Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Katufanya tuuone Muungano ni wa kikuda hapo zamani,hatukuwahi kujua kuwa hawa wazanzibar,wanaitamani Tanganyika yetu, wametunyonya sasa wanataka watuuze na sisi kama Loliondo kwa waarabu na wauze nchi yetu kwaarabu,
#Muungano ni utapeli,Kataa Muungano
 
Katufanya tuuone Muungano ni wa kikuda hapo zamani,hatukuwahi kujua kuwa hawa wazanzibar,wanaitamani Tanganyika yetu, wametunyonya sasa wanataka watuuze na sisi kama Loliondo kwa waarabu na wauze nchi yetu kwaarabu,
#Muungano ni utapeli,Kataa Muungano
[emoji1][emoji1787][emoji38][emoji38]
 
Miradi ya JPM:
1. SGR
2. NYERERE HYDROELECTRIC POWER
3. Upanuzi wa barabara njia 8 + 4(service road)=12 kimara mpaka kibaa
4. Rada 4 za kulinda anga la Tanzania
5. Kufufua ATCL kanunua ndege 12
6. Elimu bure
7. Viwanda (kalakana/gati) za kutengeneza meli ziwa Victoria
8. Daraja lefu zaidi East Africa na kati 5km la busisi ziwa Victoria
9. Elimu bure
10. Makazi bora ya vyombo vya ulinzi (polisi) nchi nzima
11. Kuunganishiwa umeme vijiji vyote karibu na bure kwa kulipa tu 27,000/= ulishaona wapi?
12. Hostel za wanafunzi UDSM
13. Serikali kuhamia Dodoma
14. Ikulu mpya Dodoma chamwino
.
.
n.k

Ongeza nyingi
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] eti uliona wapi
 
Kampa mbowe ruzuku anakula na watoto wake... Kamrudisha Lissu bongo anaishi hana pakukaa... Kamrudisha na kumlipia Lema deni la mkopo crdb alilokua amelikimbia... Kubwa zaidi nchi ipo huru wawekezaji kila kona... 💩💩💩
 
FM02cfoXMAI9nVX.jpeg
 
Kampa mbowe ruzuku anakula na watoto wake... Kamrudisha Lissu bongo anaishi hana pakukaa... Kamrudisha na kumlipia Lema deni la mkopo crdb alilokua amelikimbia... Kubwa zaidi nchi ipo huru wawekezaji kila kona... [emoji90][emoji90][emoji90]
Ujaelewa uzi! Hivyo vitu ni too common hata kila Rais anafanya: mfano JPM alimtoa Babu seya kifungoni. Kwa wenye akili uwezi kusema eti hilo ni jambo lenye mashiko

Lete jambo lenye mashiko ambalo amefanya hadi sasa SSH
 
Mama anawafanya watu wacheke na familia zao, kila mwaka anatoa ajira kwa vijana sio walimu, afya na kila idara inalamba ajira, pia anaendeleza yale mazuri ya mtangulizi wake, anajenga miundombinu ya barabara kila mkoa, anapeleka maji kila sehemu, kupandisha mishahara na kuwapandisha grade wafanyakazi, kuongeza bajeti ya kilimo pamoja na tarura.... Mimi naona yupo sawa japo na yeye ana mapungufu yake lakini anajitahidi sana.
Umeongea umbeya tu,
Mfano c lazima Wote tuajiriwe ,nimemaliza chuo Miaka 4,ckuwahi kuomba Ajira na sina Mpango ,niliamua kujiajir,
-Ajira cyo creativity,nchi za wenzetu watu hawawazi kuajirowa wanawaza wawe creativity ndo mana nafasi zipo.
Kumlipia sijui nani cjui,kumpa mbowe hela,
Inafaida gani kwa uchumi wetu ....!!
Hafai

Anatuuza

Mm nahisi angeanzia zanzibar kwanza,huku hapana
 
Yeye anatekeleza Ilani ya chama chake kulingana na bajeti sasa unataka abuni nini hicho ambacho hakipo kwenye Ilani .Kumbuka anayoyafanya ni kutekeleza ilani ya Chama tu hatakiwi kubuni jambo jipya.JPM aliyokuwa akiyafanya ilikuwa kutekeleza Ilani.
Halafu siyo lazima kuweka thread unaweza kusoma za wengine.
Za wengine zipi! Hii thread ni unique ndo maana mod ajaiunganisha na nyingine
 
ANAANDIKA BABA ASKOFU BAGONZA (PhD)

BANDARI: Tumefikaje? Tutatokaje?

Mjadala wa “kuuzwa”, “Kubinafsishwa”, “Kukodishwa” au vyovyote ilivyofanywa, umeonyesha nyufa za hatari katika nyumba yetu TANZANIA. Nitaje kadhaa:

1. Rushwa

Rushwa bandarini ndiyo imesababisha bandari ifanywe inachofanyiwa. Wakiishapeana rushwa, serikali inakosa mapato, mizigo inachelewa, inapotea, na bandari limekuwa pango la majizi.
Swali ni je, kila penye rushwa tuuze? Tubinafsishe? Tukabidhi sekta binafsi? Je rushwa ikishika kichwani na moyoni? Tujadili ufa huu bila jazba. Rushwa itavuruga wawekezaji wapya.

2. Umoja na Utaifa

Mjadala umeonyesha, wanaodai wanaujenga/kuutetea umoja na utaifa, ndio wanaubomoa. Wanaoonekana kuubomoa, ndio wanaujenga. Bandari imeujeruhi umoja na utaifa wetu. Hii ina gharama mbeleni. Tumejuana, tuishi kwa tahadhari.

3. Udini na Siasa Zetu

Viongozi wetu wana dini zao. Sitamani kuchagua kiongozi asiye na dini. Tatizo tunalo viongozi wa dini. Tunawakosoa viongozi wa dini ileee na kupongeza wa dini zetu. Au tunanyamaza mpaka tupigwe sindano ya kupongeza badala ya kushauri. Inapendeza kumkosoa na kumshauri kiongozi wa dini yako japo haizuiwi kumkosoa wa dini isiyo yako.

4. Ujuzi wa Sheria na Uchumi.

AJABU: Wanasheria walioongea tukaelewa ni wachache sana. Walio wengi ujanja wao unaishia Kisutu.
Wanauchumi wetu ujanja wao unaishia Kariakoo. Mkataba huu hawauelewi na wakiuelewa hawatuelezi tukaelewa. Huu ni ufa wa hatari.

5. Bunge

Hili lingebinafsishwa kabla ya bandari. Walichoongea bungeni sicho wanachoongea mitaani na kwenye baa. Wanamdanganya rais kuwa wanamuunga mkono wakati wamebeba mishale ya kumwangamiza. Mjadala wa Bandari umefanywa mgumu na bunge letu.

6. Serikali

Mjadala na tabia za watu vimeonyesha serikali hii si ya rais Samia hata kama kaiteua yeye. Hii ni mchanganyiko wa serikali zilizopita. Ina utii uliogawanyika - kiapo kimoja Chamwino na vingine huko makaburini, Msufini, na Butiama. Serikali bila “Uwajibikaji wa pamoja” ni sawa na genge la wasela. Ufa huu unadai tuanze upya.

7. Rushwa part 2.

Katika Mjadala wa Bandari tumesikia malalamiko ya rushwa za aina tatu: Wanaonufaika na uzembe wa bandari wakikazana kukwamisha mkataba; DP World wakikazana mkataba upite; na wanaoitwa wazalendo wasio wa taka DP World wala wazembe wa bandari LAKINI bila kutoa suluhisho. Ufa huu ni mgumu kuushughulikia bila kuchelewesha mkataba na kusikilizana kwanza.

8. Rais Wetu

Rais SSH ni wetu sote. Ni muhimu kama taifa kumkinga na mipasuko inayotokana na mjadala huu. Kuna maisha baada ya mjadala wa bandari. Yeye analo jukumu la kutuongoza sote na makundi yote mpaka tuvuke. Subira itatufundisha kuliko haraka. Ufa huu unazibwa kwa kusikiliza na kuchukua hatua.

9. Miafaka yetu

Mjadala huu umejeruhi miafaka yetu na kufukua baadhi ya makaburi. Baadhi ya makaburi tumekuta marehemu hawajaoza.
Katiba, maridhiano, Muungano, maelewano ya kidini, uhuru wa maoni na mamlaka ya wananchi bila bunge ni mambo muhimu sana katika kuziba nyufa zilizojitokeza.

10. Upinzani wetu

Mjadala unaonyesha aina mpya ya upinzani. Ndani ya chama tawala na serikali kuna upinzani mkali dhidi ya suala la bandari. Hii ni afya kwa nchi lakini hatari kwa utawala. Vyombo vyetu vijifunze kutotumia nguvu kupambana na maoni. Bora upinzani wa hadharani kuliko wa moyoni.

Nawashukuru wooote wanaochangia kwa hoja na kutuelimisha tulio wajinga wa sheria, uchumi, mikataba ya kimataifa na katiba yetu.
 
Du, kweli fadhila, mfadhili mbuzi hata mchuzi utakula.

Yaani yote aliyofanya SSH hata moja hulioni. Ngoja niishie hapa, maana kusema sana si kama mtu utakuelewa sana.
 
Kwangu chama chochote kikifa sawa tu, Cha msingi utanzania wetu.Mama Samia ni mzalendo wa kweli Sio yule mwenda zake
"Pendo hasegawa"

pamoja na kwamba umedandia uzi wangu nakushauri kama ungeanzisha wa kwako hizi point zingeelimisha wengi! Hapa ulipoichomeka wachache wataiona!
 
Back
Top Bottom