Usipende kuropoka ropoka tu ilimradi uonekane umezungumza. Kwanza uwe na adabu na heshima kwa Rais Wetu.
Rais Samia Ni Kiongozi ambaye kama Afrika ingekuwa ni nchi moja basi Rais Samia angechaguliwa kwa kishindo kuwa Rais wake.anao uwezo wa kuongoza Taifa lolote lile na likapata maendeleo makubwa kama tuliyoyapata.
Ndio maana ni katika uongozi wake tumeshuhudia ukamilishwaji wa miradi mikubwa mikubwa katika Historia ya Taifa letu ,miradi hiyo ni pamoja na bwawa la mwalimu Nyerere ambalo litatupatia megawati 2115 sawa na megawati zinazozalishwa katika mabwawa mawili ya kidatu megawati 204 pamoja na mtera megawati 80.
Ni Rais Samia ameweka historia katika macho ya watanzania kushuhudia treni ya umeme ikitembea katika ardhi ya Taifa lao.
Ni Rais Samia ameweka rekodi ya kutoa Elimu bure mpaka kidato cha sita kwa kutoa billion 33 kila mwezi,huku mikopo ya elimu ya juu ikitolewa kwa kila mwanafunzi mwenye sifa.ni Rais samia amekifanya kilimo kuwa kimbilio la watu baada ya kukipa thamani na kuja na kauli mbili ya kilimo ni biashara.pamoja na kupandisha bajeti kufikia Billion mia tisa 70.
Ni Rais Samia amewafanya watumishi wa umma kufurahia utumishi wao wa umma badala ya kuona kama ni kazi ya kitumwa.hii ni baada ya kuwapandisha madaraja kwa mserereko pamoja na kuwalipa malimbikizo ya madai yao.kutoa ajira kwa maelfu ya vijana.
Kujenga vyumba vya madarasa zaidi ya elfu 30 na hivyo kufanya katika Historia wanafunzi wote kuripoti shuleni kwa wakati mmoja.kujenga vituo vya afya kila kona ya nchi yetu .kutiririsha zaidi ya trilioni sita katika Secta ya Afya na hivyo kufanya huduma mbalimbali kupatikana hapa hapa nchini badala ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi ambako wanyonge walikuwa hawawezi kumudu gharama zake.
Kutoa zaidi ya Billion 250 kama Ruzuku katika kilimo kila mwaka na hivyo kupungua kwa bei ya pembejeo hususani mbolea.,kuongeza mapato kwa mwezi bila kukimbizana wala kufungia biashara za watu.kuimarisha uchumi na kujenga uchumi shirikishi ambao unawagusa watu moja kwa moja.
Kujenga miundombinu mbalimbali ya barabara katika kufungua fursa za kiuchumi.mfano kunakwenda kujengwa barabara ya njia nne kutoka igawa mkoani Mbeya mpaka Tunduma mkoani Songwe yenye urefu wa 237.9KM ambazo zitaongeza kasi usafirishaji,kuondoa foleni pamoja na kupunguza ajali za barabarani hasa za malori kufeli breki na kwenda kugonga magari ya abiria na madogo na kusababisha ajali na vifo,maana sasa kila magari yatakuwa yanapita njia yake.
Miradi ya maji Inaendelea kutekelezwa maeneo mbalimbali nchini.
Naomba niishie hapa. Nitarejea muda siyo mrefu