Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Ndo mkome kupapatikia watu haraka haraka!

Tuliwaambia adui yenu ni CCM. Siyo Magufuli.

Lakini hamkusikia.
ADUI?

Adui sio Magufuli, wala sio Samia na wala sio CCM; bali ADUI ni sisi wenyewe, tumekuwa wavivu wa KUFIKIRI.

TAFAKURI:

Neno hili TAFAKARI ndani ya Qur'ani, limetumika Mara 37.

"Je! Hamfikiri"?

Leo tuna miaka 60, baada ya uhuru wa BENDERA. Muda kama huu ni mrefu sana. Mbona hatujiulizi shida iko wapi?

SHIDA NI WANASIASA!!!!

WANASIASA kivipi?

Ilikuwa ni ada ukitoka form two kwenda form three, tunachaguliwa MASOMO. Wale wenye akili ya darasani hupangwa msomo ya sayansi. Na wale feliyaz (wenye kupata alama za sifuri masomoni), hupangwa masomo ya arts. {Nakumbuka mwenzetu mmoja tulisoma naye. Alipata F Tisa mtihani ule wa Kembriji miaka ile. Lakini wakati wa serikali ya Mkapa, alikuwa namba tatu kwenye usalama wa taifa}.

Weee bwana! Kumbe hii ni janja ya mkoloni. Kwani mkimaliza shule na kutoka vyuoni, wale feliaz, ndio huwa WANASIASA viongozi wa nchi, mikoa, wilaya n.k. Wao ndio wakuu wa majeshi, wakurugenzi, Mameneja kwenye maofisi hata benk na ndio Waalimu mashuleni. Wao ndio wapanga sera n.k. Wakienda ulaya hutandikiwa red kapet. Wao ni kuanguka saini bila hata kusoma kilichoandikwa, eeee. Huku anapigwa mabega wakimdhihaki -una akili!

Wale waliokuwa wana uwezo mkubwa wa KUFIKIRI darasani, wanaishia kuongozwa na hawa mbumbu Muzungu wa reli. Hawana lao, ila kufuata ukoloni mambo Leo. Ndio mainjinia, madoktari, waalimu, wahasibu n.k.

TAFAKURI:

Sasa tufanyeje? Kwani mbinu hii ya wakoloni ikikiukwa na akaingia MWEREVU IKULU, wanamuua directly au indirectily, bila hofu wala kizuizi chochote.

MUNGU TUMEMWACHA, NAYE AMETUACHILIA:

Wameweza hayo kwa kututenga mbali na Mungu wetu watu WEUSI. Kwa hiyo tukaibwaga dini yetu (UNYENYEKEVU), na kushikishwa dhehebu, taasisi na au shirika. ELIMU ikafichikana. Tumo kwenyeMKOROGO. Tumekorogwa ajabu Q50:5 . Humo, tukaingizwa kwenye uadui na faraka baina yetu. Na ndipo wakatutwanga rungu kuubwa kwa kuwakabidhi FELIAZ wetu vyama pinzani. Leo wengine wako ulaya, wanabwata ya kuwafurahisha wakoloni, hata kama anayosema ni kweli. Wazungu Hawahitaji kupambana nasi tena bali sisi wenyewe kwa wenyewe. Wao wazungu walicholenga ni KUTUFISIDI.

UFISADI:

Wameturithisha serikali iliyoundwa kuenzi wizara Mji mkuu 23. Wizara hizi, zikarudiwa kama idara mikoani na wilayani. Kwa hiyo bajeti humwagwa wizani mji mkuu kwa mabilioni. Pesa hizi kupitia idara ya MANUNUZI huishia ulaya for shopping. Manunuzi ya vifaa vya maofisini, magari n.k. Miaka sitini Leo pesa ambayo angepewa MJASIRIA MALI MMOJA, angefanya maajabu. Mwone Bahkhresa. Leo tungekuwa na Mabakhresa wangapi?

Lakini pesa ya nchi hutokomea Mji mkuu wizarani kwa mabook kipaz (makatibu wakuu), mikoani na walayani kwa wakurugenzi. Na yote inaishia shopping EEU, USA NA BRICS.
Tell me HUU SI NDIO UFISADI? Yuda 1:4

Wao WANASIASA wetu, wanaamini kuwa, manunuzi hayo wanayofanya ni ili WAJENGE NCHI Q2:11-12 kumbe wanaharibu.

ADUI YETU NI NANI?

ADUI yetu ni wewe na mimi tusio TAFAKARI juu ya mustakabali wa UMMA wetu. Na tumewaachia kikundi kidogo kilichopitia shule zilizo tayarishwa na wazungu kwa malengo yao wazungu na FAIDA kwao. Mitaala wakaisementi, Leo miaka 60 baada ya uhuru, vyuo vyetu vinazalisha wasaka AJIRA. UZALISHAJI MALI wameachiwa MAMANTILIE. Huu ni ufukara wa AKILI.

Oh!?!?!?
 
Wadau tulio wengi wakati nchi inapata kiongozi mbadala wa Hayati Magufuli kauli mbinu ilikuwa "kazi inaendelea" binafsi niliamini kazi inaendelea kwenye miradi yote aliyoiacha Hayati Magufuli kumbe ni yale yote aliyokuwa anayafanya Magufuli likiwemo la kupambana na wpinzani kwa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama.
  • Watanzania tumejionea kuendelea kupiga marufuku mikutano ya siasa lakini CCM wanafanya
  • Watanzania tumeendelea kuona kukataliwa kwa makongamano ya Katiba Mpya kwa kisingizio cha tunajenga uchumi usiojengeka toka enzi ya Magufuli
  • Watanzania tumeshuhudia kamata kamata ya polisi dhidi ya wapinzani toka enzi ya Magufuli
  • Watanzania tunashuhudia kubambikiana kesi kwa wapinzani safari hii Mh Mbowe kapewa ugaidi n.k
Kumbe falsafa ya kazi inaendelea ni kuendeleza yote aliyoyaasisi Magufuli

Tumwombe mungu ampe hekima upendo na busara Rais Samia ayaepuke ya mtangulizi wake
 
Siyo anapoteza , kishapoteza tayari
Wala!

Samia wa watu hajapotea, bali waafrika tulishapotezwa na wazungu tangu kupata uhuru wa bendera.

Hapo Samia Rais alipo, ni AJIRA. Yeye ni mwajiriwa namba moja.

Jiulize kaajiriwa na nani?

Ona! Waingeteza serikali yao ni Maanglikan. Wajerumani ni Waluteti. Waitaliano ni Makatoliki. Serikali hiyo, mbona wao wana dini?

Wahindi ni Mahindu. Wajapani ni Mashonzi, Waturuki ni Masuni. Wairani Mashia, Wamarikani ni Walokole n.k.

Njoo kwetu, sisi serikali zetu hazina Dini ila RAIA wake. Nao raia, dini hawana ila wameshikishwa mashirika ya udini, taasisi na dhehebu.

SERIKALI zetu kutokuwa na dini si kweli. Tuna dini ya UKAFIRI. Ukana Kristo ~Yuda 1:4. Huko ndiko KUPOTEA. Samia anasimamia huo UPOTOFU kulingana na katiba ya nchi iliyoidhinishwa na waziri wa mambo ya ndani wa uingereza mwaka 1959 huko London.

Na mimi na wewe, tukiikwaa nafsi ya Urais, tutakuwa si ajabu wahoviyo kweli kweli.

Dini yetu WAAFRIKA:

Waafrika kabla ya wazungu tulitawaliwa juu ya Misingi mitatu (mihimili ya uko au taifa)-
1) MILA,
2) DESTURI na
3) JADI,
UTATU MTAKATIFU ASILI, USIO KUWA FUMBO LA IMANI.
Kwa kushika mihimili hii neema ya Mungu -
1) ARDHI,
2) HEWA na
3) MAJI (MVUA)
ikatudirikia. Mazingira yakanona na kupendeza pindi Wafalme wetu walipoisimamia dini yetu kikamilifi-
1) UAMINIFU,
2) HESHIMA na
3) UTII,
Kwenye misingi yake 10-
1) Mungu ndiye kila kitu,
2) Mbora wa sifa kwa majina ni Mungu peke yake,
3) Mila ya baba wa imani kuenziwa,
4) Miiko kuchungwa,
5) Kuwaheshimu baba ba mama,
6) Wizi hapana,
7) Kusema uongo hapana
8) Kuua hapana,
9) Kuzini ilikuwa ni mwiko na
10) Chako ni cha jirani na cha jirani ni chako.
Huu ni UPENDO, dini Yetu watu Weusi.

Mwaka 1960 kurudi nyuma, hii ndiyo iliyokuwa dini yetu watu weusi. Kwenye biblia na Qur'ani imeitwa AMRI 10 ZA MUNGU.

Viongozi wa kaya uko na kabila , walienzi Amri hizi kupitia malezi ya JANDO na UNYAGO. Ni malezi ya shule ndiyo yalikuja kuficha na kuiondoa dini hii, licha kwamba Jumba LA waziri mkuu wa uingereza hadi Leo LINAITWA 10 DOWN STREET (yaani AMRI 10 ZA MUNGU CHINI MITAANI. NA langoni NAMBA 10 IMEANDIKWA). GOGO UJIONEE MWENYEWE.

Kama Samia Rais atagundua hili (na ni vigumu kwani amezungukwa na wenye digrii, washauri walioleweshwa ukasumba), ang'amue kuwa anawajibika kwa watu na sio serikali kuu (mradi wa wazungu) Afumue mifumo batili na kuanza upya kutafuta njia yetu, na IPO wazi ikiwa MUNGU TUTAMUWEKA MBELE.
 
Chanjo hawaitaki karibia 75% ya watanzania

Tozo mpesa zinaanza kafungwa.

Bei ya mafuta kuna fukuto la kupandishwa nauli au migomo ya daladala.

Miundombinu ya serikali inaungua tu na masoko, Shule sasa miundombinu ya umeme.

Bei ya Mbolea imeanza kuwavuruga wakulima maana msimu wa kilimo unakaribia na serikali imeongeza kodi.

Kafungwa kwa Mbowe na Sabaya kumeigawa nchi.

Rais anawashangaza watu kuzunguka tu nje ya nchi kama Tiara yaani full kupishana angani.

Wezi wameshika mpini tena

Wananchi wanawashangaa watu walioikataa chanjo kuishupalia.

Hakika kitaa kumechafuka aliyekaribu na mama amwambie.

Kipindi kile tulimtuma Rizi leo tutamtuma nani? Anayemjua mtoto wa mama amfikishie ujumbe huu.
 
Ujumbe tumeusikia.....
Shaka ondoa
 
Yupo mtoto wa kambo.
Mwambie Ridhwan[emoji445],,mshtue Ridhwan[emoji444].
sema na Ridhwan[emoji445]aongee na mshua[emoji444]
Hii ngoma kwanini aipigwi?
 
Yupo mtoto wa kambo.
Mwambie Ridhwan[emoji445],,mshtue Ridhwan[emoji444].
sema na Ridhwan[emoji445]aongee na mshua[emoji444]
Hii ngoma kwanini aipigwi?
Duh enzi zile Ridhiwani alifikisha ujumbe faster sana kwa mshua

Mather tatizo naye atulii watoto watamuona sangapi?

Leo huyo Rwanda
 
Huyu Mama hakuwahi kufaa kua Rais aa JMT.


Kwa wajanja wanaomzunguka, saizi ni kumshauri tu Mama Safiri...eehh sindo Rais wa Nchi banaa... Anajenga mahusiano.... Sijui Mulamula kazi yake nn

Huku wanabaki wanapigaaa.


Mimi Jiwe, nilimpinga kwenye Masuala ya haki za binadam, siasa .


Huyu Mama yenu, Tunapigwa kote kote, yaan Siasani tunapigwa, Serikani tunapigwa, wanyonge tunapigwa
 
Inafikirisha

Lakini nadhani watu wameutumia uhuru alioutoa mama vibaya

Magufuli knew this and ruled with an iron fist

mengi uliyoongea ni muhimu but I think you are judging too fast
 
Ghafla bin vuu mambo yakabadilika. Akasema hataki kodi za Dhulma.akaja na kodi za wizi, akasema atakaa na wapinzani kuweka mambo sawa ghafla kutwa nzima anawawinda kwa mitutu na Marungu.

Akasema unyanyasaji kwake mwiko mbona sheria mbovu hataki zirekebishwe??

Nani alimwambia Rais Samia kuwa kunyanyasa watu kutampa mafanikio?

Nani alimwambia Rais Samia kuminya uhuru wa maoni na kuweka misingi ya demokrasia uwazi na uwajibikaji kuaa atatoboa?

Nani anamdanganya?

Nani anamtumwa kwamba akidhibiti watu kwa mkono wa chuma nchi itasonga mbele?

Je Magufuli mtangulizi wake aliyetawala nchi kama yake alifanikiwa?

Uganda na Rwanda wamefanikiwa? vipi Somalia na Sudani wamefanikiwa?

Kenya je?

Mama unajidanganya. Fanya wajibu wako. Hao unaotaka kuwafurahisha watakufurahisha siku moja hutaaamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…