Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Suluhisho ni utawala wa majimbo, ni vigumu Rais kuchagua watu wazuri wa kuwaweka kila mahali nchi hii ni vigumu sana, haiwezekani.
Raia wachague viongozi wao wenyewe kwa kura katika Mikoa, Wilaya na Halmashauri.
 
inawezekana anaogopa kutia mguu tanesco kuna mirija minene ya wazito wenzake asije akawaudhi
Mmesahau yale masandarusi !! Na Richmond je ?!! Symbion je ?!! Wanene ni shida huwa hawaridhiki mpaka wanaingia kwa mwanandani !!
Suluhisho ni utawala wa majimbo, ni vigumu Rais kuchagua watu wazuri wa kuwaweka kila mahali nchi hii ni vigumu sana, haiwezekani.
Raia wachague viongozi wao wenyewe kwa kura katika Mikoa, Wilaya na Halmashauri.
Kabisa kabisa! Nchi hii ni kubwa sana na ina watu selfish sana ! Kipindi cha Mwalimu utawala ulikuwa hauna matatizo sana maana watu walikuwa wachache sana !! Wakati wa Uhuru walikuwepo milioni nane tu. !
 
KamaWasaidizi wake hawamsaidii aendelee kuganda tu ofisini akisubiri kudra za mungu?,wewe ni hopeless kabisa,tena [emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]kabisa
 
Akili ni nywele na marope ana kipara [emoji17][emoji17]
 
Sio mpaka uende kila mahali mfano mrahisi,

Jiwe alijuaje wachungaji wanauza vifaa vilivyokuja kwa msamaha wa kodi..?

Alijuaje mabwawa ya kufua umeme yanafunguliwa usiku ili sababu iwe kina cha maji kimeshuka wauze majenereta yao..?

Alijuaje butimba kuna simu na biashara ya ganja...?

Alijuaje, alijuaje alijuaje...?

Kuwa Rais sio mpaka uende kila sehemu unahitaji watu sahihi wa kukupa info hilo tuu.
 
Hizi ndo akili nazo chukia, yaani tunasubiri mtu atutetee?
 
Unaongea kama Tanesco, ATCL na hao wengine walikuwa kama Google au Apple! ni lini mashirika haya yalikuwa na unafuu, maana toka tumepata uhuru hata tuliyorithi kwa wakoloni tumefilisi nitajie shirika moja lilikuwa imara na awamu hii linakufa. Tumefilisi mpaka vyama vya ushirika. Toka Nyerere. Mwinyi, Mkapa, Kikwete na JPM wanaweza kujivunia shirika hili la uma limesimama. wizi mtupu.
 
Nakubaliana na kitu kimoja tu January hafai hili naunga mkono.
 
Wapo lakini pekee yao hawatoshi. Tumempata Bashiru kaanza na wakulima, Ndugai alikaa na mikopo naye kamaliza. Sasahivi tunawahitaji hawa wengi sana badala ya kulia lia tuamke tuliamshe, kumwachia Bashiru pekee ni kujisariti wenyewe
 
Kwahiyo akichezea kipigo itambadili fulani kua malkia ?
 

Na hapo ndio wabongo / wasaidizi wanampiga sana
Kwa tanzania viongozi wote mawazo yao ni kupiga ela,

Nakupa mfano wa ile ishu ya kuchora twiga kwenye ndege, bajet yake ilikuwaje?

Kwa tanzania bila kuwa close kwenye mashirika ni wizi tu
 
Nii lini hayo mashirika yetu ya umma yalisonga mbele tangu enzi za JKN?

Mfano:
1) Shirika la ndege ATC tangu lilipoanzishwa lilikuwa la kubahatisha mwisho likaitwa Any Time Cancellation (tunakumbuka sana)
2) NDC sijui iliishia wapi.
3) TANELEC je imekwenda wapi?
4) TRC hakuna maendeleo yo yote linachechemea
5) Bandari ndiyo usiseme miaka yote hiyo bado tuko pale pale kazi wachache kupiga pesa tu
6) Viwanda vya Urafiki, Mwatex, Cotex, Tanganyika Packers vimeishia wapi?

Munataka kumtwika Rais mzigo ambao ulimshinda Mnyamwezi kuubeba kwa kumuonea tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…