Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Kwa kumsaidia:
Kuna suala la panya road na matukio mengi ya mauaji ya raia, hadi leo hajasema chochote. Ni kama hakuna kiongozi wa nchi. viongozi wa mikoa na wilaya wanatamka tu wanavyoona inafaa.

Kuna suala la kupanda holela kwa gharama za bidhaa kwa kisingizio cha vita, badala ya kudhibiti yeye anasema bidhaa zitapanda zaidi.

Kuna suala la mkanganyiko wa taarifa kati ya viongozi, mfano suala la vice na naibu waziri kuhusu uhifadhi wa samaki, mama hajasema chochote!

Suala la tozo amemuachia mwigulu.
Suala la nyongeza ya mshahara 2.3% badala ya 23% akamuachia Kasimu afafanue!
Viongozi wa kisiasa wanadharau jeshi la polisi, na anaunga mkono! Yuko kimya!
Hayo na mengine mengi yanaonesha hatuna rais.
Sasa Rais amechagua wasaidizi wake ili wamsaidie, kama mambo yote tumsubiri rais afanye haina haja ya kuwa na mawaziri. Acheni basi mama achape kazi basi.
 
Sasa Rais amechagua wasaidizi wake ili wamsaidie, kama mambo yote tumsubiri rais afanye haina haja ya kuwa na mawaziri. Acheni basi mama achape kazi basi
Hii nchi ilimhitaji mtu kama jiwe japo kidoplomasia tuliyumba lakini alileta full respects watu wakachapa kazi nchi ilitulia tulii kama maji ya mtungi aisee ...RIP mwamba wa AFRIKA
 
Unaposema hafai unatakiwa useme kwanini,mtu analeta hoja za hovyo kama yupo FB.
Yani kuna watu bado hawaamini kwamba hakuna marehemu alisha wahi kufufuka kwenye zama hizi.
 
Hii nchi ilimhitaji mtu kama jiwe japo kidoplomasia tuliyumba lakini alileta full respects watu wakachapa kazi nchi ilitulia tulii kama maji ya mtungi aisee ...RIP mwamba wa AFRIKA
Kweli kabisa mkuu
 
Hii nchi ilimhitaji mtu kama jiwe japo kidoplomasia tuliyumba lakini alileta full respects watu wakachapa kazi nchi ilitulia tulii kama maji ya mtungi aisee ...RIP mwamba wa AFRIKA
Haiwezekani taifa lipige kelele then alie muumba akamwache aendelee kuwepo,si umeona nguvu ya masononeko ya watu?
 
Basi heshima kidogo Kwa rais wa inchi yako,

Uhuru wa kujieleza usizidi Kwa Aina hii ni hatari kwako na Maisha yako
 
Haiwezekani taifa lipige kelele then alie muumba akamwache aendelee kuwepo,si umeona nguvu ya masononeko ya watu?
Hata siyo mkono wa Mungu mimi naamini mwamba aliondolewa na watu wasiojulikana .........Mungu asisingiziwe kabisa , kama Thomas Sankara tuu....
 
Haiwezekani taifa lipige kelele then alie muumba akamwache aendelee kuwepo,si umeona nguvu ya masononeko ya watu?
Moja ya watu mnaopenda nchi iwe shamba la bibi. Hongera Sana mkuu. Sasa wamewaambia msijenge bomba la mafuta na mmewafuta
 
Kwa Kumbukumbu zangu wewe ni MFUASI WA KAYAFA

Hope Mabadiliko yanayokuja UMESOMBWA NA MAJI....
 
Kwa kumsaidia:
Kuna suala la panya road na matukio mengi ya mauaji ya raia, hadi leo hajasema chochote. Ni kama hakuna kiongozi wa nchi. viongozi wa mikoa na wilaya wanatamka tu wanavyoona inafaa
Yaani unataka rais aongelee panya road? Waziri Masauni anatosha. Rais anaongelea mambo makubwa mfano nchi ilivamiwa na nchi iirani kama vile Ukraine ilivyovamiwa na Urusi.
 
Back
Top Bottom