aleesha
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 798
- 1,178
Utotoni kwetu, tafauti zetu nyingi tukizimaliza kwa mapigano. Lakini kupigana kwetu hakukumaanisha kuwa sisi si marafiki tena. Wakati mwengine waliopigana mchana, jioni wanatafautiana wakacheze mpira na keshokutwa wanachangiana kumpiga mwengine. Staili za kupigana zilikuwa mbili maarufu: moja ya kurusha mateke, magumi na vichwa (nadhani ndiyo leo iitwayo kick boxing).
Nyengine ni ya kutia kabari na kunamia (labda inafanana na ngware na mieleka). Hii, mimi ndiyo niliyokuwa nikiitegemea sana. Kwenye kunamia, huwa najielekeza kwenye mbavu za mtu, kumzonga mpinzani wangu kwa mikono na kumbiruwa kichalichali, kisha naanza kumshindilia magumi shibaye. Kwenye kabari, badala ya kupigana uso kwa uso na mpinzani wako, wewe unamgeukia nyuma yake na kumkaba shingo hadi uone pumzi zinampaa.
Raha ya hizi mbinu ni UDHIBITI. Yaani adui sio tu kwamba unampiga, kisha unamuacha akusanye nguvu, bali unamdhibiti kabisa. Kila akikukumbuka, akilini mwake inamjia jinsi pumzi zinavyomkukurika. Nimegunduwa Mama Samia anatumia mbinu ya KABARI na KUNAMIA kwenye mapambano.
Credit: Mohammed Al Ghassan wa DW