si muhimu, Cha muhimu ni kumtii kiongozi aliye mbele yao awe anadanganya au adanganyi wao kwao utii wa binadamu unazidi hata utii wao kwa Mungu. Tumepoteana.

2. Baada ya JPM kuondoka tumetangaziwa kwamba Kuna corona,tumeambiwa Delta ipo nchini na tumepokea msaada na mkopo kupambana na Delta. Lakini pia tumepokea dawa miliaoni moja kutoka kwa wamarekani na siyo mabeberu Kama alivyotuaminisha Prof. Kabudi. Pamoja na kupokea hivi vyote na kutangaza kuanza kuchukua taadhari unamwona Waziri Mkuu akiwatangazia watu wachukue taadhara huku akiwa amewakusanya mamia kwa mamia na uoni aliyevaa barakoa. Unamwona Waziri wa fedha amekusanya watu Tunduma huku Ummy akiwa kakusanya watu Tanga kwenye Mpira. Nyumbani kwa Makamu wa Rais Kigoma wanakutana zaidi ya watu elfu kumi na Saba kwenye Mpira wa Yqnga na simba. Lakini haya yakiwa yanatokea kila mkuu wa mkoa na wilaya anatangaza tuchukue taadhari si kwamba anaweza kusimamia hiyo taadhari ila naamini kwa sababu mama kasema. Tumekwama.

3. Tunasema adharani kwamba JPM alikosea kuweka watu ndani kwa kesi za uhujumu uchumi na Ugaidi na tunaelekeza watu hao bila kusikiliza wanafutiwa kesi na kurejea mtaani. Tunawaomba wawekezaji waje Hali imetulia, maana yake tunaamini alipokuwepo JPM Hali ilikuwa haijatulia. Tunamka adharani watu waache kuficha fedha nje wazilete nchini na mwisho tunatangaza maridhiano na kuanza kujenga nchi. Wananchi wanafurahi nakuanza kufanya kazi huku wakiwashawishi marafiki zao waliokimbia nchi na kukimbiza mitaji warudi kazi iendelee. Sijui Kuna mzimu gani huko wanapokaa watawala aidha magogoni au chamwino. Watu wanapoanza kuingia tu nchini tunamkamata Mbowe na wafuasi wake, tunakwenda mbali zaidi na kuitangazia Dunia kuwa tumemkamata mshukiwa wa Ugaidi. Dunia inasikia na inahifanya hii ndiyo habari kuu kwenye vyombo vya kimataifa. Kinachofuata badala waitangaze kwa wema wanaanza kutangaza nchi haina utawala wa sheria wala demokrasia. Matokeo yake wawekezaji waliokuwa wamefungasha mabegi wanayarudisha ndani kwa kauli mbiu tusikilizie Kwanza wamalize Ugaidi. Uchumi unadumaa. Tumepoteana.

4. Wakati haya yanatokea Waziri wa fedha anakwenda kupambana na taarifa ambazo hazijathibitika kwamba Watanzania wanakimbia nchi na kwenda kufanya biashara nje yaani Zambia. Kitendo hiki kinatafsiriwa kwamba Ni kweli Hali nchini siyo swari na Watanzania wanakimbia kwenda nje, TBC na vyombo vingine vinaifanya hii kuwa habari kuu wananchi hata wale wakijiijini wanaanza kudadisi wanakuta Kodi imependa wanashangaa awqtumiwi Tena pesa maana watumaji wanayaofia makato, hofu inatawala tunapoteana. Hatujakaa vizuri unasikia Tanesco nao wanakuja kusema wanakiji na wapiga kura wanaotumia chini ya unit 70 kwa mwezi ambao walikuwa na bei nafuu ya umeme wengi wakiwa ni wale wa REA watalipa Kama watu wa mjini. Yaani elfu tano units 14 kutoka units 40+ , tunaelekea wapi? Umeme ndio unaotumika kuzalisha huko kijijini kwa kutumika kukoboa nafaka, kuchomelea kwa mafundi na kuwasaidia watoto waweze kujisomea. Tumekwenda kuzima taa watoto wakalale. Tumepoteana.

5. Mkuu wa nchi anasikia wananchi wanalalamika anaunda tume lakini kabla ajapokea ripoti anajitokeza nakusema adharani too ipo palepale, hiyo tume inaweza kushauri kinyume na msimamo wake, jibu Ni No na hata Kama walipanga kushauri kinyume Basi usiku huu Wapo wanafanya editing. Tumekwama

Endapo tutataka kujikwamua hapa tulipo hatuna budi kwenda kwenye majengo yetu ya magogoni na chamwino na kuparejeshea utakatifu. Hakuna mtu anathubutu kuchezea msikiti Wala kanisa, kumbuka Yale Ni majengo Kama mengine na hata Polisi wanapaogopa. Kinachofanya nyumba za ibada ziheahimiwe ndicho kilichokuwa kinafanya ikulu iheshimike. Mchujo wakumpata Mufti na Askofu katika taasisi za dini ndio ulikuwa unatumika kupata viongozi wakuu wa nchi na walikuwa wazuri wakusikiliza ila walikuwa na masikio mengi. Siku hizi naamini tunaweza tukawa na mtu sahihi lakini akakosa masikio yakusikia kwingi kabla ajasema. Kumbuka akisema ndo mwisho, hivyo anapaswa Sana na kuhakikisha anasikia kabla ya kusema ameaikia.

Tukubaliane tumepoteana, tunarudi vipi sehemu sahihi? Ni kwa Mwenye nchi kukaa kwenye kiti akasikia Sana na kutoka pale tu anapoamini amesikia sawasawa ili atuambie alichokisikia anakionaje na msimamo wetu kwenye tunayoyasikia Ni upi.
 
Tume iliundwa ili kushauri namna bora ya ukusanyaji na upangaji wa tozo hizo. Ni wapi uliambiwa tume imeundwa kuja kufuta tozo, kama suala ni kufuta ingefutwa tu pasipo kuunda tume.
 
Huko ulaya wapo bize wanapambana na Corona, mwekezaji gani aliyefungasha begi kuja TZ akahairisha kisa mchepuko wako Mbowe ni mshukiwa wa ugaidi!?...
 
tangu Nabii aondoke Taifa linazidi kuyumba,natumain hii Tanzania itakuja simuliwa ktk biblia ya miaka 1000 ijayo
 
Tumeingizwa cha walemavu bila kupenda Tu ataka katiba mpya na tume hulu ya uchaguzi
TUME HURU YA UCHAGUZI:

Tumeona na kukubali kuwa KATIBA YA JMT toleo la mwaka wa 1977, SIO.

SIO! Kwa maana si KATIBA, bali ni kitabu chenye kuonyesha mfumo wa kikoloni walivyoweza kutawala MAKOLONI yao (WASHENZI) kwa mbinu ya kuwatia KHOFU.

KHOFU:

KHOFU ni dini ya wakoloni watawala waliyoturithisha. Ni UTATU MTAKATIFU TISHIO -
1) POLISI,
2) MAHAKAMA na
3) JELA.

Kwa vile shughuli za maisha ya kila Leo, wewe RAIA hujashikwa na polisi, uko huru hata kuasi AMRI KUMI ZA MUNGU. Kwa hiyo serikali zetu watu weusi, hazina habari na MASUALA ya Mwenyezi Mungu (DINI) na dhahiri hutangaza kuwa serikali haina dini.

Kumbuka tunaambiwa SERIKALI ni WATU. Basi! Ikiwa serikali ambayo ni watu haina dini, ina maana watu hatuna dini. Simple Aljebra-!

TUSHANGAE:

Inakuaje serikali ya uingereza, sio ya watu, bali ni ya MALKIA/ MFALME? Tena rejea sherehe ya kutawazwa Malkia Elizabeth II (corronation) ya mwaka wa 1953; Aliapishwa kuwa mkuu wa Kanisa LA anglikan na mkuu wa taifa. Na pia kuwa ni Malkia wa great Britain na nchi za Jumuia ya madola (COMMONWEALTH -utajiri wa pamoja). Nchi ni yake na Waziri mkuu ni mwanaye licha kwamba hawaiti watoto wa Malkia kaka au Dada.

Jumba la bunge alipo waziri mkuu mtawala linaitwa 10 DOWN STREET (YAANI AMRI KUMI ZA MUNGU CHINI MITAANI). Na hawana KATIBA iliyoandika na wao kama sisi walivyotuandikia. Bali wanafuata SHARIA ZA KIBRITISH NA MILA ZAO, kama babu zetu weusi walivyokuwa- Mila, Desturi na Jadi. MALKIA ni wa kudumu na hana CHAMA.

Wao, kiongozi wa nchi akihisiwa na nyumba ndogo-- OUT (Anatumbuliwa).

AMINI USIAMINI:

Inakuwaje nchi zetu tuna mfumo tofauti na huo?

Rais ndiye mtawala, SIO kiongozi wa dini, ana vipindi, ANA CHAMA TAWALA n.k. Suala LA dini ni binafsi, hata ukitaka kuwa mkana dini, sawa.

Na ili kutufanya tuwe kama wanyama, wakapigilia MSUMARI - MIHIMILI YA NCHI MI3~
1) katiba ya nchi,
2) serikali isiyo na dini. Ni ya wasomi wahitimu wa elimu iitwayo elimu kwa uongo 1 tom 6:20 na
3) mahakama ya kikoloni.

Haya wameturithisha baada ya kutugawa kiitikadi. Tuko wale waliowaitikia kuwa Yesu mungu wao, ndiye Mungu.

Na hawa wa taasisi za misikiti wanao kirihika pakitajwa eti Mungu ni watatu.
Ah!!!!

KWA HOJA KAMA HII, WALE WENYE ELIMU YA AKIDUNIA (sekyula edukesheni)) NAO NDIO WALIOTUNUKIWA KUKAA BADALA WAKOLONI KWENYE UTAWALA WA NCHI, ili kukwepa msuguano huo, wakakubalisha kuwa serikali, ikulu, KATIBA na vyama vya siasa visiwe na dini. Kwa hiyo sisi na nchi zetu tumekuwa wapinga Kristo (rejea yuda 1:4) ~MAKAFIRI bila kujua licha ya kupakwa rangu kwa majina ya kizungu na kiarabu.

UJAMBAZI DHAHIRI:

Eee!

Wazungu masikini wa rasilimali, wako JUU. Wajapani, Wachina, Wahindi, Wakorea n.k; wakuu wao hawakumkiri mungu wa Wazungu, tunawaona Leo wako mbele. Why?

SISI na utajiri kefu tulionao, tuko chini kuliko walio chini. Why?

TUMEUZIWA MBUZI KATIKA GUNIA:

Leo nimevaa kanzu, naitwa Muislamu.

Ehe! Uislamu ni nini?
Uislam ni jina LA dini lililotujia kwa lugha ya kiarabu. Je, kwa kikikuyu, Kipare, kichaga, kiswahili, kisukuma n.k neno hili unasemaje?

Vivyo hivyo UKRISTO, kwa lugha zetu, unasemaje neno hili? Hakika tumeuziwa mbuzi katika gunia.

Wazungu nchi ZAO zina dini ya ukanisa, waarabu na wayunani nchi ZAO wana dini ya kiislamu. Wahindi sana uhindu. Wajapani, wachina, wakorea, wavietinamu n.k sana dini za kishonzi, kihindu, kibudha n.k.

Nasi weusi kumbe ni uzao wa kinabii, dini yetu ni UHANIF {UNYENYEKEVU} Q3:67.

Let us find our ground, so that we can stand up and proclaim our true faith.

TUJIONGEZE:

Mimi chama tawala niko madarakani, wajumbe wa tume ya uchaguzi nitakuachia wewe chama pinzani UNIPANGIE?

Leo Yuko CCM. Kweli tukubali tuwe na tume HURU? Na kesho kweli Chadema UMESHIKA HATAMU, tukuamini kuwa hutarudisha tume kuwa KANDAMIZI kama unavyodai?

Mkuki kwa nguruwe ni mtamu, lakini kwa BINADAMU ni mchungu.

Ndugu zangu, tumeshikishwa MKENGE.

Wazungu watawala wametukamata pabaya. Kuchomoka SIO kwa kuwategemea wasaka AJIRA [wahitimu wa vyuo vyetu ambavyo ni kopi and pesti].

Something have to be done.

Huraaaaaa!

MAGUFULI AKAANZA - * "Mungu tumuweke mbele".
SAMIA KAAHIDI kuendeleza......

EEEEMMMIIN!
Let us not forget.

VIPI TUMUWEKE MBELE. KWANI YUKO NYUMA?

Na ni nini hicho chenye kuwekwa mbele, ambacho ndiye MUNGU?
 
Hata Mwendazake mlimtetea hivihivi na sasa amebaki mifupa
Bro, nisamehe. Komenti yako hii nimeshindwa kuvumilia.

Mimi Magufuli hakuwa chaguo langu. Simtetei, bali WEWE UNAHITAJI KUJITAMBUA, UBADILIKE NA UACHE MAZOEA. jua kuwa KUONA NI KUAMINI.

Tunachotakiwa kuona humu kwenye viwanja hivi, ni fikra za kujenga (constructive ideas) na sio lugha chafu kwa Marehemu wetu. Kesho ni wewe au mimi. Utapenda kuitwa MIFUPA.

Watake radhi washiriki wenzako kaka.
Asante. Mungu akubariki.
Eeeemmmiin
Oh!!!
 
Hata Mwendazake mlimtetea hivihivi na sasa amebaki mifupa
Tatizo sisi ni selfish, tunatumia mihemko na hisia katika kutatua matatizo, mpeni muda mama, mbona ni mapema mno mmeshaanza kulalama!
 
Mkuu Kajiarashid nashukulu sana kwa majibu mjalabu lakini tulejee hapohapo kwenye tume Tume ikiwa haina upendelo tutapata viongozi halisi watakao tokana na matakwa yetu na. Si matakwa ya wenye polis lakini pia tutakua na Uhuru wa kuchagua watu na so chama Leo hii watu wanavunja hata hizo kanuni zetu mbovu tumewasikia kwenye uchaguzi uliopita wakisema msipochagua wa chama changu hampati maendereo dah kwani maendereo yamekua hisani kisa tu tumechagua chama cha mwenye mamlaka? Hii si sawa tutakapo wapumzisha mfano Ccm sio kwamba tutakua tumewatupa jumla tutawapumzisha ili kupisha mawazo mapya angalau nao wapate kuonyesha nini kipya wanacho lakini kumbuka uccm na uchadema tunautafasili kana kwamba wengine wasudani wengine ni watanzania kumbe haya yote ni zao moja la mama Tanzania kwa zana hii ya uccm Tanzania sana na uchadema sudani uanakuja kuzaa kutokuelewana maana ni mbegu inayopandwa na inamea kwa kasi sana ccm wanajitahidi kuwapumbaza watanzania kuwaaminisha kwamba viongozi mwenyesifa anatkiawa atoke ccm kumbe uongozi ni wito anaweza akawa mwana ACT ndie mwenye wito wa uongozi na wewe umetukalilisha tuchague ccm hebu tulejee hapa nyuma kidogo kuna watumwa wa kisiasa walinunuliwa kwa lupia zetu leo wapo ccm na wanafanya vyema pengingine kuliko CCM wenyewe hii inatupa imani kwamba mambo ya kulazimishana kuchagua chama badala ya watu nitatizo tuliloaminishwa na hao ndugu zetu ccma hatimae ile mbinu ya kutupumbaza imepitwa na wakati wameamua kuanza kubambikia watu makes kama njia yakuwaaminisha watawaliwa kua hawa hawafai na hawa wanafaa sana huku wakiendelea kukwiba lasilimali zetu kifupi hatuwakatai ccm ila tuwapumzishe ccm wapate kujua kwamba hakuna aliezaliwa maalum kuongoza uongozi ni kupokezana
 
Naomba tutoe mchango yakinifu usio kuwa huu mfumo wa utawala wazungu walioturithisha.

UKWELI UKIDHIHIRI, UONGO UTAJITENGA:

Soon nitajaribu kubainisha kuwa tuwe na vyama vitatu tu. Lakini sera ni ya taifa na sio chama. Tuwe na ilani ya uongozi na ilani ya utawala za kitaifa.

Na hatuhitaji TUME YA UCHAGUZI, ila jopo LA wazee mfano house of lords kule Uingereza.

Na mengine mengi matamu tutaonyesha.

MUHIMU ni tufikie-
1) MAISHA BORA na
2) UHAI (Rehema ya Mungu).
 
Tatizo sisi ni selfish, tunatumia mihemko na hisia katika kutatua matatizo, mpeni muda mama, mbona ni mapema mno mmeshaanza kulalama!
DUNIA:

Vumilika, Mapito Mwanza, nawe Kijana wa Jana, mimi ni Mzee wa juziii! Lakini hebu tushee fikra mujarabu pamoja.

Dunia ina UMBILE. Nalo lina TABIA.

Tabia ya UMBILE la Dunia, lina thubutu kwa Mwanadamu ili kuweza kufaulu, ni kwa kuyashika kwa kujua mambo MATATU- MAISHA, UHAI NA ELIMU.

Ni Wakoloni watawala wakijificha nyuma ya wakoloni Wamisionari, Utatu kama huo-
1) Maisha,
2) Uhai na
3) Elimu;
waliuita UTATU MTAKATIFU, fumbo la Imani. Lakini kwa upembuzi wetu, tatu tatu ziko nyingi. Kwa lugha ya Maandiko Matakatifu, UTATU MTAKATIFU, ndicho KITU kilicho MAARUFU. Bali Tatu Tatu hizo, tutazikabili kila moja muda wake ukifika.

UTATU, TABIA YA UMBILE LA DUNIA:

Katika Mwadamu kuwa sehemu ya Dunia, yaani MTU na MAZINGIRA; utawala (serikali) ijitambue kwamba, mafanikio ya watu wake, yako kwenye MTIHANI (KUTAHINIWA). Ili binadamu kuweza kuishi (MAISHA ni nini?), lengo ni aweze kudumu kuwa hai (UHAI ni nini?). Na hayo, yanahitaji elimu (ELIMU ni nini?). Kwa hiyo, serikali isipo UJUA UTATU huu-
1) MAISHA,
2) UHAI na
3) ELIMU,
Vinavyo tegemeana, mahusiano yake, ukaribu wake, ukweli wake na UMUHIMU wake; itawaingiza RAIA wake kwenye mifumo ya maisha ya kufikirika, kwa gharama kubwa na hasara isiyo pimika. Kwani kama Vumilia alivyo pima, UBINAFSI ndio tulio ukumbatia.

Nitapata nini kwa ajili yangu na familia. Ni MIHEMKO tu.

Wazungu wametulia, wanatuchunga tusitoke hapo. Ni malumbano, ni kebehi, ni dharau, ni ghadhabu; vyote vinapinga upole, busara na hekima, ndicho wazungu wakoloni wanavyo tuelekeza tuvidumishe kwa istilahi ya DEMOKRASIA.

Ndio maana, Mzee Nyerere alikuwa bayana, VIJANA tutafute ELIMU kwanza, ILI KUWEZA KUJENGA NCHI. Kwa hiyo akaja na UHURU na KAZI. UJAMAA NI IMANI n.k.

Mwinyi akaendeleza uhuru na kazi, ujamaa ni imani; akiamini iko siku vijana watakuja na ELIMU, tujenge nchi.

Kijana wa kwanza kuja, akawa ni MKAPA. Akaja na UKWELI na UWAZI na kuishia mtaji wa masikini ni NGUVU zake. Ile ELIMU hakuja nayo.

O'o ooo!
Kijana wa pili KIKWETE, yupo. Akaja na yake. Yale ya Nyerere na Mkapa a'a. Bali KASI MPIA, NGUVU MPYA na ARI MPYA. Elimu yenye kuletwa Ili NCHI IJENGWE haikuwepo kwenye AGENDA zake Kikwete.

IH iiiii!
Kijana wa tatu ni MAGUFULI. Kweli KUONA ni KUAMINI. Kumbe tunaweza. Tunaweza MAKUBWA tu, haya aliyofanya Magufuli ni cha Mtoto.

*****TUNAWEEZAAAAA! Pindi tukimuweka MUNGU MBELE.Kwani Yesu/Isa, alinukuliwa kusema (kwa kumuweka Mungu mbele), huu ndio UZIMA WA MILELE, UTATU mtakatifu usiokuwa fumbo la Imani-
1) tumjue Mungu Mmoja,
2) wa kusadikishwa [wakupigiwa kura za ndio (KATIBA)] na
3) mjumbe mtumishi wa Mungu.
Yoh 17:3.
Yazingatie hayo Vumilika na wenzako-

Tumeona miundo mbinu Magufuli ameijenga kwa kasi. Kaja na HAPA KAZI tu. Akatutaka kwa kurejelea rejelea "MUNGU TUMUWEKE MBELE. Haka KAELIMU ka Mungu kuwekwa mbale, alikasemaaaa; bali hakufanikiwa kukabainisha. Kama kawaida yao, wakiona kuna mtu Afrika, ameona kamwangaza katakako wapa nao kumiliki uchumi wao kidogo tu, wanamgaddafi.

Hata hivyo basi, tumsome Magufuli rais wa tatu Tanzania (Mwinyi na Nyerere tusiwahesabu) katika dhamira ya Nyerere, nchi ijengwe kwa kuleta ELIMU.

MUNGU TUMUWEKE MBELE:

Mungu kuwekwa MBELE ni IJE Elimu ambayo kwayo WATU, UHAI wao utasalimika kwa jinsi WANAVYO ISHI. Zingatia maneno mitatu haya- Maosha. Uhai na Elimu. Yana siri gani.

Kwa hiyo MAISHA ni nini?

MAISHA ni namna ya kuishi Watu, kwa kuzijua NJIA zake. Na ili maisha hayo yawe mazuri, ni lazima jamii husika IENZI mambo MATATU-{njia za kuishi tatu}:
* UAMINIFU,
** HESHIMA na
*** UTII.
Na kwa JAMII kuelekeza nyuso kushika UTATU huu, hali hiyo (hicho kilicho shikwa) ndiyo huitwa DINI ya watu.

HISTORIA:

Kumbe Uaminifu, Heshima na Utii ndiyo dini yetu watu weusi. Wazungu walipo livamia bara letu, waliwakuta babu zetu wameyatawala MAZINGIRA vizuri , kwani walijua MAISHA ni kuwa muanifu, mwenye heshima na kuwa mtiifu. Na ni kwa kukumbatia dini yetu watu weusi (UTATU mtakatifu adilifu -uaminifu, heshima na utii), Mungu hutukamilishia Rehema zake, kwa kutuletea mawingu yanyeshayo mvua tele. Atupe MALI, WATOTO, MABUSTANI na MITO Q71:10-13

Babu zetu wakajua pia kuwa, Ili kuwa na MAISHA MAZURI {kuwezeshwa kuishika dini yetu vizuri [uaminifu, heshima na utii]} ni lazima jamii ielimishwe.

ELIMU:
Kumbe elimu ni zao LA malezi. Kwa hili kwezeshwa kuwa na MAISHA mazuri, ilibidi watu waleleke IPADAVYO. Yaani kuweka mfumo wa malezi kwa watoto ulio RASMI (jando/unyago) na usiyo RASMI (kuamrisha mema na kukataza mabaya, kuchunga miiko, kusoma kwa kuona na kusikia n.k). Naam, kwa namba hii, jamii ikavuna walichokipanda; kwa Mungu kuwaletea mawongu yanyeshayo mvua tele. Akawapa Mali, Watoto, Mabustani na Moyo.

MALEZI RASMI:

Kamwe hawakuchanganyika wanaume na wanawake. La! Na Marika pia yalizingatiwa. Kijana aliona fahari kufuzu kwa kila hatua ya UKUZI wake. Nayo jamii ikampa heshima na thamani kwa utiifu, heshima na uaminifu wake kuwa ndio kielelezo cha kufuzu kwake.

Ima UHODARI, WELEDI, HESHIMA, SIBRA, IMANI, IADILIFU, UCHANGAMFU, UPOLE, HURUMA ADABU n.k, ikawa ni sifa zenye kumpa mtu HAKI kwenye jamii na mazingira yaliyo mzunguka.

Yote hayo ni MATUNDA ya Malezi, uthibitisho wa kijana KUELIMIKA.

Tujiulize ELIMU ni nini?

Elimu ni ZAO LA MALEZI. MAZAO hayo, Mtu ameyafikia kwa kuyaumia magego Mambo matatu (UTATU MTAKATIFU ASILI [wakijadi]), ambao ni mihimili ya TAIFA Mitatu-
1) MILA,
2) DESTURI na
3) JADI.
kuwa ndio liokuwa mfumo wao wa uongozi na utawala zama za kabla wageni wavamizi kuipora ardhi yetu.

....itaendelezwa
 
Mheshimiwa rais kwa upole nikuambie nchi imekushinda


Tanzania imekushinda, vitu vinapanda bei kwa amri yako

Tozo ni baraka zako

Vyakula vimepanda bei


Bado maluku naskia unapandisha

Hapo bado gasi zinapanda bei


Yaani mheshimiwa sikutarajia ungebadilika hivi....mheshimiwa utafanya watu wammis mwendazake wallah


Mama kiukweli umechemsha nchi imekushinda watanzania tumeshakuchoka


Samia must go.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…