Rais Samia Suluhu alianza vizuri katika siku zake 100. Baada ya kuanza kukandamiza haki za binadamu, kukubali kudanganywa na wakina Siro kuhusu kesi ya ugaidi wa Mbowe, kuanza kusema uongo, kuanza kuvimba kichwa, hapo ndipo alipoanza kujiharibia sifa zake kama kiongozi wa nchi.
Kwa lililotokea Marekani ile zomea zomea ni haibu kubwa mno. Tena kubwa mnooooo hasa kwa kiongozi kama yeye, mwenye miezi 6 tu na Mwanamke. Yale mabango yalibandikwa pale mlangoni. Kila aliyekuwa anaingia lazima akutane nayo. Yeye mwenyewe alikutana nayo na kuyasoma. Ebu imagine dunia nzima inapita wanakusoma kwa mambo ya ajabu, unajisikiaje? . aisee ni fedheha na haibu kubwa mno kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo.
Kwa hakika I feel bad kuongozwa na Rais huyu. Mimi ni CCM damdam na kiongozi mwandamizi ila haya yanayoendelea yanasikitisha.
One, thing i can assure You. Kwa ile aibu ya juzi. Rais huyu atabadilika sana sana. kaona namna unaweza kuaibishwa na kudhalilishwa kule nje. Taking a note kuwa Wanawake wote duniani hakuna kitu wanakiogopa na kujishtukia kama kupata aibu au kudhalilishwa...
Rais wetu. Mwenyekiti wetu. Badilika. Kwa hakika suala la Mbowe hata sisi hatulikubali. Linachafua nchi. na kubwa zaidi linaweka wazi uozo wa polisi wetu.... Kwa ule ushahidi wa jana wa Adamoo, kama kweli wasaidizi wako watakuwa wanakupenda Jumatatu kabla mtuhumiwa wa pili kuanza kutoa ushahidi DPP afute kesi hiyo. Inatudhalilisha sana sana, sijui kama unajua.
anyway, niseme tu tayari tumemtengeneza Mgombea wa upinzani wenyewe na kumpa nguvu wenyewe. Mbowe is new Hichilema. 2025 ndio candidate wa upinzani. Tumempa umaarufu huo na fursa hiyo wenyewe.... Ni sober, cool, composed, organized than Lisu...
Kama Rais unajua kabisa bado kuna vuguvugu la watu wa awamu ya 5 hawajakukubali. Bado unajua kuna suala la Kanda ya ziwa yote hukubaliki. Bado unajua Kanda ya Kaskazini hukubaliki. Bado unajua majiji kama Dar, Mbeya hukubaliki. Usingewasikiliza washauri wanaotaka kukupoteza. Hawakusaidii bali wanakupoteza. Wameanza tena kuwapiga Machinga. Leo hii Machinga, Mama Ntilie, Boda boda wanamlilia na kumkumbuka Magufuli mithili ya mbegu ilioshamiri. Nikwambia tu altenative ya magufuli wenyewe kwa uwepesi wataona na Mbowe. Kwa sababu tumeamua kumkuza na kumpa nguvu kwa issue ya kitoto za polisi... 2025 sio mbali. CCM tunakiri tutakuwa na uchaguzi ulio mgumu kuwahi kutokea katika nchi hii. Kama utagombea wewe!... ili uwe rahisi basi badili gia angani. Usiwasikilize hao washauri wako. tumia akili yako zaidi kama Magufuli alivyokuwa anafanya.