Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anaekulazimisha afanye kama anajikuna popote alipo tumwone tafadhali🤔
 
Kwanini watulazimishe kuona mazuri yake? sisi hatumwelewi ndiyo ukweli
 
Hivi mahusiano na ujirani mwema kwa Tanzania maana yake ni kuwagawia kila kitu majirani zako na wazungu? Huku ndiyo kufungua nchi?

Kweli Uganda ni wa kuiuzia umeme Tanzania? Kweli Tanzania ni ya kwenda kuomba sukari uganda?
Kwa hiyo ajira za kwenye sukari kule kilombero na mtibwa zihamie Uganda?

Sera ya Tanzania ya viwanda ambayo ipo kwenye ilani ya ccm imeishia wapi?

Kwa press release hii watanzania na Tanzania kwa ujumla tutaendelea kudharaulika sana, tena sana. Ni mentality hii ilisababisha tukagawa kila kitu hadi Tanzanite.

Na kama maendeleo yangekuwa ni kujikomba na kujishusha hadhi namna hii basi Tanzania ingekuwa imeshapata maendeleo kitambo sana. Rais Samia asingeikuta Tanzania iko kwenye list ya nchi masikini.
 
Nchi imegawanyika sana hii na ikiendelea kama hivi itasambaratika tuu. Wengi wanataka iongozwe kidikteta, iongozwe kama China. Wengine wanataka iongozwe kidemokrasia kama nchi za magharibi. Mwisho wake tutakuwa kama ilivyokuwa Korea, upande wa kaskazini unafungamana na China, upande wa kusini unafungamana na Marekani. Nchi ikagawanyika na kuwa nchi mbili, North Korea na South Korea. Nchi haiwezi kubaki pamoja kama watu wanataka mifumo tofauti.
 
Nchi ipi iliyogawanyika hapa.
 
Unapotaka kujenga hoja usiwe na ukakasi wa hadidu za rejea......

Nakukumbusha kuwa mh.Rais Y.Museveni alipotutembelea alituomba TUNUNUE SUKARI KUTOKA UGANDA....tusisahau kuwa Kenya imepunguza kiwango cha kuingiza sukari ya Uganda(wao pia wananunua kutoka Zambia ,Sychelles na kwengineko)....Sasa ule msemo wa "if I scratch you ,scratch me back"-Bomba la mafuta kutoka HOIMA limepitishwa Tanzania badala ya njia fupi(kuelekea Mombasa).....

#Siempre JMT🙏
 
🤣🤣
 
Watanzania wanashabikia wanachopenda sio kinachofaaa.

Mama anaupiga Mwingi sana.

Watanzania wanapaswa kuongeza uzalishaji na ushindani mana nchi imefunguka. Tusiposhirikiana na wenzetu hatuwezi kuendelea.

Mwalimu alishauri kuwa Afrika mashariki ni vema wakaungana kiuchumi baina ya nchi na nchi.

Umeme kutoka Uganda ni WA Muda mrefu na ni grid kubwa ya Taifa. Ni umeme unaosababisha mji wa Bukoba kuwa na umeme wa uhakika muda wote.Mama ameomba TU uongezewe ili utosheleze na mikoa jirani . Umeme ukiwa mwingi Huko baadae utapungua Bei sana hasa bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere litakapoanza kuzalisha.

Huwezi kutegemea chanzo kimoja TU Cha umeme kwenye nchi kubwa kama Tanzania.
Umeme wa Uganda ni WA uhakika sana Kwa mkoa wa Kagera.
 
Nchi aligawa yule DIKTETA wa Chato ambaye alisema hapeleki maendeleo kwenye majimbo yanayoshikiliwa na upinzani. Na akatumia fedha zetu kujenga miundombinu mikubwa kijijini kwake Chato.
Tangu mama yako aliporudi nyumbani kwa cheti bandia akili zenu ziliyumba mpaka leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…