Mambo aliyoyafanya mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani Ni ngumu Sana kuyamaliza hapa, Hivyo nitajitahidi kuyaelezea kwa kadri nitakavyoweza,
Wakulima. Hapa mh Rais wetu mpendwa amewagusa wakulima ambalo Ni kundi kubwa Sana, Hapa mh Rais wetu ametoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini na kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni, mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa laki na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa elfu 70, Hali hii imewagusa Sana wakulima na kukonga nyoyo zetu wakulima Hadi tunatamani uchaguzi uwe Leo ili Tumlipe kwa kumpigia kura za kutosha Kama asanteeeeeee,
Pili mh Rais wetu mpendwa mama Samia amewagusa Sana watanzania hasa wanaotoka familia masikini na familia nyonge kwa uamuzi wake wa kutoa Elimu bure Hadi kidato Cha sita na gharama zake kubebwa na serikali yetu sikivu, hapa kiukweli Rais wetu amezigusa nyoyo za watanzania wanyonge, Jambo hili limetoa nuru na mwanga kwa watanzania wanyonge
Katika Afya. mh Rais wetu mpendwa kipenzi Cha watanzania Amechukua hatua za kujenga vituo vya Afya kila Kona ya nchi hii, mfano majuzi tu hapa vituo vya Afya takribani 234 vimejengwa hapa nchini, hii imegusa maisha ya watanzania wanyonge kwani hii imerahisisha upatikanaji wa huduma karibu na mwananchi na kupunguza safari za kutembea umbali mrefu kutafuta na kupata huduma, Jambo hili limegusa Sana mioyo ya watanzania wanaoendelea kumshukuru mh Rais na Kuendelea kumwombea Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia watanzania
Nitaendelea
Acheni uongo...nina ndugu yangu ni mmoja wa aliyepata ajira ya afya serekalini kipindi cha mzee. Magu kupitia mkono wa taasisi ya benjamini mkapa foundation 2018.
Mpaka rais magu anafariki katika kipindi cha 2015-2020 alikuwa amekamilisha ujenzi wa vituo vya afya.498. Na vingine vikiwa bado vinaendelea kujengwa...na hivyo ndo vimekamilika kipindi hiki cha rais samia, ivyo huo sio mradi wake bali ni mpango wa utekelezaji wa awamu ya tano na sio sita(ya samia).
Ona hapo ni 2018...utekelezaji wa hiyo miradi ya Vituo vya afya, zahanati, hospitali za rufaa wilaya na mikoa. Sikumbuki idadi kamili zilikuwa ngapi(zahanati, hospitali za rufaa wilaya na mikoa). Ila ulikuwa ni mradi wa Rais.Magu na sio Samia.
Toggle navigation
JAFO: Ukamilishaji wa Ujenzi wa vituo vya afya 210 nchini ni wa kihistoria.
Posted On: November 9th, 2018
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa tayari serikali imeshakamilisha ujenzi wa miundombinu vituo vya afya 210 na wakati huohuo vituo vingine vipo katika hatua za ukamilishaji na kuwa najumla ya vituo 350 vilivyojengwa katika Serikali ya awamu ya Tano ya Mhe. John Pombe Magufuli.
Mhe. Jafo ameyasema hayo wakati alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya vya Murriet na Kaloleni vilivyopo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha leo
Amesema vituo vya afya 350 vimejengwa ndani ya miezi kumi na nane (18) ukilinganisha na vituo vya afya 115 viliyokuwa vikitoa huduma ya upasuaji tangu uhuru hadi mwaka 2015 hivyo ni mabadiliko makubwa katika sekta ya afya.
Amewashukuru Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Kamati za Ujenzi na wananchi kwa ujumla kwa kusimamia ujenzi wa miundombinu ya vituo vya afya kwa weledi na kuhakikisha miundombinu hiyo inakamilika kwa wakati na ubora wa hali ya juu.
“Ninawashukuru Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Kamati za Ujenzi wa Vituo vya afya, wananchi kwa kuwa kazi kubwa imefanyakika katika ujenzi wa miundombinu ya afya nchini na kuweza kukamilisha ujenzi huo kwa wakati” Anasema Mhe. Jafo
Mhe. Jafo amekiri kuwepo kwa changamoto za upelekeji wa vifaa tiba kwenye Vituo vya afya vilivyokamilika na kuwaagiza MSD kuhakikisha wanapeleka haraka vifaa tiba kwenye vituo vya afya vilivyokamilika ili viweze kutoa huduma kwa jamii.
“Bado kunachangamoto katika upelekaji wa vifaa tiba katika vituo vya afya vilivyokamilika wakati katika ujenzi wa miundombinu kulikuwa na fedha zilizotengwa kwa ajili ya vifaa tiba amabazo zilipelekwa MSD lakini inasikitisha kila eninapopita kwenye vituo vya afya vifaa tiba bado havijafika, hivyo nawaagiza MSD kuhakikisha wanapeleka haraka vifaa tiba katika Vituo vya afya ili viweze kutoa huma kwa wananchi” Anasisitiza Jafo
Mhe. Jafo anasisistiza kuwa haiwezekani kuwa na miundombinu bora ya afya lakini kunakosekana vifaa tiba jambo ambalo linasababisha kukamisha maendeleo na wananchi kutokupata huduma bora za afya na kwa wakati.
Akiongelea kuhusu changamoto ya Vifaa tiba Mhe Jafo amesema kuwa bado kuna changamoto kubwa ya uwpo wa vifaa tiba hivyo amewaagiza MSD kuhakikisha wanaweledi ujenzi na ukarabaati wa vituo vya afya nchini na kuwa kazi ya mfano katika ujenzi wa miundombinu ya afya na kuwa kazi ya mfano nchini.
Wakati huohuo Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt. Simon Chacha amesema kuwa Ujenzi na ukarabati wa Kituo cha afya cha Kaloleni umegharimu shilingi milioni 400 ambapo hadi sasa ujenzi huo umefikia asilimi 45 na tayari majengo yaliyojengwa ni jengo la X-Rays, Jengo la Wazazi na Upasuaji, jengo la Kufulia nguo na ukarabati wa miundombinu.
Dkt. Chacha anasema kwa upande wa Kituo cha afya cha Murriet jumla ya shilingi milioni 700,000 zimetumika katika ujenzi wa jengo la wagonjwa, maabara, Jengo la Wazazi, jengo la upasuaji, Chumba cha kuifadhia maiti,, kichomea taka, Mfumo wa kuifadhia maji taka na ujenzi wa barabara ndani ya site lengo likiwa ni kutoa huduma za afya katika maeneo ya jirani kwa kuzingatia idadi ya watu wanaokadiriwa kufikia takriban 56401
Video
Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
More Videos
Quick Links
Related Links
World visitors tracker
Location Map
Contact us
Other Contacts
Visitors Counter
Counter Started on: 27th. July 2015
click here
Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.