Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

MATAGA bhana..
Kwani jiwe alikuwa anakubaliana na kuendeleza ya mtangulizi wake yoote?

Mfano 1 tu, Bandari ya Bagamoyo vipi?

Kila mmoja anakuwa na MAONO, hawezi kuenenda kwa kufuata tu nyayo kama kasuku.

Mfano, angalia USA. Siku ya kwanza tu rais mpya akiingia ofisini, anabatilisha "presidential decrees" kibao za mtangulizi wake na ku saini "executive orders" na "memorandum" nyiiiingi utafikiri ndo kwanza nchi imepata uhuru siku hiyo!

MATAGA mlizoea kukalia wananchi vichwani, tena kwa uonevu na dharau.

Mkombozi wa kweli kapatikana, muacheni afanye kazi ya UKOMBOZI kuitoa nchi UTUMWANi
 
Sasa mm sio unafiki hapo. Kama mtu aliwaikusema ukimshauri ndio una mvuruga kabsaa, unategemea hapo watu waishije nae? Kama sio kwenda kama anavyotaka yeye?

Mazingira ya unafiki aliyatengene hayati mwenyewe. Kwaiyo ata huyu akitaka kuabudiwa ajue atakuwa anajitengenezea mazingira ya kunafikiwa mwenyewe
 
Sio yeye tu hata WaTanzania ni wanafiki sana. Mfano inajulikana kabisa kuwa Tundu Lisu aliibiwa kura, wagombea wa upinzani wengi waliibiwa kura lakini WaTanzania tunajua na tukanyamaza kimya. Unafiki unatusumbua sana.

Hapa ndipo waKenya wanatupigiaga hapa. Wana ujasiri wa kupinga uzinguzi.

Afadhali huyu anayeruhusu kuzinguliwa ili naye akuzingue.

Yule hakutaka hata kuzinguliwa kabisa.
 
Mwacheni Mama afanye kazi msiwashwewashe,; hamjui jinsi watu walivyokosa matumaini chini ya mwenda zake; hotuba mbili tu watu wameshaanza kureje
sha furaha hata kama hawana fedha, lakini wanayo amani.Kaza hapo hapo mama.Kama yeye hakutaka kupangiwa maneno nawe Fanya hivyo hivyo.
 
Unafiki wake nini, mbona hayati nae alikuwa hivo hivo wakati anamuambia JK asafir tu ili alete mahela, alivoingia unakumbuka akasemaje na akatendaje?

Mtateseka sana, nchi imechukuliwa na CDM kiulaini bila hata push up yani
Ala kumbe CDM wako Ikulu ? Duh, maajabu hayataisha duniani !
 
Watu kama nyie ndio maana magufuli alikuwa anawanyosha sana

Unawezaje kumwita Rais wa inchi yako Mnafiki?
 
Huo uhuru wa kuandika hivi, ni kwa ajili ya Yeye! Mwezi uliopita tu usingethubutu kuandika haya!

Muacheni mama afanya anavyoona inafaa misilazimishe WAFANANE!

Mbona awamu ya tano iliwasimanga awamu ya nne na walivumilia?
 
Mkono wa chuma tuliuzika chato, kwa sasa tuna mkono wa nyama unaojua maumivu ya kuumizwa,
Ni nani aliyekuwa anaweza kumshauri au kumkosoa bwana yule?
 
Ni mzuri sana leo tungejuaje bado tunapigwa Mererani pamoja na kujenga ukuta wa mamilioni, atcl hasara tupu wakati mwendakwao alitudanganya anatengeneza faida, wewe ulitaka tudanganywe mpaka lini, wa ajabu sana wewe
 
MATAGA bhana..
Kwani jiwe alikuwa anakubaliana na kuendeleza ya mtangulizi wake yoote?

Mfano tu, Bandari ya Bagamoyo vipi?

Kila mmoja anakuwa na MAONO, hawezi kuenenda kwa kufuata tu nyayo kama kasuku.

Mfano, angalia USA. Siku ya kwanza tu rais mpya akiingia ofisini, anabatilisha presidential decrees kibao za mtangulizi wake na ku saini "executive orders" nyiiiingi utafikiri ndo kwanza nchi imepata uhuru.

MATAGA mlizoea kukalia wananchi vichwani.

Mkombozi wa kweli kapatikana, muacheni afanye kazi ya UKOMBOZI kuitoa nchi UTUMWANi

Tatizo lenu watu wengine ni kwamba ushabiki wa kisiasa ndio mnaouweka mbele. Huoni kwamba JPM alikuwa ana ilani yake na watangulizi wake nao walikuwa na ilani zao?
 
Tukisema huyu Mama hajielewi wala haelewi hii nchi inataka nini kwa sasa,kuna watu wanakuja na hadithi za Sukuma Gang Mara MATAGA!!

Acha ujjnga wako wewe taga!!
Huyu alikuwa ni VP wa Jiwe,JPM,Mwamba, Dikteta and whatever you may call the late!

Unaposema huyu mama hajielewi means hata mtangulizi wake WOTE HAWAJIELWI na kwa lugha rahisi ni kwamba CCM HAIJIELEWI WATZ WANATAKA NINI??
Marehemu Magufuli kwa miaka 5 amewaburuza Watanzania bila kujua wanataka nini....!!!
Nashangaa sana mataga leo mnapoanza kumlaumu mama aliyekuwa msaidizi wa CCM YA MAGUFULI na TANZANIA YA MAGUFULI...!!!
Shame on you CCM members and all Matagas. This time around CCM mtaisoma namba!! GOD ALWAYS DO THINGS IN A VERY PECULIAR AND UNDEFINED WAY NOT UNDERSTANDABLE TO MANKIND!!!
Yale ya KANU ya Kenya yanakwenda kutokea Tanzania. Watch 2025, time gonna tell!
 
Nyiee acheni mambo yenu, Zama za Mwendazake zimeshaisha.
Kwani JPM alijiuzulu uwaziri wakati wa Kikwete? Mbona hamkumuita mnafiki wakati anamkosoa hadharani baada ya kuwa raisi?
Msiwe ma sore looser, mipango ya mungu haiwezi shindwa na nyie wanadam.
 
Mama Samia ndio mwokozi, Watanzania walikuwa wanamsubiria... Praise team mtahama nchi..

Mnafiki ni yule aliyekuwa anajifanya mtetezi wa wanyonge kumbe hana lolote...
Eti tunajenga kwa fedha zetu za ndani, kumbe ni fedha za mikopo...

Akwende zake huko akaongoze malaika...
Eti Malaika! Unadhani Malaika wanafuata amri ya Kibwengo chochote?

Malaika hufuata amri za Muumba wao tu.
 
Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
Wafuasi wa Jiwe hamuamini macho yenu. Vumilieni ustaarabu unaporejeshwa . Huyo mwendazake keisha maliza majukumu yake na hawezi kunyanyuka tena .

Mnapoambiwa katiba mbaya muwe mnaelewa. Tunayo katiba ambayo Rais ana mamlaka ya kimungumtu . Akiingia atafanya chochote na huwezi kumfanya kitu . Tuwe na katiba itakayoilinda nchi dhidi mtu yeyote wakiwemo viongozi .

Odhis *
 
Tatizo lenu watu wengine ni kwamba ushabiki wa kisiasa ndio mnaouweka mbele. Huoni kwamba JPM alikuwa ana ilani yake na watangulizi wake nao walikuwa na ilani zao?
Ilani kitu gani?!!!

Kile ni kipeperushi cha kikundi kidogo tu cha watu, wala hakina uhusiano wowote na matakwa ya umma wa wananchi
 
Back
Top Bottom