Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Utotoni kwetu, tafauti zetu nyingi tukizimaliza kwa mapigano. Lakini kupigana kwetu hakukumaanisha kuwa sisi si marafiki tena. Wakati mwengine waliopigana mchana, jioni wanatafautiana wakacheze mpira na keshokutwa wanachangiana kumpiga mwengine. Staili za kupigana zilikuwa mbili maarufu: moja ya kurusha mateke, magumi na vichwa (nadhani ndiyo leo iitwayo kick boxing).

Nyengine ni ya kutia kabari na kunamia (labda inafanana na ngware na mieleka). Hii, mimi ndiyo niliyokuwa nikiitegemea sana. Kwenye kunamia, huwa najielekeza kwenye mbavu za mtu, kumzonga mpinzani wangu kwa mikono na kumbiruwa kichalichali, kisha naanza kumshindilia magumi shibaye. Kwenye kabari, badala ya kupigana uso kwa uso na mpinzani wako, wewe unamgeukia nyuma yake na kumkaba shingo hadi uone pumzi zinampaa.

Raha ya hizi mbinu ni UDHIBITI. Yaani adui sio tu kwamba unampiga, kisha unamuacha akusanye nguvu, bali unamdhibiti kabisa. Kila akikukumbuka, akilini mwake inamjia jinsi pumzi zinavyomkukurika. Nimegunduwa Mama Samia anatumia mbinu ya KABARI na KUNAMIA kwenye mapambano.

Credit: Mohammed Al Ghassan wa DW
 
Bi Mikopo hata hajui maadui zake ni akina nani hasa! She is about to be fully & permanently surprised and flabbergasted!
 
Kazi zake zinajipambanua,kingine uimara na kujiamini. Walimu-under estimate.
 
Kitendo cha jana kutamka wazi wazi kuwa mawaziri wajipimie wasizidishe sana, kimenikatisha tamaa kabisa hii ni dharau kubwa kwa watanzania tumedharauliwa sana hadharani,

na hii ni kuonekana kwamba sisi sio lolote wala chochote kwake
siwezi kuwa mfuasi wa siasa za namna hii za maji taka, nilimtetea sana lakini kwa sasa hapana aisee

siwezi

IMG_20220113_093129.jpg
 
Nyie wenye imani na CCM ni laana kwa nchi yetu na mnatuponza kwa mengi.

Wamefanya maovu na madudu mengi ila bado tu mnawang'ang'ania.

Mnakera sana watanzania wa aina hii.
 
Kitendo cha jana kutamka wazi wazi kuwa mawaziri wajipimie wasizidishe sana, kimenikatisha tamaa kabisa hii ni dharau kubwa kwa watanzania tumedharauliwa sana hadharani,

na hii ni kuonekana kwamba sisi sio lolote wala chochote kwake
siwezi kuwa mfuasi wa siasa za namna hii za maji taka, nilimtetea sana lakini kwa sasa hapana aisee

siwezi

View attachment 2080308
Ni kauli ya ajabu sana,kutolea na kiongozi wa nchi,laiti ingekuwa nchi za Watu wanao tafakari vizuri,Leo tulipaswa kuwa barabarani,tulipa Kodi na matozo makubwa,alafu watu wanaambia waibe taratibu?
 
Ni kauli ya ajabu sana,kutolea na kiongozi wa nchi,laiti ingekuwa nchi za Watu wanao tafakari vizuri,Leo tulipaswa kuwa barabarani,tulipa Kodi na matozo makubwa,alafu watu wanaambia waibe taratibu?
Hapa mama kateleza ila bado hao hao mawaziri wanazidi kumpigia makofi.

Kwa hili naamini hawa viongozi wanapigania kuingia madarakani kwa ajili ya manufaa yao
 
Huyo ndiye Rais wa nchi hiyo cheap popularity inaingiaje?

Mkitaka msitake yeye ndiyo kiongozi mkuu wa nchi na ndiye aliyeachiwa hatamu ya uongozi, mbona aliyepita kuna miradi aliiwacha hivyo hivyo?

Tuwe na subira, kwani yeye hajatoka upinzani ni kiongozi wa CCM ileile na ilani ileile kinachotofautiana ni utendaji tu. Ukizingua unazinguliwa.
sasa kama rais hajatoka upinza na ccm ni ile ile kuna sababu gani ya kutofuata ilan ya chama? miradi iliyoanzishwa inatakiwa ifanyiwe utekelezaji sasa iweje yeye achane na hii miradi aibue miradi yake mingine? shame on her!
 
^POSSESSION OF POWER THAT WAS NOT ACQUIRED THROUGH SELF-EFFORT^

^Power in the hands of one who did not acquire it gradually, is often fatal^
 
Hapa mama kateleza ila bado hao hao mawaziri wanazidi kumpigia makofi.

Kwa hili naamini hawa viongozi wanapigania kuingia madarakani kwa ajili ya manufaa yao
CCM ni janga la Taifa, na hatutapata maendeleo ya kweli kamwe chini ya CCM, wamejipambanua kwamba wao ni wezi, sasa wanashauriana kuiba kidogokidogo, Twafaaa
 
Back
Top Bottom