Excuses, ndiyo gundi inayomgandisha mtu katika confort zone yake. Huwezi kupiga hatua yoyote kimaendekeo, huwezi kubadili kitu chochote katika maisha yako kama ukichangua kusalia 'in your confort zone' Na njia rahisi ya kusalia humo ni ku make excuses.
Rais wetu ni muumini wa excuses. Sana sio kidogo. Nilimuona kipindi kile watu wanalalamikia kupanda kwa gharana za maisha zilizosababishwa na mfumuko wa bei kutokana na kupanda kwa bei za mafuta, RAIS akasimama jukwaani akaanza kutoa excuses. Mara corona, mara vita vya ukrain. Kwahyo baada ya kuambia raia hivo, she is confortable. Tutaishi hivi hivi mpaka i dont know when. She cant evern crack her mind tunatokaje hapa. Hali hiyo ikatuburuza.
Leo tupo kwenye mgao mkibwa wa umeme. Juzi nimemuona akitoa excuses tena. Ooh, tunarekebisha mitambo, oooh mabadiliko ya tabia ya nchi etc.. halafu katoa miezi sita asisikie kelele za umeme. Ndo keshamaliza hivo. And guess what, she is gonna go to sleep asubirie six months aulizie tena mmefikia wapi? The confort zone. Our president likes it in there.
Kuna haya maswali nadhani kila mwenye akili atakuwa kajiuliza ile siku madame anatoa excuses zake.
1. Ile mitambo inayofanyiwa ukarabati, yeye personally ameiona au analetewa tuu report mezani na hao anaowateua? Maana hii habari ya ukarabati tumeanza kuisikia mwanzo tuu mtoto wa makamba alivyo kabidhiwa ile wizara hadi leo.
2. Hii miezi sita aliyotoa, imetokana na uono wake juu ya hali halisi ilivyo kule Tanesco au ni hawa hawa wateule wamemletea mapendekezo hayo?
Na swali jingine binafsi najiuliza kila wakati. Hivi Mh. Kalemani alilikosea nini Taifa hili akapokwa ile wizara? Mbona he was going perfectly tu?
Kuna tuhuna zinasambaa mtandaoni. Kwamba mwezi March, mtoto wa makamba na maharage waliagiza Mtera maji yafunguliwe. Wawili hawa walitupilia mbali mawazo ya wataalamu kuhusu jinsi uamuzi huo ungeliingiza taifa katika upungufu mkubwa wa umeme. Kwamba kitendo hicho ndicho kimeliingiza taifa katika huu mgao wa umeme.
Inawezekana tuhuma hizi ni za kweli au la. lakini binafsi siwezi kuzipuuza kwa sababu kwanza Hayati JPM aliwahi kuli adress jambo hili publically kabisa. Huu mchezo wa kufungulia maji mtera ili nchi ikose umeme watu wauze majenereta. Pili mgao si huu hapa tunao? Je, kuwaondoa Huyo mtoto wa makamba na maharage pale nishati hakuwezi kuwa kunahusishwa kwa vyovyote na tuhuma hii?? Ikiwa hivo ndivyo, kwanini Rais anaanza kutoa excuses, kwanini asitoboe tuu ukweli na kutoa kalipio kali ikiwa ni pamoja na kuwatumbua moja kwa moja wahusika?
Rais anapaka paka rangi. Anamwambia mkurungenzi mteule wa Tanesco. ooh, maharage siju nini na nini, sijamtoa pale kwa sababu ya shida ya umeme, aikuwa anaenda vizuri, ukaendelee alipoishia. Seriously? Huyu Rais wetu anafanya Teuzi for fun! Yaani mtu pahala anafanya vizuri unaamua tu kumuondoa yani... she cant be serious. Yaani alikuwa ni kama anajikomba kwa maharage simchukie? Rais gani huyu?
Rais unapaswa kusema pale nimeona madhaifu 1,2,3. Nimemwondoa huyu sababu kashindwa ku deliver. Nakupa wewe hii kazi. Ndani ya mwezi nataka nione matokeo. Kama utaona huwezi nawewe uondoke. Finishi. Halafu uone watu watakavyo chakarika usiku na mchana ku meet target.
Nasema hivi. Rais akiamua kufanya kazi na watu kikazi, tatizo la umeme litakwisha ndani ya muda mfupi sana. Wala siomiezi 6 waliyompanga. Hata hilo bwawa la nyerere linalosemwa kila siku lipo 92%, haziongezeki tangu mwaka umeanza litakamilika na tutapata umeme wa uhakika. Ila kama ndo hizi teuzi za kirafiki, kishemeji anawachekea chekea wateule wake, miezi 6 itaisha na inchi itazidi kuwa gizani. Bwawa la nyerere litasalia kuwa 92% milele yote.
Mh. Rais, wewe umekalia kiti kikubwa sana katika taifa hili. Hupaswi kuwa mtu wa excuses. Ondoka kwenye confort zone. Fanya kazi fuatilia mambo. Hao watu unao waamini ndio wanakupotosha. Katika taifa hili umeme ni hitaji la msingi kwasasa. Taifa lenye ukosefumkubwa wa ajira, kila mtu anajaribu kufanya chochote kujipatia riziki. Katika harakati hizi umeme umekua ni nishati mhimu kuendesha miradi mingi ya watu. Hatuhitaji umeme kwaajili ya kuchaji simu tu. TUNA MIRADI INAHITAJI UMEME KUINGIZA PESA. NYINYI WATU MBONA HAMUELEWIII??....Aggggghhh😡