Kwani mbolea haujaona namna zilivyopungua Bei? Japo Sina uhakika Kama hata unafahamu habari za kilimo maana katika kusoma maelezo yako nimeona Ni mtu ambaye huna taarifa nyingi Sana juu ya yanayoendelea hapa nchini katika secta nyingi tu,Sasa Kama hufahamu ni kuwa mbolea zilipaa Sana Bei na siyo hapa tu Bali maeneo mengi tu katika Bara la afrika, lakini mh Rais wetu mpendwa mama Samia kwa umadhubuti na ushupavu wake kiuongozi akaamua kuwaokoa wakulima kwa kuamua kutoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini Hali iliyopelekea kushuka kwa Bei ya mbolea zaidi ya nusu ya Ile ya msimu uliopita sokoni,
Sasa je hapa wewe huoni kuwa mh Rais amewagusa wananchi moja kwa moja? Huoni kilimo Ni pumzi ya watanzania wanyonge walio wengi? Huoni hapa Ni Kama mama Amewapa pumzi mpya na Safi mamilioni ya wakulima? Huoni ameleta matumaini kwa watanzania? Unajuwa athari ya mtu kuishi bila matumaini wewe?
Vipi kuhusu bajeti ya kilimo? Unajuwa mama aliikuta Ni shilingi ngapi na kwa Sasa Ni shilingi ngapi? Unajuwa Ni vipi kilimo kwa Sasa kimekuwa na tija kutokana na juhudi za mh Rais wetu kutilia mkazo?
Najuwa huwezi ukayaelewa haya maana akili yako imefubazwa na chuki zilizojaa katika akili na moyo wako juu ya Rais wetu mpendwa, lakini utake usitake huyu ndiye Rais wako mwenye kibali Cha watanzania na ambaye amepewa baraka zote na watanzania kutuongoza Hadi 2030
Pia lazima ufahamu kuwa Ni utaratibu wa Rais yoyote Yule katika nchi yetu kufanya Kama ambavyo baba wa Taifa amewahi kutuasa kuwa unaanzia alipoishia mwenzio katika Yale mema na kurekebisha Yale yenye kasoro, huuwi ulivyovikuta Wala huviharibu ulivyovikuta Bali unakamilisha,kuendeleza na kukamilisha vilivyokuwa katika mipango na mikakati ikiwa tu vitaonekana vina faida pale vitakapokamilishwa na hapo ndipo hatua zako zinapoanza katika kuibua au kuanzisha na kutekeleza miradi mingine,mikakati mingine kulingana na bajeti itakavyoruhusu na uchumi wa wakati huo,
Amefanya hivyo Samia ,alifanya hivyo Hayati Magufuli na atafanya mwingine pia miaka ya mbele huko, kwa hiyo acha ushamba wa kiuongozi, nchi ina utaratibu wake wa kimaendeleo, chama ni kimoja kilichoongoza nchi hii na kitakachoendelea kuongoza nchi hii, kwa hiyo hakuna anayekuja kuongoza nchi utazaninmgombea binafsi, Soma uelewe , siyo kuandika tu utazani mtu alikuwa peke yake katika kwenda kufanya vibarua na kuleta hela za kujengea nchi yetu,Urais Ni Taasisi siyo mtu binafsi
Na wala sikumaanisha eti kupata ajira kwa uyo mtu...kuzuie rais samia asitoe ajira kwa wengine.
Na hakuna niliposema Magufuli alikuwa mgombea binafsi SOTE TUNAFAHAMU alikuwa ni wa CCM, Na maana ya kwamba miradi ya maendeleo iliyowepo katika ilani ya CCM awamu ya tano tunaifahamu. Na hadi ivi sasa tupo ndani ya miaka miwili ya awamu mpya ya sita...semeni kipi kipya ambacho hakijaachwa na hayati Magu kimefanywa na mama samia???
Maana itakuwa ni upumbavu leo hii Stiegler's Gorge ikamilike alafu tuseme MAMA SAMIA AMEJENGA KATIKA AWAMU YAKE YA 6. Wakati inafahamika kuwa mradi uliletwa na magu akauwacha ukiendelea kutekelezwa na bajeti yake ikiwa ilishapangwa kabisa. Tokea awamu ya tano.