Tatizo sisi ni selfish, tunatumia mihemko na hisia katika kutatua matatizo, mpeni muda mama, mbona ni mapema mno mmeshaanza kulalama!
DUNIA:
Vumilika, Mapito Mwanza, nawe Kijana wa Jana, mimi ni Mzee wa juziii! Lakini hebu tushee fikra mujarabu pamoja.
Dunia ina UMBILE. Nalo lina TABIA.
Tabia ya UMBILE la Dunia, lina thubutu kwa Mwanadamu ili kuweza kufaulu, ni kwa kuyashika kwa kujua mambo MATATU- MAISHA, UHAI NA ELIMU.
Ni Wakoloni watawala wakijificha nyuma ya wakoloni Wamisionari, Utatu kama huo-
1) Maisha,
2) Uhai na
3) Elimu;
waliuita UTATU MTAKATIFU, fumbo la Imani. Lakini kwa upembuzi wetu, tatu tatu ziko nyingi. Kwa lugha ya Maandiko Matakatifu, UTATU MTAKATIFU, ndicho KITU kilicho MAARUFU. Bali Tatu Tatu hizo, tutazikabili kila moja muda wake ukifika.
UTATU, TABIA YA UMBILE LA DUNIA:
Katika Mwadamu kuwa sehemu ya Dunia, yaani MTU na MAZINGIRA; utawala (serikali) ijitambue kwamba, mafanikio ya watu wake, yako kwenye MTIHANI (KUTAHINIWA). Ili binadamu kuweza kuishi (MAISHA ni nini?), lengo ni aweze kudumu kuwa hai (UHAI ni nini?). Na hayo, yanahitaji elimu (ELIMU ni nini?). Kwa hiyo, serikali isipo UJUA UTATU huu-
1) MAISHA,
2) UHAI na
3) ELIMU,
Vinavyo tegemeana, mahusiano yake, ukaribu wake, ukweli wake na UMUHIMU wake; itawaingiza RAIA wake kwenye mifumo ya maisha ya kufikirika, kwa gharama kubwa na hasara isiyo pimika. Kwani kama Vumilia alivyo pima, UBINAFSI ndio tulio ukumbatia.
Nitapata nini kwa ajili yangu na familia. Ni MIHEMKO tu.
Wazungu wametulia, wanatuchunga tusitoke hapo. Ni malumbano, ni kebehi, ni dharau, ni ghadhabu; vyote vinapinga upole, busara na hekima, ndicho wazungu wakoloni wanavyo tuelekeza tuvidumishe kwa istilahi ya DEMOKRASIA.
Ndio maana, Mzee Nyerere alikuwa bayana, VIJANA tutafute ELIMU kwanza, ILI KUWEZA KUJENGA NCHI. Kwa hiyo akaja na UHURU na KAZI. UJAMAA NI IMANI n.k.
Mwinyi akaendeleza uhuru na kazi, ujamaa ni imani; akiamini iko siku vijana watakuja na ELIMU, tujenge nchi.
Kijana wa kwanza kuja, akawa ni MKAPA. Akaja na UKWELI na UWAZI na kuishia mtaji wa masikini ni NGUVU zake. Ile ELIMU hakuja nayo.
O'o ooo!
Kijana wa pili KIKWETE, yupo. Akaja na yake. Yale ya Nyerere na Mkapa a'a. Bali KASI MPIA, NGUVU MPYA na ARI MPYA. Elimu yenye kuletwa Ili NCHI IJENGWE haikuwepo kwenye AGENDA zake Kikwete.
IH iiiii!
Kijana wa tatu ni MAGUFULI. Kweli KUONA ni KUAMINI. Kumbe tunaweza. Tunaweza MAKUBWA tu, haya aliyofanya Magufuli ni cha Mtoto.
*****TUNAWEEZAAAAA! Pindi tukimuweka MUNGU MBELE.Kwani Yesu/Isa, alinukuliwa kusema (kwa kumuweka Mungu mbele), huu ndio UZIMA WA MILELE, UTATU mtakatifu usiokuwa fumbo la Imani-
1) tumjue Mungu Mmoja,
2) wa kusadikishwa [wakupigiwa kura za ndio (KATIBA)] na
3) mjumbe mtumishi wa Mungu.
Yoh 17:3.
Yazingatie hayo Vumilika na wenzako-
Tumeona miundo mbinu Magufuli ameijenga kwa kasi. Kaja na HAPA KAZI tu. Akatutaka kwa kurejelea rejelea "MUNGU TUMUWEKE MBELE. Haka KAELIMU ka Mungu kuwekwa mbale, alikasemaaaa; bali hakufanikiwa kukabainisha. Kama kawaida yao, wakiona kuna mtu Afrika, ameona kamwangaza katakako wapa nao kumiliki uchumi wao kidogo tu, wanamgaddafi.
Hata hivyo basi, tumsome Magufuli rais wa tatu Tanzania (Mwinyi na Nyerere tusiwahesabu) katika dhamira ya Nyerere, nchi ijengwe kwa kuleta ELIMU.
MUNGU TUMUWEKE MBELE:
Mungu kuwekwa MBELE ni IJE Elimu ambayo kwayo WATU, UHAI wao utasalimika kwa jinsi WANAVYO ISHI. Zingatia maneno mitatu haya- Maosha. Uhai na Elimu. Yana siri gani.
Kwa hiyo MAISHA ni nini?
MAISHA ni namna ya kuishi Watu, kwa kuzijua NJIA zake. Na ili maisha hayo yawe mazuri, ni lazima jamii husika IENZI mambo MATATU-{njia za kuishi tatu}:
* UAMINIFU,
** HESHIMA na
*** UTII.
Na kwa JAMII kuelekeza nyuso kushika UTATU huu, hali hiyo (hicho kilicho shikwa) ndiyo huitwa DINI ya watu.
HISTORIA:
Kumbe Uaminifu, Heshima na Utii ndiyo dini yetu watu weusi. Wazungu walipo livamia bara letu, waliwakuta babu zetu wameyatawala MAZINGIRA vizuri , kwani walijua MAISHA ni kuwa muanifu, mwenye heshima na kuwa mtiifu. Na ni kwa kukumbatia dini yetu watu weusi (UTATU mtakatifu adilifu -uaminifu, heshima na utii), Mungu hutukamilishia Rehema zake, kwa kutuletea mawingu yanyeshayo mvua tele. Atupe MALI, WATOTO, MABUSTANI na MITO Q71:10-13
Babu zetu wakajua pia kuwa, Ili kuwa na MAISHA MAZURI {kuwezeshwa kuishika dini yetu vizuri [uaminifu, heshima na utii]} ni lazima jamii ielimishwe.
ELIMU:
Kumbe elimu ni zao LA malezi. Kwa hili kwezeshwa kuwa na MAISHA mazuri, ilibidi watu waleleke IPADAVYO. Yaani kuweka mfumo wa malezi kwa watoto ulio RASMI (jando/unyago) na usiyo RASMI (kuamrisha mema na kukataza mabaya, kuchunga miiko, kusoma kwa kuona na kusikia n.k). Naam, kwa namba hii, jamii ikavuna walichokipanda; kwa Mungu kuwaletea mawongu yanyeshayo mvua tele. Akawapa Mali, Watoto, Mabustani na Moyo.
MALEZI RASMI:
Kamwe hawakuchanganyika wanaume na wanawake. La! Na Marika pia yalizingatiwa. Kijana aliona fahari kufuzu kwa kila hatua ya UKUZI wake. Nayo jamii ikampa heshima na thamani kwa utiifu, heshima na uaminifu wake kuwa ndio kielelezo cha kufuzu kwake.
Ima UHODARI, WELEDI, HESHIMA, SIBRA, IMANI, IADILIFU, UCHANGAMFU, UPOLE, HURUMA ADABU n.k, ikawa ni sifa zenye kumpa mtu HAKI kwenye jamii na mazingira yaliyo mzunguka.
Yote hayo ni MATUNDA ya Malezi, uthibitisho wa kijana KUELIMIKA.
Tujiulize ELIMU ni nini?
Elimu ni ZAO LA MALEZI. MAZAO hayo, Mtu ameyafikia kwa kuyaumia magego Mambo matatu (UTATU MTAKATIFU ASILI [wakijadi]), ambao ni mihimili ya TAIFA Mitatu-
1) MILA,
2) DESTURI na
3) JADI.
kuwa ndio liokuwa mfumo wao wa uongozi na utawala zama za kabla wageni wavamizi kuipora ardhi yetu.
....itaendelezwa