Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Unawatoa Prof Kabudi, Kalemani na Mh Lukuvi, unaweka Nape, Makamba na Ridhiwani Kikwete.

Unafanya re-shuffle kuwatengenezea nafasi familia chache, halafu unashangaa kwanini hupendwi.

Unawarudisha watu waliofukuzwa kwa kutokuwa na Vyeti. Ungeweza ungetaka kuajiri vijana wenye vigezo.

Mikopo ya ajabu kujenga vyoo, kupambana na Covid.

Umeme,maji, bidhaa, mafuta, vifaa vya ujenzi. Kila kitu umeshindwa kukisimamia. Mipasho mingi, vitendo zero.

Vitu vya msingi unashindwa kuvisimamia, kuvijali.
 
Tuonesheni Tanzania ya viwanda ile kwenye ilani ya 2015.
Hawa Viongozi wote Wana Vinasaba vinavyofanana wanatamani kutuvusha kutoka hapa tulipo lakini mbinu za kututoa hapa hawana kwahyo wanachofanya ni business as usual wachache wale wengi wabaki kuwa watazamaji,Mfumo wao ni Kama umeshapitwa na wakati.
 
Si nasikia kuna TIMU CHATO ambayo inamikakati ya kukwamisha mama na kumkosoa kwa kila afanyacho eti kisa kaanza kueleza ukweli wa yale yaliyo kuwa yanatendeka sirini, naona mmeanza kazi sasa.
Hakuna mkakati wowote waku Mkwamisha isipokua hali ya Umaskini na Mfumuko wa Bei ndiyo utakao Mkwamisha,Adui yake wasasa ni yeye Mwenyewe kuongeza gharama za Matumizi kwenye Serikali bila kuongeza Mapato na kuongeza Deni la Taifa kwa kukopa kila uchao.
 
Kama anataka Kodi na sio Dhuluma izi Tozo za kwenye Simu sio Dhuluma,je? hii Kodi ya ardhi aliyoiweka kwenye LUKU sio Dhuluma yaani Mpangaji alipe Kodi ya Ardhi ambayo sio yake na bado useme sio Dhuluma. ameondoa Baadhi ya Tozo kwenye petrol na Diesel vp Bei ya Mafuta imeshuka? Ugonjwa unawasumbua Watanzania ni Usahaulifu tu.
 
Hawa Viongozi wote Wana Vinasaba vinavyofanana wanatamani kutuvusha kutoka hapa tulipo lakini mbinu za kututoa hapa hawana kwahyo wanachofanya ni business as usual wachache wale wengi wabaki kuwa watazamaji,Mfumo wao ni Kama umeshapitwa na wakati.
No where to hide

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Kwa kila mwenye akili timamu atakubaliana na mimi kuwa kwa sasa Rais wa Zambia Mh. Hakainde Hichilema ni Moja ya Viongozi Bora kabisa kuwahi kutokea Africa.

Anawafikia Raia wake bila kuweka ulinzi wa kukera na kutisha yeye ni kiongozi wa Kiraia, huyu hakupitishwa na polisi, jeshi wala tume ya uchaguzi ama mbeleko ya kuwa makamu wa Raisi wananchi walipanga foleni na kumpigia kura ya NDIO hivyo anatambua uchungu wa wananchi waliomchagua yeye kuwa RAISI.

Hapa kwetu Chifu Hangaya a.k.a Chui Jike kutwa kutengeza mazingira ya kukubalika kwa kujitengenezea maigizo ya kupachikwa Uchifu ambao hauna msaada wowote kwa wananchi wa hali ya chini ilihali kuna mambo ya msingi anapaswa kuyashughulikia kuepuka manung’uko kutoka kwa raia wake mambo kama mfumuko wa bidhaa mbalimbali za viwanda, umeme kukatika kila baada ya masaa fulani, kubambikia watu kesi za ugaidi na uhujumu uchumi kwa kisingizio cha kuwatisha, ni mambo ambayo yeye kama namba moja anatakiwa kuyaangaliza macho maana yanamchafulia sana.

Kwa miezi kumi ya uongozi wake tunaona akijipachika majina ya hovyo, kuvikwa ngozi za wanyama, kukusanya vibuyu na mikuki bila kusahau kujiongezea ulinzi wa jadi ili kuongeza mvuto kwa wananchi.

Tumalize kwa kusema “If you protect The People, The People will protect you , the Army , the Police will not be everywhere all the time anytime”.
 
Sawa mZee nyboma vip ile show yako ya three some uliwezaje kutekeleza ...
 
Mm naomba kuuliza tangu MAMA achkue nchi kuna mradi gani ulio kamilika asilimia100% mna kila cku 2nackia miradi na pesa anakopeshwa kma zote.
 
CCM wasipotengua utaratibu wao wa kumpitisha mgombea wao wa urais kwa awamu mbili safari hii itakula kwao.

Ili CCM iondoke madarakani kiwepesi basi wamruhusu Samia agombee urais 2025 maana Samia amefeli sehemu nyingi sana hakuna sehemu angalau unaweza ukamsifia amefanya vizuri, angalau hayati Magufuli kuna sehemu amefanya vizuri sana licha ya mapungufu machache ya kibinadamu aliyokuwa nayo.

Sasa kwa huyu Samia kila sehemu holaaa na hana meno kabisa watu wanafanya mambo ya ovyo kila kukicha kadri wanavyojisikia yeye yupo tu anaangalia.

Anachokiweza labda kuipambania Zanzibar na sio Tanzania bara.

CCM ili ilete ushindani mkubwa basi wampitishe Kasimu Majaliwa awe mgombea wa urais na sio Samia.
 
Nimeona watu wengi wanamnyooshea vidole IGP na Waziri wa Mambo ya Ndani. Mimi nina mawazo tofauti kidogo naomba nisikilizwe.

Kwa maoni yangu, Rais wetu mpendwa ameshindwa kutulinda, mauaji ya kutisha yamefululiza mno, yanayoripotiwa ni sehemu tu ya yanayotokea, pia huko barabarani ajali zinapukutisha watu kila kukicha.

Nadhani Rais ukubali tu kukaa pembeni, tunakupenda ila huwezi kutulinda.

Ni maoni yangu, naamini sijavunja sheria za JF.
 
Sasa raisi anahusikaje watu wanachomana visu kwa wivu Rais aje awapokonye?

Madereva kila siku wanapigiwa kelele lakini ni vichwa mbovu unadhani atafanyeje

Mauwaji ya kuingilia kati ni yale yanayosababishwa na polisi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…