Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Elimu bure ililetwa tokea mwaka 2015 na sio yeye ililetwa na mwendazake na ndo alisimamia hili yeye samia hajaja na sera ya elimu bure wacha kudanganya
Elimu bure ni sera na ilani ya ccm, na kweli alianza kuitekeleza magufuli, ila samia ametokea chadema ndio shida ilipoanzia
 
Kama hawamkubali Samia watakuwa wanamkubali Mwigulu Nchemba
 
Umesema ukweli kabisa.huyu bibi bora angeongoza kwao tu huko zanzibar lakini siyo huku Tz bara.Na kama ingekuwa umefanyika uchaguzi na siyo urithi asingekuwa rais kabisa.
 
Kama kuna watu 1000 hapa Tz ambao sio wanasiasa wala watumishi wa umma wala wafanyabiashara wanaomkubali rais samia basi nipo tayari kutoa gari yangu

Wanaomkubali Samia kwasasa kati ya watu milioni 60 huku Bara basi hata 1000 hawafiki

Nimetafuta raia wa kawaida anayemuunga mkono huyu bibi hayupo hata 1000 hawafiki nchi nzima

Hakubaliki, hapendwi wala hakuna mwenye hamu ya kumsikia huo ndio ukweli, mtaani ni ngumu sana kumkuta mtu anamkumbali rais Samia ukiachana na watumishi wachache wa umma na wanasiasa, na wafanyabiashara baadhi.

Huo ndio ukweli, mwambieni Rais ukweli kuwa hakubaliki kabisa kwa upande wa Tanzania bara.
Anapendwa na wengi na anakubalika kwa 98%,sisi ccm kindakindaki hutuambii lolote, yapo mapungufu lakini ni kidogo mono! Zaidi yamesimamia kwenye kupanda kwa nafaka za vyakula jambo ambalo linafanyiwa kazi, acha kusemea wengi.
N. B, nchi iliaribika kupitiliza it needs/takes times to heal wounds!
 
1. Elimu bure hadi KIDATO CHA SITA

2. UJENZI WA MADARASA

3. KUPANDISHA MADARAJA YA WATUMISHI NA KUONGEZA MISHAHARA YAO.

4. KODI BILA MTUTU WA BUNDUKI NA DHULMA KWA WAFANYABIASHARA.

5. AJIRA SEKTA ZOTE (ELIMU, AFYA, ULINZI NA USALAMA, TAASISI ZOTE NK)

6. BARABARA NYINGI HASA ZINAZOSIMAMIWANA TARURA.

TUNAWEZA KUANDIKA MPAKA KESHO.

NB. CHUKI ZA DINI YAKE USILETE KWENYE MAISHA YA KAWAIDA NA KUTAKA WATU WENGINE WAMCHUKIA. ADUI WAKO SIO ADUI WETU SISI.
Kwa hiyo asisemwe kwa sababau ya dini yake? Nchi yenye watu kama wewe in haki ya kubaki maskini milele
 
Mnaweza kunambia ni kipi cha maana alichokifanya rais Samia hadi sasa ambacho kimegusa raia wa kawaida au kumsaidia??

Nambieni ni kipi kakifanya ambacho kinaweza kuwa sababu ya yeye kusema amefanya kazi ya kusaidia wananchi wake

Nataka kimoja tu ambacho kakifanya ambacho tunaweza kusema kimemgusa mtu wa chini tokea awe Rais
TOZO limemgusa sana Mtu wa CHINI
 
Mkuu ngoja tuwekane sawa...

1. Mama ameongeza tu miaka miwili ya A'level, lakini iyo ilikuwa ni sera ya mzee magu kuwa elimu bure adi kidato cha nne.

2. Madarasa yalishajengwa miaka mingi isipokuwa labda useme ameboresha miundombinu chakavu za madarasa na kuweka vifaa kazi vya kufundishia.

3. Hapo kwenye kupandisha madaraja na mishahara nampa pongezi lakini kuna maana gani kuongeza mishahara na huku garama za maisha na mfumuko wa bei ukiongezeka pia siku hadi siku(natumai ili unalifahamu hususani katika bidhaa za madukani tuzitumiazo kila nyakati NI TATIZO KUBWA).

4. Kodi bila mtutu, sawa ni nzuri hasa kwa kuwa kuna unafuu kwetu sie masikini lakini apo ndo anapigwa na matajiri/wafanyabiashara wakubwa...kwakuwa hakuna mifumo sahihi ya kudumu ya ukusanyaji kodi isipokuwa nguvu ya ukusanyaji mapato ndo imepungua.

5. Ajira za serikali alizotoa mama tumeshuhudia wazi sanasana ni za Afya na uwalimu...unavyosema ajira za taasis zote...unamaanisha zipi mbali na izo?

6. Hapo kwenye barabara ndo kabisa labda useme tu mama ameboresha ila asilimia 99% ni miradi aliyoitekeleza magufuli...kama hutojali tuwekee hapa barabara mpya zilizoanzwa kujengwa na rais samia(sio kukamilika kipindi hiki alichokuwa yeye rais)

NB: NA MWISHO KABISA MTOA MADA HAKUONYESHA VIASHIRIA VYA UDINI NA MADA YAKE, HIVYO NA WEWE UWACHE KUHUSISHA DINI YA MTU/WATU NA UTENDAJI WAKE PIA.
Samahani wewe ni MJINGA, yaan samahani sana. NCHI HII KUNA RAIS ALIFANYA MAPYA KAMA SIO MWENDELEZO WA YALIYOPITA? Hivi huwa mnafikirikia kwa kutumia makalio au akili??

Mmetaka alichofanya mmewekewa sasa mnaanza kubishia nini?? Huyo boya wenu MAGUFULI alifanya nini lenye manufaa kwa watu wa CHINI??
 
Mnaweza kunambia ni kipi cha maana alichokifanya rais Samia hadi sasa ambacho kimegusa raia wa kawaida au kumsaidia??

Nambieni ni kipi kakifanya ambacho kinaweza kuwa sababu ya yeye kusema amefanya kazi ya kusaidia wananchi wake

Nataka kimoja tu ambacho kakifanya ambacho tunaweza kusema kimemgusa mtu wa chini tokea awe Rais
Ajira. Jpm hajaajiri miaka mitano yote lakini mama kaajiri walimu na madaktari na bado anaendelea. Jpm msisitizo wake ulikuwa watu wawe mamachinga hata kma una degree au masters kata kitambulisho kuwa machinga.

Uwekezaji umerudi kwa kasi. Pale manzese mahoteli takaribani yote yalifungwa kwabiasjara kuwa mbaya lakini sasa yamefunguliwa wale waliosoma hotel management wanaenjoy baada ya kusota mtaani sasa Wana ajira. Kule Arusha utalilii umeshamili hivyo waliosoma tourism wanapata ajira kwa mamia. Kule bagamoyo viwanda vya chumvi vilikufa kifo Cha mende kipindi Cha jpm sasa vimesimama na vinaajori watu kwa mamia. Financial institutions sasa zinatengeneza faida na watu wanakopa pia graduates wanaajiriwa japo so wote lakini alhamdulilah.

Sasahivi kuna Uhuru na tunaenjoy kuwa watanzania badala ya kipindi Cha jpm tunaogopana wenyewe kwa wenyewe Kama tuko uhamidhoni.

Hakuna mwananchi wa kawaida anayeokotwa kwenye viloba tena kule kokobeach.

To conclude, jpm aliharibu Kila Kona ya nchi hii mpaka nikahisi kuhamia Burundi. Hata mo alitaka kuikimbia nchi hii.
 
Kwa hiyo asisemwe kwa sababau ya dini yake? Nchi yenye watu kama wewe in haki ya kubaki maskini milele
Mama Samia anaandamwa zaidi na DINI yake, ila kwa kazi zenye manufaa na UWAZI amemuacha mbali sana MAGUFULI. Uongozi sio vitisho, ni kuongoza kwa taratibu na sheria, Haya Kabudi aliongea wazi kuwa ile ishu ya MAKINIKIA walitung uongo. Sasa ile ilitusaidia nini??

Mada nyingi za Mama Samia zimejificha kwenye CHUKI ZA DINI YAKE. Hali hii hata kwa KIKWETE. WAKRISTO mara zote huwa mnahisi mko njia sahihi, na huwa mna beba sana chuki za kipumbavu.

HAYA NIAMBIE WEWE KUNA JAMBO LINALOIGUSA JAMII MOJA KWA MOJA KUSHINDA AJIRA, UPANDIASHWAJI WA MADARAJA NA VYEO???

Magufuli aliwahi kufanya hayo??? Acha chuki, hazitokusaidia, and pata kujua hii nchi ni ya wote na kila mtu ana haki ya kuongoza.
 
Mnahangaika bure kwani hakuna marehemu aliyewahi kufufuka zaidi ya kristo.
Enyi wafuwasi wa Kayafa ifike mahali mkubali matokeo.
Yule dhalimu hawezi kurudi tena.
Wasalimie usukumani mkuu.
"Mwangaluka mayoo"
Nani alikudanganya yechu alifufuka?,kile kipigo hakikuwa cha mchezo [emoji706][emoji706]
 
Nataka kimoja tu ambacho kakifanya ambacho tunaweza kusema kimemgusa mtu wa chini tokea awe Rais
Amewezesha wananchi wote kushiriki katika kuchangia maendeleo ya Taifa badala ya jukumu hilo kuwaachia wafanyakazi wa Umma na wafanyabiashara wakati na wakubwa baadhi. Sasa hivi mkulima, mvuvi, muwindaji, muimbaji, mchekeshaji, wataje unao wajua hawa wote wanashiriki kikamilifu bila shuruti kuchangia Pato la Taifa, furusa ambayo walinyimwa siku nyingi.

Sidhani kama utaniuliza hawa wananchi wanachangiaje Pato la Taifa. Eti, utaniuliza kweli swali hilo?
 
Ameboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania

Kazi ya serikali sio kumsaidia kila mtu, ni kutengeneza mazingira ambayo watu wanaweza kuyatumia kuboresha maisha yao. Mazingira ya biashara yamekuwa bora zaidi, shughuli za kiuchumi zimeongezeka, ujenzi umeongezeka, mauzo ya chakula nje yameongezeka; mabenki yanatengeneza faida haijawahi kuonekana hapa Tanzania i.e mikopo inakopwa na inalipika.
 
Mnaweza kunambia ni kipi cha maana alichokifanya rais Samia hadi sasa ambacho kimegusa raia wa kawaida au kumsaidia??

Nambieni ni kipi kakifanya ambacho kinaweza kuwa sababu ya yeye kusema amefanya kazi ya kusaidia wananchi wake

Nataka kimoja tu ambacho kakifanya ambacho tunaweza kusema kimemgusa mtu wa chini tokea awe Rais
Kuanzisha tozo za huduma mbalimbali za kifedha.
 
Acheni uongo...nina ndugu yangu ni mmoja wa aliyepata ajira ya afya serekalini kipindi cha mzee. Magu kupitia mkono wa taasisi ya benjamini mkapa foundation 2018.

Mpaka rais magu anafariki katika kipindi cha 2015-2020 alikuwa amekamilisha ujenzi wa vituo vya afya.498. Na vingine vikiwa bado vinaendelea kujengwa...na hivyo ndo vimekamilika kipindi hiki cha rais samia, ivyo huo sio mradi wake bali ni mpango wa utekelezaji wa awamu ya tano na sio sita(ya samia).

Ona hapo ni 2018...utekelezaji wa hiyo miradi ya Vituo vya afya, zahanati, hospitali za rufaa wilaya na mikoa. Sikumbuki idadi kamili zilikuwa ngapi(zahanati, hospitali za rufaa wilaya na mikoa). Ila ulikuwa ni mradi wa Rais.Magu na sio Samia.

President's Office - Regional Administration and Local Government

Toggle navigation

JAFO: Ukamilishaji wa Ujenzi wa vituo vya afya 210 nchini ni wa kihistoria.​

thumb_1704_800x420_0_0_auto.jpeg
Posted On: November 9th, 2018
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa tayari serikali imeshakamilisha ujenzi wa miundombinu vituo vya afya 210 na wakati huohuo vituo vingine vipo katika hatua za ukamilishaji na kuwa najumla ya vituo 350 vilivyojengwa katika Serikali ya awamu ya Tano ya Mhe. John Pombe Magufuli.
Mhe. Jafo ameyasema hayo wakati alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya vya Murriet na Kaloleni vilivyopo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha leo
Amesema vituo vya afya 350 vimejengwa ndani ya miezi kumi na nane (18) ukilinganisha na vituo vya afya 115 viliyokuwa vikitoa huduma ya upasuaji tangu uhuru hadi mwaka 2015 hivyo ni mabadiliko makubwa katika sekta ya afya.
Amewashukuru Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Kamati za Ujenzi na wananchi kwa ujumla kwa kusimamia ujenzi wa miundombinu ya vituo vya afya kwa weledi na kuhakikisha miundombinu hiyo inakamilika kwa wakati na ubora wa hali ya juu.
“Ninawashukuru Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Kamati za Ujenzi wa Vituo vya afya, wananchi kwa kuwa kazi kubwa imefanyakika katika ujenzi wa miundombinu ya afya nchini na kuweza kukamilisha ujenzi huo kwa wakati” Anasema Mhe. Jafo
Mhe. Jafo amekiri kuwepo kwa changamoto za upelekeji wa vifaa tiba kwenye Vituo vya afya vilivyokamilika na kuwaagiza MSD kuhakikisha wanapeleka haraka vifaa tiba kwenye vituo vya afya vilivyokamilika ili viweze kutoa huduma kwa jamii.
“Bado kunachangamoto katika upelekaji wa vifaa tiba katika vituo vya afya vilivyokamilika wakati katika ujenzi wa miundombinu kulikuwa na fedha zilizotengwa kwa ajili ya vifaa tiba amabazo zilipelekwa MSD lakini inasikitisha kila eninapopita kwenye vituo vya afya vifaa tiba bado havijafika, hivyo nawaagiza MSD kuhakikisha wanapeleka haraka vifaa tiba katika Vituo vya afya ili viweze kutoa huma kwa wananchi” Anasisitiza Jafo
Mhe. Jafo anasisistiza kuwa haiwezekani kuwa na miundombinu bora ya afya lakini kunakosekana vifaa tiba jambo ambalo linasababisha kukamisha maendeleo na wananchi kutokupata huduma bora za afya na kwa wakati.
Akiongelea kuhusu changamoto ya Vifaa tiba Mhe Jafo amesema kuwa bado kuna changamoto kubwa ya uwpo wa vifaa tiba hivyo amewaagiza MSD kuhakikisha wanaweledi ujenzi na ukarabaati wa vituo vya afya nchini na kuwa kazi ya mfano katika ujenzi wa miundombinu ya afya na kuwa kazi ya mfano nchini.
Wakati huohuo Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt. Simon Chacha amesema kuwa Ujenzi na ukarabati wa Kituo cha afya cha Kaloleni umegharimu shilingi milioni 400 ambapo hadi sasa ujenzi huo umefikia asilimi 45 na tayari majengo yaliyojengwa ni jengo la X-Rays, Jengo la Wazazi na Upasuaji, jengo la Kufulia nguo na ukarabati wa miundombinu.
Dkt. Chacha anasema kwa upande wa Kituo cha afya cha Murriet jumla ya shilingi milioni 700,000 zimetumika katika ujenzi wa jengo la wagonjwa, maabara, Jengo la Wazazi, jengo la upasuaji, Chumba cha kuifadhia maiti,, kichomea taka, Mfumo wa kuifadhia maji taka na ujenzi wa barabara ndani ya site lengo likiwa ni kutoa huduma za afya katika maeneo ya jirani kwa kuzingatia idadi ya watu wanaokadiriwa kufikia takriban 56401

Video​


Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22​

More Videos

Quick Links​

Related Links​

World visitors tracker​

world map hits counter


Location Map​


Contact us​

Other Contacts



Visitors Counter​

Counter Started on: 27th. July 2015​

click here
matomo.php



Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.
Wewe unamatatizo kichwani, kwani Hayati Dr Magufuli Alikuwa Ni mgombea Binafsi? Kwani Hakuwa na chama? Kama alikuwa na chama ni chama gani? Halafu hata bila aibu unajenga hoja kwa kusema mdogo wako alipata ajira 2018,swali je kupata ajira kwa mdogo wako ndio kulizuia ajira zisitoke kipindi hiki Cha mama Samia? Au mdogo wako kupata kazi ndio ajira zikafungwa serikalini mpaka leo? Au ulitaka kuleta ujumbe gani hapa kuhusu kuajiliwa kwa mdogo wako?

Alipofariki Dr Magufuli mama Samia alikuwa Ni Nani serikalini? Vipi mh kasimu majaliwa? Uliona uchaguzi mkuu ukiitishwa Tena? Unajuwa kwanini haukuitishwa kwa akili yako? Jibu Ni kuwa Ni kwa kuwa mh Rais wetu mpendwa kipenzi Cha watanzania Alipiga kampeni na aliinadi ilani ya CCM na alikuwa katika utekelezaji wake katika kipindi chote na hata alipofariki Hayati Magufuli na kuapishwa mama samia kwa mujibu wa katiba yetu alikuwa anajuwa kazi iliyopo mbele yake,

Mama Samia Rais wetu kafanya mambo makubwa Sana ndani ya muda mfupi Sana, mpaka amalize miaka yake hiyo 2030 hakika Tanzania itakuwa inapendeza sanaaa na kuvutia Sana, Hutaki unataka huyu ndio Rais Wako tuu labda uhame nchi, na kwa akili yako utaenda kuwa mtumwa ugenini
 
Back
Top Bottom